Ndio Prof Lipumba lazima afie kwenye kiti,lazima agombee uRais hilo liko wazi jamaa yuko kimaslahi zaidi.
Zitto yuko kimkakati zaidi,yeye ni Kiongozi mkuu nguvu zote za chama ziko chini yake nafasi ya mwenyekiti ACT ni sawa na katibu mwenezi unapiga parapanda weeee mwisho wa siku Kiongozi Mkuu ndio mwenye kauli ya mwisho.
Prof Lipumba na Zitto lazima wataparangana kwasababu kila mmoja atapenda kugombea urais,kila mmoja atapenda ukuu wa chama na kuwa na kauli ya mwisho katika masuala yote ya chama.
Kwanini Zitto kakubali kumpokea Prof Lipumba,Mosi anajua ACT ipo Kigoma tu haina anafsi ya kufurukuta katika siasa za Tanganyika.Prof ana uzoefu wa fitna za siasa ana weza kuleta base kubwa ya wanachama wasiofikiri hasa wale wanywa ghahawa washinda vibarazani.Anafahamu kanda ya kusini hasa pwani CUF ilikuwa na base kubwa sana ya wanachama yamkini Prof anaweza kuondoka nayo.