Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Tetesi: Prof. Lipumba awafukuza kazi wakurugenzi wote wa CUF

Status
Not open for further replies.
Duh, inabidi watafute njia ya kudeal na huyu jamaa kabla hajaleta further damage
Cause hali ikiendelea hivi, chama kinaonekana kiko on the edge ya kuparanganyika
Ila this prof should REALLY be ASHAMED of himself kwa huu ujinga anaofanya na kukubali kupelekeshwa kuharibu/dhoofisha chama ambacho amekuwa nacho na kukitumikia for years.
Big up prof pambana na mamluki wa chadema.
 
Kuna uhusiano wa katazo la mikutano ya ndani la police na kuruhusu kisha fujo hizi....
 
Kumbe matukio ya kina mtatiro yalikuwa ni mihemko tu??
Watu wanaposisitizwa KUFIKIRI wanachukia na kuporomosha matusi.
 
hali tete...
 
Attachments

  • 1474808138494.jpg
    1474808138494.jpg
    26.9 KB · Views: 23
Kwa hiyo hapa tunabadilisha habari....IPTL...ESCROW.....zinatulizwa kwanza...baada ya hapo...tunaendelea na biashara nyingine.
 
Sasa kila jambo mtakimbilia kuilaumu CCM.

Inawezekana ni kweli CCM kama Watazamaji wengine ukumbini wanaonekana kucheka kwa sauti ya juu kuliko wengine...lakini je mnataka CCM wafanye nini? walie.

Wakicheza Yanga na Ndanda, Mshabiki wa Simba atashangilia Ndanda au Yanga?

Hao jamaaa watwangane tu, hamna namna nyingine.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mimi sasa hivi simushangai prof Lipumba kwani ninajua amechanganyikiwa,ninaye mshangaa ni huyu mtu anayejiita jaij mtungi kuhalalisha shudu kuwa mbegu.
Huyu jaji ni kibogoyo yuko pale kimkakati kuakikisha vyama vya siasa vinakufa
 
Madai yao makuu wafuasi wa bara ni chama kujali siasa za Zanzibar zaidi
kutojali yanayotokea huku bara
hadi ruzuku na rasilimali kutumikia Zanzibar zaidi......
ni kama wabara wanaburuzwa...Seif kuwa kama ndo mwenye sauti ya mwisho kuliko yoyoye...
na sasa Mtatiro ni kama anatumika kuwa kibaraka....
Mkuu The Boss, Zanzibar ndiko kuna wabunge wengi wa CUF, idadi ya wabunge ndio inayofanya chama kipate ruzuku kidogo au nyingi. Lipumba anastahili lawama katika kuifanya CUF isiwe na wabunge wengi bara, anataka kuwatumia wafuasi wanaomuunga mkono kuficha udhaifu wake. Maana yake ni kwamba kule Zanzibar CUF wanapiga mzigo kwelikweli, tofauti na huku bara ambako Lipumba amekuwa akisaidia CCM tangu muda mrefu badala ya kupambana kwa ajili ya CUF. Unaweza kukumbuka kwamba ni Lipumba alitumia msikiti kuwashawishi Waislamu wampigie kura Kikwete (CCM) kuliko kuiingiza madarakani Chadema chini ya Dk Slaa katika uchaguzi wa mwaka 2010. Tungeonyeshwa kama mfano suala moja tu ambalo Seif "alilitolea sauti ya mwisho" tungeweza kuchangia kwa upana kidogo. Lipumba na wanaomtuma wanafahamu misimo ya Mtatiro, na usishangae kuona Lipumba inafikia mahali analindwa na bunduki ambazo zimenunuliwa kwa kodi zetu, kuharibu taswira ya upinzani! Nadhani umma sasa usimame kumkabili Lipumba, huyu Lipumba wa kuanzia 2010 ni hatari kwa upinzani hapa nchini!
 
Hatua hii kaichukua kwa madai ya kwamba anakisuka chama upya. Professor Lipumba kachukua hatua hii mara baada ya jana kurudi katika kiti chake ikiwa ni maamuzi ya msajili wa vyama vya siasa, ambaye kisheria ndio mlezi wa vyama vyote vya siasa!...

