TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

Na sio mara moja. Kuna siku tulikutana kwenye hafla moja Mbeya yeye akiwa mgeni rasmi pia alisema hivyo kuwa yeye Prof anayemtambua hapa Tanzania ni Mark Mwandosya tu.

Ila tuache utani huyu Prof alikuwa zaidi ya kichwa. Ukisoma CV yake mmh.

Sema alikuwa na dharau sana ndio weakness yake.

R.I.P

Walikuwa marafiki na kuna kitabu kimoja nondo kweli cha Telecom wameandika pamoja...

"Control System Analysis and Design Using the Smith Chart", chapisho la mwaka 1990 toka Wiley
 
Hata mimi nilipokuwa UDSM, VC alikuwa Kuhanga, na Mzee Punch alikuwa amempa jina la "Octopus" kama sikosei; ninamkumbuka sana "Poacher" na Dean of Students "Akili Hana". Baada ya Kuhanga, alikuja Prof Mmari wakati nikiwa TA, na Luhanga akiwa ni mwalimu mwenzangu wa kawaida hapo FoE. Jamaa alikuwa mtu poa sana, niliwahi kusafiri naye kwenda kwenye Conference Harare, kweli anisaidia sana kama mwanae. Mwaka mmoja baada ya kutoka Harare ndipo jamaa akaanza kupanda vyeo haraka haraka hadi kufikia kuwa VC.

Eeh Mola, pumzisha roho ya Marehemu Luhanga pema peponi.
Bila shaka utakua Professor kwa Sasa au ndo unnasubiri uteuzi na ww kama Bashiru?
 
Kumbe humu Kuna Baba au Babu zetu.

Shikamoo mzee wangu na heshima kwako
Asante tupo pamoja, mbona mimi nimo miaka tu na "ban" nyingi ninazo hasa wakati ule wa uchafuzi.
Shule hiyo ilitoa wakurugenzi TRC (Mboma), TBS (Mwakyembe), Tanesco (Luhanga sr), Chuo cha Usafirishaji (Mbwanji) na VC Udsm (Luhanga jr) Katibu Mkuu Nishati (Mwakapugi). Hao wote walikuwa pamoja wakati mmoja.
 
Kumbe pale ilikuwa chuo cha TTCL? Aiseee zamani serikali iliwekeza,mbona siku hizi naona Kama kwenye elimu serikali Wala haiweki nguvu yeyote?
Siku hizi inawapa kipaumbele watu wenye vipaji maalumu kama Haji Manara, Cyprian Msiba, na Pierre Liquid
 
Hii machine ilinifundisha Electronics for Engineers second year Foe Engineering..

Mwana saa 2 kamili yupo mlangoni,halafu anawaambia ametoka airport ndio ameingia kutoka United States

Anavunja circuits kwa kichwa kwa hesabu za Laplace Transforms nilikua nabaki natoa macho tu..

Pamoja na umri ulikua umeenda ila kichwa chake ni something else
Sasa vijana CoET pale wanamkubali Manara zaidi kuliko huyo Prof
 
Asante tupo pamoja, mbona mimi nimo miaka tu na "ban" nyingi ninazo hasa wakati ule wa uchafuzi.
Shule hiyo ilitoa wakurugenzi TRC (Mboma), TBS (Mwakyembe), Tanesco (Luhanga sr), Chuo cha Usafirishaji (Mbwanji) na VC Udsm (Luhanga jr). Hao wote walikuwa pamoja wakati mmoja.
Heshima yako mzee wangu!
 
Hata mimi nilipokuwa UDSM, VC alikuwa Kuhanga, na Mzee Punch alikuwa amempa jina la "Octopus" kama sikosei; ninamkumbuka sana "Poacher" na Dean of Students "Akili Hana". Baada ya Kuhanga, alikuja Prof Mmari wakati nikiwa TA, na Luhanga akiwa ni mwalimu mwenzangu wa kawaida hapo FoE. Jamaa alikuwa mtu poa sana, niliwahi kusafiri naye kwenda kwenye Conference Harare, kweli anisaidia sana kama mwanae. Mwaka mmoja baada ya kutoka Harare ndipo jamaa akaanza kupanda vyeo haraka haraka hadi kufikia kuwa VC.

Eeh Mola, pumzisha roho ya Marehemu Luhanga pema peponi.
Nakupata vizuri.
 
dunia ni mapito tu lkn bado kuna baadhi ya watu wanawatendea binaadamu wenzao sivyo.
 
Hapa umejielekeza vibaya. Unajua u-vc wa Luhanga uliishia lini? Na je, ni lini TTCL College imeingia Udsm? Kwa hili pongezi ziende kwa aliyemfuata. Profesa Mkandala alifanya transformation nyingi udsm.
Hajatokea wa kufananishwa nae. Ndio alihakikisha TTCL college Kijitonyama iwe sehemu ya UDSM na ndio hii inaitwa CoICT vijana wanapata maarifa kwa viwango vya kimataifa hapa hapa nchini.

Professor wa kweli alieacha legacy katika Uongozi wa vyuo vikuu.
 
Huyu Prof bwana enzi zake akiwa VC UDSM alianza kozi ya Law hapohapo UDSM akadisco mwaka wa kwanza [emoji3]
Kivipi Mkuu? Huyo aliyem disco alikuwa na ujasiri wa kujifunika shuka moja na nyoka[emoji3][emoji3]
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye anasikitika kutangaza kifo cha PROF. MATTHEW LUHANGA, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia 1991 hadi 2006, kilichotokea jioni ya leo tarehe 16.09. 2021. Tunatoa pole kwa familia, Chuo chetu na Tanzania kwa ujumla. Taarifa zaidi tutaendelea kujulishana. Tumwombee apumzike kwa Amani. Amina.

Dkt. Dotto P. Kuhenga, Mratibu wa Mawasiliano na Habari, UDSM.

View attachment 1941008

=======

Professor Matthew Luhanga ndie Mwanasayansi wa Zama hizi mwenye historia iliyotukuka dunian
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye anasikitika kutangaza kifo cha PROF. MATTHEW LUHANGA, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia 1991 hadi 2006, kilichotokea jioni ya leo tarehe 16.09. 2021. Tunatoa pole kwa familia, Chuo chetu na Tanzania kwa ujumla. Taarifa zaidi tutaendelea kujulishana. Tumwombee apumzike kwa Amani. Amina.

Dkt. Dotto P. Kuhenga, Mratibu wa Mawasiliano na Habari, UDSM.

View attachment 1941008

=======

Professor Matthew Luhanga ndie Mwanasayansi wa Zama hizi mwenye historia iliyotukuka duniani
CV
yake si ya kitoto
 
Back
Top Bottom