TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye anasikitika kutangaza kifo cha PROF. MATTHEW LUHANGA, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia 1991 hadi 2006...

Apumzike kwa amani Profesa Matthew Luhanga.

Nyie serikali endeleeni kusimamisha uchumi wenu kwanza.

Kipaumbele chenu ni kusimika rais mwanamke 2025.
 
Nakumbuka siku moja tukiwa Mlimani UDSM, nilimsikia akisema alikuwa ana mheshimu Prof. Mark James Mwandosya tu!!!

R.I.P Prof. Mathew Luhanga!
Na sio mara moja. Kuna siku tulikutana kwenye hafla moja Mbeya yeye akiwa mgeni rasmi pia alisema hivyo kuwa yeye Prof anayemtambua hapa Tanzania ni Mark Mwandosya tu.

Ila tuache utani huyu Prof alikuwa zaidi ya kichwa. Ukisoma CV yake mmh.

Sema alikuwa na dharau sana ndio weakness yake.

R.I.P
 
Yes!!! Tanzania hakuna prof zaidi yake na mark mwandosya.
Wengine wanapeana tu.
Mtu akikusimamia afu anakuchukia ama hakupendi anatafuta sababu za wewe kukuangusha...
😆😆😆😆😆 asante sana!! Nakumbuka habari ya Prof. Magimbi na Marehemu Chachage Seith Chachage kuhusu machapisho yao!!, nafikili wakati wa kupata PhD mpaka wakakosana!!
 
Ameacha legacy duniani, Je! Mbinguni alijiandaaje? (Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu😉

Ufunuo wa Yohana 14:13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Kila la heri kwenye maisha yake mapya alioyachagua alipokuepo hapa duniani
 
Hata mm nilikuwepo siku hyo, alisema huwezi kuwa professor wa kiswahili au development study kisha ukajisifu eti ww ni professor! Nchi hii maprofessor tumebaki wawili tu mm na mwingine hayupo hapa anaitwa mark mwandosya" mbele ya jk na asha rose migiro nafikiri kulikua na uzinduzi wa coet kama kumbukumbu zangu ziko sahihi.
Oooh uko sahihi kabisa!😆😆😆😆
 
Pole Prof. Mark Mwandosya rafiki mkubwa wa marehemu...
Nafikili Prof. Mark James Mwandosya atakuwa anajiandaa kuandika risala fupi atakayomuelezea kwa ufupi rafiki yake Marehemu Prof. Mathew Luhanga kuhusu enzi zao at the HILL - UDSM na mahali popote walipokuwa pamoja!

R.I.P Prof. Mathew Luhanga!
 
Hajatokea wa kufananishwa nae. Ndio alihakikisha TTCL college Kijitonyama iwe sehemu ya UDSM na ndio hii inaitwa CoICT vijana wanapata maarifa kwa viwango vya kimataifa hapa hapa nchini.

Professor wa kweli alieacha legacy katika Uongozi wa vyuo vikuu.
Kumbe pale ilikuwa chuo cha TTCL? Aiseee zamani serikali iliwekeza,mbona siku hizi naona Kama kwenye elimu serikali Wala haiweki nguvu yeyote?
 
Hata mm nilikuwepo siku hyo, alisema huwezi kuwa professor wa kiswahili au development study kisha ukajisifu eti ww ni professor! Nchi hii maprofessor tumebaki wawili tu mm na mwingine hayupo hapa anaitwa mark mwandosya" mbele ya jk na asha rose migiro nafikiri kulikua na uzinduzi wa coet kama kumbukumbu zangu ziko sahihi.
Dah mbona jamaa alikuwa jeuri Sana.Ukiwa na mbongo kumbe unakuwa jeuri
 
Prof. Luhanga akiwa VC iliishauri serikali itilie mkazo sana kwenye elimu ya chekechea na msingi badala ya sekondari, kufeli kwetu kwenye elimu kunatokana na wanafunzi kuanza kujifunza kusoma, kuhesabu na kuandika wakiwa sekondari tofauti na enzi za mkoloni. Alitoa ushauri huo wakati huo baada ya kuona kiwango cha elimu ya wanafunzi wanaoingia chuo kikuu hairidhishi.
Ushauri huu sio wa kupuuzwa unapaswa kufanyiwa kazi
 
Hata mm nilikuwepo siku hyo, alisema huwezi kuwa professor wa kiswahili au development study kisha ukajisifu eti ww ni professor! Nchi hii maprofessor tumebaki wawili tu mm na mwingine hayupo hapa anaitwa mark mwandosya" mbele ya jk na asha rose migiro nafikiri kulikua na uzinduzi wa coet kama kumbukumbu zangu ziko sahihi.
Sahihi kabisa. Ilikuwa April 2006
 
Enzi zetu vc Mlimani alikuwa prof. Nicholas Kuhanga. RIP prof. Mathew Luhanga.
Hata mimi nilipokuwa UDSM, VC alikuwa Kuhanga, na Mzee Punch alikuwa amempa jina la "Octopus" kama sikosei; ninamkumbuka sana "Poacher" na Dean of Students "Akili Hana". Baada ya Kuhanga, alikuja Prof Mmari wakati nikiwa TA, na Luhanga akiwa ni mwalimu mwenzangu wa kawaida hapo FoE. Jamaa alikuwa mtu poa sana, niliwahi kusafiri naye kwenda kwenye Conference Harare, kweli anisaidia sana kama mwanae. Mwaka mmoja baada ya kutoka Harare ndipo jamaa akaanza kupanda vyeo haraka haraka hadi kufikia kuwa VC.

Eeh Mola, pumzisha roho ya Marehemu Luhanga pema peponi.
 
Back
Top Bottom