Katika kauli yake, kasema hii ni hatua ya kawaida katika kusuka chama ili kiendane na wakati na kujipanga kwa uchaguzi wa meya Kinondoni na Ubungo, na uchaguzi mkuu wa 2020...

Pia, Prof. Lipumba kawaonya wabunge wa CUF kuacha kurukia mambo na kasema watii katiba, sheria, na kanuni za chama hicho vinginevyo watapoteza nafasi zao

Hayo yakiwa yanaendelea kwa upande mwingine viongozi wa mpito wakiongozwa na Mtatiro na Maalim Seif wameitisha baraza kuu itakayofanyika siku ya Jumanne Zanzibar ili kutoa kauli ya pamoja ya kupinga maamuzi ya Jaji Mtungi
Hongera sanaa Profesa lipumba fukuza hao wasaliti wote ndani ya CUF! MTATIRO na MAALIM wamelikoroga waacheni walinywe utashirikianaje na Dikteta Mbowe na FIsadi nyangumi Lowasa
 
Duh???

Kumbe ndo maana watu wanauana na Machafuko huttokea.

Nilikuwa siyajuhi haya hata kidogo, Naacha rasmi kusoma naogopa kuitwa msomi kwa kauli hizi za Ki-Lipumba
 
Ni hatua nzuri kukisuka chama. Ili chama chochote kiwe na nguvu za kujidhatiti kimkakati ni lazima kuwa na kiongozi makini. Prof. Lipumba kaonesha umakini mkubwa. Ikumbukwe kwamba, Prof. Lipumba ndiye muasisi wa UKAWA baada ya bunge la katiba. Prof. Lipumba pamoja na Dr. Slaa walipinduliwa na CCM katika dakika za mwisho karibu kabisa na uchaguzi pale Edward Lowassa alipotumwa na CCM na kuwanunua baadhi ya wapinzani ili wamsafishe kuhusu kashfa ya Richmond. Ni Prof. Lipumba na Dr. Slaa pekee walioweza kujua mbinu hizo na kutamka hadharani kwamba uchqguzi utatawaliwa na CCM iliyojigawa pande mbili. CCM 'A' na CCM 'B'. Upinzani sasa unaweza kuimarika iwapo wapinzania halisi watarejea ulingoni. Dr. Slaa reja nyumbani uungane na mwenzako kwenye mapambano ya ukombozi wa mTanzania anayekosa haki zake za msingi. Maandamano sasa hayana mtu wa kuyazuia.
 
Mkuu The Boss, Zanzibar ndiko kuna wabunge wengi wa CUF, idadi ya wabunge ndio inayofanya chama kipate ruzuku kidogo au nyingi. Lipumba anastahili lawama katika kuifanya CUF isiwe na wabunge wengi bara, anataka kuwatumia wafuasi wanaomuunga mkono kuficha udhaifu wake. Maana yake ni kwamba kule Zanzibar CUF wanapiga mzigo kwelikweli, tofauti na huku bara ambako Lipumba amekuwa akisaidia CCM tangu muda mrefu badala ya kupambana kwa ajili ya CUF. Unaweza kukumbuka kwamba ni Lipumba alitumia msikiti kuwashawishi Waislamu wampigie kura Kikwete (CCM) kuliko kuiingiza madarakani Chadema chini ya Dk Slaa katika uchaguzi wa mwaka 2010. Tungeonyeshwa kama mfano suala moja tu ambalo Seif "alilitolea sauti ya mwisho" tungeweza kuchangia kwa upana kidogo. Lipumba na wanaomtuma wanafahamu misimo ya Mtatiro, na usishangae kuona Lipumba inafikia mahali analindwa na bunduki ambazo zimenunuliwa kwa kodi zetu, kuharibu taswira ya upinzani! Nadhani umma sasa usimame kumkabili Lipumba, huyu Lipumba wa kuanzia 2010 ni hatari kwa upinzani hapa nchini!

Siasa za nchi hii hata huyo Mtatiro usishangae nae ni 'wakala' tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom