Wadau,
Katika kile kinachoonekana kwa mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Wananchi (CUF) kuipenda nafasi hiyo ambayo huenda alikula kiapo kwamba hadi allah atakapomuita basi aondoke akiwa katika nafasi hiyo ya uenyekiti, haijalishi ni wapi ila awe mwenyekiti tu! Yaani iwe kwenye siasa, vyama vya kijamii (kufa na kuzikana) au kwenye vigodoro lazima awe mwenyekiti tu!
Leo ameibukia hukooo kwa kiongozi mkuu wa chama, Hukooo! kwenye chama cha wazalendo ACT kwa lemgo la kuungana na akina M1, M2, sijui na nani mwingine vile. Vyanzo vya karibu vinatonya kuwa huko nako anataka uenyekiti. Sasa najiuliza Iron Lady aliyepeperusha bendera kwa nafasi ya Urais na kuweka historia ya kuwa mwanamke pekee Tanzania aliyegombea nafasi hiyo katika uchaguzi uliopita wa Rais, Wabunge na Madiwani. Je atakubali kumpisha Mzee wa Intarahamwe ili ashike usukani???????.....
Move ndo kwanza inaanza!!!!
Tusubiri Babu na yeye sijui atakuja na song la kutaka ukatibu!!!!!!!!