Prof. Mbarawa: Treni hii ya Tanzania siyo high speed train kama zile za vichwa vilivyochongoka, Wananchi eleweni hilo

Prof. Mbarawa: Treni hii ya Tanzania siyo high speed train kama zile za vichwa vilivyochongoka, Wananchi eleweni hilo

Bullet train ipo toka miaka ya sitini na ya kwanza ilijengwa na mjapani huku reli yake ni ya zege, sasa wewe unaposema ni tekinolojia ya kisasa nakuona uko kwenye kundi hasi la kutudanganya.
Kwa hiyo unataka kufananisha teknolojia iliyotumika kutengeneza bullet train ya mwaka sitini na latest edition ya hiyo train, wee jamaa sijui unatumia ubongo upi kufikiri...
 
Kwa hiyo unataka kufananisha teknolojia iliyotumika kutengeneza bullet train ya mwaka sitini na latest edition ya hiyo train, wee jamaa sijui unatumia ubongo upi kufikiri...
Sema wazi kuwa haukujua ilianza mwaka gani, hata hivyo toleo la mwezi wa kwanza haliwezi kufanana na toleo la mwezi wa kumi na mbili.
 
Na msemaji wa serikali alipost hizi picha za mabehewa vitumbua na kichwa kile cha kuchongoka...sasa mbona mnatuchanganya?

Mnajua sana kutupiga!
 
Ni kweli..lakini mbona kwenye picha zao za mwanzo hao TRC walituonesha kitu tofauti na tulicholetewa?
Huwa hauchukui muda angalau mdogo tu wa kukusanya maarifa kwa maana ya kujifunza tunakimbilia kwenye lawama na shutuma.
 
Mmeanza kubadilishana usemi. Kama sio high speed treni ina faida gani? Au mlifanya kuwaiga Kenya. Bora nipande Happy National Luxury dar to Mwanza kuliko hizo treni nikeshe njiani.
"Mmeanza" akina nani?!

Btw, ina maana gari linalotembea 80 to 100km/saa ni bora kuliko treni inayotembea kwa 160km/saa?!
 
Kama ni hivyo kwa Nini tunajenga reli nyingine.
Ina maana SGR ni sawa na Meter Gauge?! Ina maana huoni tofauti ya electrified SGR na Meter Gauge Railway?

Man, hiyo ni 160KM/HOUR. Hata likipiga 120km/hour, ina maana saa 2 nyingi inakuwa umeshafika Morogoro.

Within 12-15 hours unaweza kufika Mwanza. Je, hivi sasa Mwanza tunatumia saa ngapi?
 
Hila kwa nchi yetu na ukubwa wake Ni Bora wengejenga vipis vipisi angalau tuende hyo 250 had 320 kwa saa kuliko kujenga 160 kwa saaa na bado haitaleta tija ya kuwai
Chifu,

Asikudanganye mtu... high speed train ISN'T commercially viable kwa nchi maskini kama Tanzania!

Kabla ya yote, soma karipoti haka ka Australian Government:-
High Speed.png


Utaona hapo, gharama ya ujenzi tu ina-range from A$16M to A$110M. Now, fanya tu iwe US$20M/km.

Dar to Mwanza ni zaidi ya 1000KM... fanya tu iwe 1000KM X20M = 20,000,000,000

Yaani kujenga Dar to Mwanza peke yake ingechukua AT LEAST US$20 BILLION....

Hii ya sasa itachukua less than $8Billion lakini bado inatutoa jasho... je, huo ubavu tunao?!

Taarifa kama hiyo inafanana na ya World Bank waliyoitoa 2014 kwamba;-
The paper notes that construction cost of high speed rail in China tends to be lower than in other countries. China’s high speed rail with a maximum speed of 350 km/h has a typical infrastructure unit cost of about US$ 17-21m per km, with a high ratio of viaducts and tunnels, as compared with US$25-39 m per km in Europe and as high as US$ 56m per km currently estimated in California.
Gusa bei ya hizo treni zenyewe sasa....

Marekani na utajiri wake wote lakini bado high speed trains ni za kutafuta manake zipo sehemu chache sana!

Wenyewe wanasingizia ni teknolojia iliyopitwa na wakati kwa sababu, kimsingi wanaona hiyo speed hivi sasa inapatikana kwenye ndege
 
Sipingi usemacho, lakini kwa taarifa yako waliokuwa wanasema kuhusu hiyo reli ya umeme, walikuwa wanatuhadaa kuwa itakuwa high speed train. Na waliokuwa wakileta hizo computer image za high speed trains ni hao hao TRC! Imefika wakati wa ukweli kuonekana ndiyo wanaleta hayo mambo ya ajabu.
Hizo picha za TRC nilikuwa sijawahi kuziona lakini bado treni kama hizo zinaweza kutumia reli yetu kwa sababu zipo kama hizo ambazo sio high speed trains.
Lakini pia usisahau, ambavyo watu wanaponda sio treni bali mabehewa!

Point yangu ni kwamba, inawezekana kabisa kutumia hizo treni zilizokuwa zimeoneshwa na TRC lakini pia zikafunga na hizo behewa zinazopondwa ili kutengeneza madaraja ya abiria!
Na kwa kuongezea tu, hata hata hiyo train ya umeme wanayosema sio jambo la kauminika sana. Maana kama umeme wa nchi nzima umewashinda na bado wanakaza fuvu, ndio itakuwa umeme kwenye train?
Bhana wee... we acha tu! Ndicho nilichosema hapo juu kwamba maajabu ya nchi hii wakati umeme wa matumizi ya kawaida hatuna lakini tuna reli ya umeme.

