Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Tetesi: Prof. Lipumba kuhamia ACT Wazalendo muda wowote

Status
Not open for further replies.
Si jambo la ajabu sana kwenda huko maana wote kiitikadi (Zitto na Lipumba) ni sawa. Sale outs. Hakuna jipya. Kwa wasiolewa watashangalia lakini hii ni political strategy ya CCM kucheza na akili za watu. Ni dhahiri kuwa ACT ni CCM B na kipindi cha uchaguzi kina Slaa walipokuwa wanakaa Serena kwa siri akikutana na Mwakyembe na Lipumba kwenda vacation Rwanda halafu States sasa ni wakati wa kutumikia ruzuku waliozokula. Hamjiulizi Lipumba alikuwa wapi siku zote toka alipojiuzulu asidai ueneyekiti wake tena mpaka juzi na baada ya kuja tu CUF imesambaratika. Alikuwa kwenye mission kaitimiza.

Dhamira hapa ni kudhoofisha upinzani. Kitakochofuata Slaa nae atajiunga ACT na wale wachumia tumbo wa upinzani wote watakwenda huko pia kujifanya wanapigania nchi.

CUF tayari kuna mtafuruku ambao Lipumba ana mkono wake, CHADEMA napo hakukaliki kina Lema na Lissu kutwa wapo lupango, mwenyekiti anadhoofishwa kiuchumi, muda si mrefu watakuwa chali. Hapo sasa ACT wataonekana ndio tegemezi la wanyonge while in reality ni decoy tu.

Come 2020 aidha Lipumba ama Slaa atasimama kugombea urais ambapo in reality itakuwa ni CCM A versus CCM B na mshindi mnajua atakuwa nani. Na hii ndio Tanzania yetu ya kidemokrasia na amani tele............................
 
Ha ha ha haaa!..huko wanafaa wanaendana kabisa!..hilo litakua kundi la vinyonga.wanabadilika badilika
 
Naiona CUF ikifutika bara kwa kasi. Dhambi ya ubaguzi inawamaliza CUF.
 
WanaJF

Kuna tetesi zinasambaa kwa kasi kwamba aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof Ibrahim Lipumba anajiandaa wakati wowote kutoka sasa kutangaza kujiunga na ACT Wazalendo

Taarifa hizo zinazidi kubainisha kwamba mara atakapojiunga Mwenyekiti wa chama hicho Anna Mgwira atajiuzulu nafasi hiyo ili kumpisha Lipumba

Taarifa zaidi zitawajia hivi punde
Huko ndiyo kutamfaa sana na sasa timu itakuwa imekamilika haswa na act sasa wajiandae kukikosa hata kile kiti kimoja cha ubunge
 
Rekebisha usemi, sio aliyekuwa, bali ni mwenyekiti hadi sasa according to profesa mwenyewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom