Watu wengi wanapenda kufanya mambo kihisia tu
hawataki kutazama reality....Lipumba hata kama kanunuliwa na CCM..
akiweza kuwa na wafuasi tu basi ni tatizo
siasa ni watu na sio sheria...
Kuwa na watu siyo big deal, kama sheria na kanuni za chama haziko upande wako. Kama kuwa na watu tu ndiyo kilakitu Zitto asingeshindwa dhidi ya Chadema. Tatizo la CUF ni kwamba walifanya procedural mistake wakati Lipumba kaandika barua ya kujiuzulu. Walikalia barua ya Lipumba muda mrefu mpaka Lipumba akapata muda wa kutafakari/kushauriwa na kuja kuandika barua nyingine ya kubatilisha uamuzi wake wa awali wa kutaka kujiuzulu. Kisheria hapa Lipumba anaweza kuwabwaga CUF, unless CUF wathibitishe kwamba walipokea na kukubali maamuzi ya awali ya Lipumba kwa kufuata taratibu zote za chama; kitu ambacho CUF hawakufanya. Retracting your statement is legal; and Lipumba did just that, within time.