Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.

anakiimarisha chama, sasa hivi cuf imebakwa na maalim, Lipumba anarudisha heshima ya chama
 
Watu wengi wanapenda kufanya mambo kihisia tu
hawataki kutazama reality....Lipumba hata kama kanunuliwa na CCM..
akiweza kuwa na wafuasi tu basi ni tatizo
siasa ni watu na sio sheria...
Watu siyo hoja hata Rungwe, dovutwa wote hao wana watu.
 
Nawaambia Maalim Seif akipata urais nahama nchi kwa sababu ya usaliti na unafiki wake! Nawaambia hivi MTATIRO akipata ubunge ata udiwani naama nchi kutokana na unafiki wake!
 
Nawaambia Maalim Seif akipata urais nahama nchi kwa sababu ya usaliti na unafiki wake! Nawaambia hivi MTATIRO akipata ubunge ata udiwani naama nchi kutokana na unafiki wake!
Utaenda kukaa nchi gani Mkuu?
 
KUMBE KWELI, NDIYO MAANA....?

Prof Juma Kapuya alifundisha Botany pale mlimani, lakini kinachomtambulisha sasa ni ubunge wa Urambo Magharibi/Kaliua huko na uwaziri wa elimu, michezo, kazi,vijana, ulinzi nk.

Prof Philemon Sarungi alikuwa mzalendo wa kwanza kuwa bingwa wa fani ya mifupa, lakini hiyo haikumsaidia "kula nchi", badala yake "kilichomtoa" ni ubunge, uwaziri, ukuu wa mkoa, ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM.

Dr Mohamed Bilal ni mtaalam wa nuclear physics, lakini bado hakuonekana wa maana katika fani hiyo, hadi alipoingia siasa za ukatibu mkuu wakati huo Mkapa akiwa Waziri wa Elimu ya Juu,Sayansi na Technolojia,baadae uwaziri kiongozi, kugombea urais nk.Na sasa yeye na academics issues ndio basi tena

Dr Ali Mohamed Shein ni mwanasayansi mahiri tena katika fani yenye wataalamu wachache sana ya "molecular genetics", akiwa ameandika PhD thesis yake kuhusu "inborn errors of metabolism", lakini huko hakuona "utamu" hadi alipoingia kula nchi na wenye meno wengine kwenye siasa.Baada ya kifo cha Vice President Dr Omar Alli Juma,hakuwahi kugeuka nyuma.

Ukifanya "search" ya jina "Mark Mwandosya" kwenye google scholar utadondoshewa hints kibao za machapisho ya kisomi, na utashangaa kwa nini profesa kama huyu hakukaa chuo kikuu kufundisha na kuendeleza fani hiyo, badala yake yuko kwenye siasa!Kwanini hakutaka kurithisha maarifa haya na uweledi wake kwa vijana akazama kwenye siasa!?Jibu ni jepesi sana.....Maisha baada ya kustaafu!!Chapaaa!!

Wako wengine kibao kina Profesa David Mwakyusa,kina Dr Kadhege mzee wa LG100 wakaenda kuwa ma-DC huko Mbozi wakaacha taaluma zao kufundisha Udsm na wakawekwa kapu moja na kina Mulongo.Kuna kina Dr Kabwe S Kabwe,huyu ni daktari wa binadamu na Rais wa DARUSO-MUCHS(MUHAS siku hizi) enzi hizo.Kaacha taaluma yake na anakimbizana na vyeo vya kupewa,kajiweka kundi moja na kina Anthony Mtaka.

Gwiji wa Jiolojia Afrika,juzi tulivyopatwa na tetemeko Bukoba tukaambiwa moja ya changamoto ya GST sio mitambo tu,bali hata wataalamu wa fani hiyo,na kwa Tz wapo wawili tu level ya Phd..Mmoja ndio huyo Muhongo Sospeter,na yeye "kakimbilia" kwenye siasa na hataki tena kurudi kufundisha ili kuzalisha kina "Muhongo" wengine kwa vizazi vijavyo.Halafu unasema mtu azidi kusoma!!Usome nini wakati bongo siasa ndio kila kitu?

Mwingine alikuwa mwalimu wa Kemia.Alifundisha Organic Chemistry kwa madaha na staha.Akaongeza masters na baadae Phd.Kaukacha ualimu na hana mpango wa kurudi tena.Kazama kwenye siasa mpaka kufikia "cheo cha juu" ktk ulimwengu wa siasa.Ualimu umebaki kwenye vyeti na kumbukumbu tu.Anahimiza twende Isukamahela,Sikonge-Tabora kuongeza nguvu za walimu wa Sayansi shule za kata.Mhhhh...Nani aende na wao walikimbia?Vijana komaeni na siasa...Huko hakuna maisha.

