Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Kura sio siri tena

Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Kura sio siri tena

Hatari sana hii
Mimi nadhani hii ni nzuri, ili litasaidia kwa wale wanaosema kuna kura fake zimepigwa na wakajifanya kwenda kushitaki mahakamani, kura zitaletwa na kuchambuliwa.

Ole wako ushitaki kwa sababu za uzushi na uongo lazima ufilisiwe kwa Usumbufu utakaokuwa umeusababishia mahakama na wahusika wengine!!!

Mpaka sasa sijaona ubaya wa jambo hili.
 
Ile karatasi yakupigia kura haina namba hawawezi kujua nimeiangalia kwa makini
kuna maandishi mengine ni madogo mno na mengine mpaka mwanga maalum kitengo kitayafanyia kazi wakati wa teuzi.
naunga mkono hoja ya lipumba namba zetu hazikupaswa kunakiliwa kwenye vishina.
 
Mnaeleta habari nusunusu lengo ni kupotosha hakuna lingine. Weka maelezo yote, weka ushahidi wa barua inayoonyesha kweli huyo alikuwa wakala, weka namba ya kituo, namba ya msimamizi wa kituo, na utambulisho mwingine wa eneo husika, pia mpe nafasi ya kujieleza kwa uhuru huyo 'wakala', muonyeshe kwa picha zilizo clear siyo zenye ukungu!!!
 
Kweli kabisa na mm nimeona hiyo kitu nilipokuwa nakabidhiwa karatasi za kura nikajua huu ni mchezo mchafu, jiwe anataka kujua wasiompigia kura ili badae awabane
 
Mnaeleta habari nusunusu lengo ni kupotosha hakuna lingine. Weka maelezo yote, weka ushahidi wa barua inayoonyesha kweli huyo alikuwa wakala, weka namba ya kituo, namba ya msimamizi wa kituo, na utambulisho mwingine wa eneo husika, pia mpe nafasi ya kujieleza kwa uhuru huyo 'wakala', muonyeshe kwa picha zilizo clear siyo zenye ukungu!!!
 
Mpaka sasa sijafahamu kama Mh Tundu Lissu ameshapiga kura au la maana sijapata taarifa zozote kuhusu yeye.
 
Wakala wetu kapigwa sana hapa Geita swali langu Je Huu ni Uchaguzi wa aina gani??
 
Hii naona imepangwa ili kuwatia hofu makada wa CCM & watumishi wa umma maana mtu kama mimi hata ukinitrace utanifanya nini sasa
 
Wakala wetu kapigwa sana hapa Geita swali zangu Je Huu ni Uchaguzi wa aina gani??
Hakuna haja ya kulalamika, vyama vyote vilikuwa na miaka mitano ya kudai tume huru ya uchaguzi vikawa vinauzunguka mbuyu, muda ukaisha wakakubali kuingia hivyo hivyo acha wapigwe.
 
Hakuna haja ya kulalamika, vyama vyote vilikuwa na miaka mitano ya kudai tume huru ya uchaguzi vikawa vinauzunguka mbuyu, muda ukaisha wakakubali kuingia hivyo hivyo acha wapigwe.
Utadai Tume wakati umefungiwa kufanya Siasa
 
Huu uchaguzi ni upuuzi kama upuuzi mwingine, na ndio maana watanzania wengi wamepuuza zoezi zima. Idadi ya wapiga kura ni ndogo kuliko maelezo kwenye vituo. Mambo kama hayo nani yuko tayari kwenda kushiriki huo upuuzi?
Akiandika namba zako hapo hapo unamgomea,lakini kutokujitokeza kupiga kura huo ni udhaifu binafsi,maana haiwezkani mtu uhangaike kupiga makelele siku ya kampeni halafu uchaguzi upotee usionekana,hautachinja hapo utakuwa umejichinja
 
Prof. Lipumba ameibua hoja nzito kuhusu USIRI WA KURA kwenye Uchaguzi huu...
Yeye kulisemea hilo wakati watu wakipiga kura tayari anashirikiana na CCM kuwatisha wananchi. Itawalazimu sasa kuichagua CCM ambayo ndiyo ina serikali.
 
Utadai Tume wakati umefungiwa kufanya Siasa
Walifungiwa kwa mujibu wa sheria ipi ?
Kuna wakati walikuja na UKUTA iliishia wapi?
Wanasema ujinga ni kurudia kufanya kile kile huku ukitegemea matokeo tofauti.
 
Back
Top Bottom