Kama unakumbuka kwenye ule mkutano uliovunjika ilipigwa kura kama Prof. aendelee au vipi (kitu kama hicho). Kura nyingi zilizopigwa zilimkataa, waliomuunga mkono ni kama 14 lakini kulikuwa na kundi kubwa ambalo lilikataa kupiga kura. Hii kwangu naisoma kuwa hao wako nyuma ya Prof. Na inavyoelekea wengi ni wa bara na hivyo hivyo wasiomkataa wengi ni wa ZNZ. Ikitokea kila upande una nguvu basi - na naaamini ni hivyo CUF inatatizo kubwa. Bila kupatanishwa chama kinaweza ku-split. Ni wazi CCM watafurahia na kuchochea mpasuko utokee na UKAWA watakua hatarini. Mambo yakiharibika UKAWA (CDM, NCCR, na NLD) itabidi waamue waende na nani. Kwa siasa za sasa hivi huenda wakaenda na CUF zenj na kukawa na uhasama na CUF Tanganyika. Tuombe yasifike huku upinzani ukizorota ............