Tujiulize, ni matatizo ya mfumo (hauwatunzi wataalamu wake) au ya elimu ya wataalamu hawa (wanashindwa kuitumia kuleta mabadiliko kwenye fani zao?) Maana kipimo cha kwanza cha elimu kuwa inafaa au la, ni jinsi inavyoweza kuleta mabadiliko kwa msingi wa malengo ya elimu ile. Sasa hawa wasomi wetu ni kwamba elimu imewatupa au wao ndio wameitupa elimu?

Miaka kadhaa huko nyuma,Prof fulani maarufu Tz alistaafu kazi,baada ya kufundisha kwa zaidi ya miaka 30.Akitoa magwiji na wataalamu mbalimbali.Mafao yake hayakuzidi milioni 100.Huyu ni Phd holder,mtaalamu mbobezi...aliyetumia akili na koo lake miaka nenda rudi.. hicho ndicho kiasi alichofungshiwa kurudi nacho nyumbani.Wakati huku Bungeni Jah People na Maji marefu wanakunja 200 baada ya miaka mitano tu.Unakaa unajiuliza...Hivi inakuwaje mtu toka UN-Habitat anakuja kukaa kundi moja la Kibajaji wa Mtere?Jibu ni pesa...Pesa rahisi rahisi ipo huko.

Ooh vijana mjiajiri...Fursa zipo kila kona...Hizo fursa mbona nyie hamzitumii?Mbona nyie hamjiajiri?Kila siku kukimbizana na vyeo vya uteuzi kwenye bodi za mashirika ya umma na nafasi za kisiasa.Wacha tubanane huko huko...Siku elimu ikilipa watu watahamia huko.

Emeritus Prof...Walau unapata mkwanja hata baada ya kustaafu kwa serikali kuthamini mchango wako.Huku ni kapa bin kwapa.Ndio maana si ajabu kumkuta Prof mstaafu wa Udsm akila part time RUCO na Makumila ili kuganga njaa...Wacha tubanane humu humu
 
Upuuzi kama huu ufanyike pale ccm muone kama kuna kibaka atabaki pale. Mijitu haijielewi ndio maana mnaburuzwa kama mkokoteni. Nawapongeza chadema kwa kuwa imara katika kukijenga chama chao.
 
Taswira Rasmi Za Mapokezi Ya Mwenyekiti Wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba | H@ki Ngowi
Uzuri wa Binadamu ni kusahau mapema sana! Lipumba sio wakupuzwa kiasi cha kumweka mtatiro apambane nae, inahitajika nguvu zaidi kupambana na Lipumba kuliko CUF wanavyofikilia,.

Na wakizubaaa kidogo tu basi ndo anawapiga bao, Magdalena Sakaya kajitoa kufa na kupona kumtetea Lipumba ikibidi hata kupoteza ubunge wake!


Bado mnaamini Mtatiro ndo size ya Lipumba? Hapo ni sawa na Fredi Mbuna unamweka amkabe Rhonaldinho
 
Huyu ndio mtu wa kupewa nchi kweli?
 
HUYO PROF PUMBA .....MPUUZ KWELI ANATUMIWA NA CCM KUKIANGAMIZA CUF..ILA ANACHOKITAFUTA ATAKIPATA

OVA
Muasisi wa hiko chama ni nani? kama ni lipumba basi ni cha kwake na anakitumia atakavyo
 

Naungana nawe huo ndio ukweli, maana suala LA Zanzibar sasa lipo masikioni Kwa jumuia za kimataifa. Hili litawaletea shida Kwa serikali ya Zanzibar. Cha kusikitisha sana anayetumika kuisambaratisha ni huyuhuyu aliyekuwa kila Mara akilalamika kuonewa na polisi Kutimwa na chama tawala, Leo yeye ndo yupo mbele. Haihitajiki akili kubwa sana kuona mzee wetu msomi kiwango cha PhD akifanya mambo ya kitoto, natambua Kwa usomi wake anauwezo Wa kuforesee the bad impact ahead, kila maadamu, mabomu kesha jifunga tayari kujilipua, hajali effect yoyote.
Inakera sana, ila malipo ni hapa hapa duniani, wasaliti wote wataumbuka.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…