Hata hivyo, bado sio mbaya kwa sababu suala la kuwa na umeme wa kutosha lipo ndani ya uwezo wetu sema ndo vile tu viongozi wenyewe wanatuangusha!

Binafsi, sioni ubaya wowote kwa kujenga reli ya umeme.
Unasema hizo train za high speed ni very expensive, kwahiyo $7.5b kwa mujibu wa figure zao ambazo haziamaniki, sio very expensive?
Hapo juu nimeweka ka-screenshot!

Wachina ndo wanaonekana highspeed train yao ndo wamejenga kwa bei nafuu ambayo ni $17M to 21M per km. Sasa fanya sisi tujenge kwa 20M/KM... Je, hiyo $7.5B ingejenga km ngapi?!

Kwa haraka haraka, ingejenga roughly 300KM na hilo ndo KISIO LA CHINI KABISA. Hapo hujagusa treni zenyewe!

Btw, hivi watu wanavyoponda hapa ni treni au mabehewa ya treni?
 
Funguka, zile picha za TRC zikionesha treni iliyochongoka na ubavuni jina la TRC aliweka nani? Kama hauvai barakoa utakuwa umeambukizwa uongo.
Sasa picha ndo railway?!

Issue hapa hizo high speed train zinapita kwenye reli ya aina gani...

Na nimekuambia SGR yetu inatumia reli zinazoweza kwenda hadi 160km/hour. Treni inaweza kuwa na vichwa vilivyochongoka lakini haimaanishi hiyo ni high speed train.

Kwa maana nyingine, hata zile picha ambazo TRC waliweka, treni za aina hiyo zinaweza kupita lakini haimaanishi ni high speed trains.

Aidha, hizo hizo ambazo zilioneshwa na TRC pia zinaweza kufunga mabehewa ambayo hapa yanapondwa kwa sababu, kimsingi hiki ambacho watu wanaponda sio treni bali mabehewa!
 
Kulikua na haja ya Mh Waziri kuja na hii kauli ya ufafanuzi kipindi hiki? Kwa nini?
Hiyo anajua mwenyewe kwanini katoa huo ufafanuzi...

Kwa bahati mbaya kabisa, hao wanasiasa wenyewe wala siwafuatilii. Na kama mtu angeniuliza waziri wa uchukuzi ni nani, basi ningejibu kwa kubahatisha!
 
Waziri wa Uchukuzi Prof Mbarawa amewataka Wananchi kutochanganya Treni hii ya Tanzania na zile za high speed zenye vichwa vilivyochongoka.

Prof Mbarawa amesema picha zinazorushwa mitandaoni na watu wasio na nia njema ni zile za high speed zinazotembea zaidi ya km 200 kwa saa.

Za kwetu ni hizi mnazoona tunazipokea na haya ni Mabehewa 14 ya Daraja la tatu(economy) na mwezi February mwakani tutapokea Ya Business class na First class

Mabehewa haya ni kwa ajili ya masafa marefu na yatavutwa na Vichwa vya Umeme lakini yale ya high speed Vichwa vyake vinaunganishwa direct na mabehewa, amesisitiza Mbarawa

Source ITV Habari
Vikiunganishwa direct na mabehewa,hiyo meli itakuwa na ukubwa Gani wa kuhandle cargo hiyo?Au ulimi uliteleza au Mimi ndio sijui
 
johnthebaptist hii nchi ni shida. Viongozi hutuona watanzania hatuna akili. Kulikuwa na sababu gani kutudanganya hapo mwanzo na picha za vichwa mchongoko?? Ila tukumbuke kilikuwa kipindi cha bwana yule, ambaye kudanganya ilikuwa ni sifa nzuri.
Pamoja na mapungufu bwana Yule,alitekeleza aliyotamka kwa ubora.kila wizi wa awamu ya sita unaelekezwa kwa bwana yule.si sahihi.mikataba ya mabehewa imesainiwa awamu ya sita.kama walibaini hawawezi kuleta Aina ile wasingeendelea kutuaminisha .je kuhusu malipo makubwa kwa mabehewa chakavu bwana Yule yupo?mwenda zake alishaenda bi mkubwa apambane na hali yake
 
Kila mtu ataubeba mzigo wake. Kila mtu ataamjni anachotaka kuamini
 
Chifu,

Asikudanganye mtu... high speed train ISN'T commercially viable kwa nchi maskini kama Tanzania!

Kabla ya yote, soma karipoti haka ka Australian Government:-
View attachment 2431487

Utaona hapo, gharama ya ujenzi tu ina-range from A$16M to A$110M. Now, fanya tu iwe US$20M/km.

Dar to Mwanza ni zaidi ya 1000KM... fanya tu iwe 1000KM X20M = 20,000,000,000

Yaani kujenga Dar to Mwanza peke yake ingechukua AT LEAST US$20 BILLION....

Hii ya sasa itachukua less than $8Billion lakini bado inatutoa jasho... je, huo ubavu tunao?!

Taarifa kama hiyo inafanana na ya World Bank waliyoitoa 2014 kwamba;-

Gusa bei ya hizo treni zenyewe sasa....

Marekani na utajiri wake wote lakini bado high speed trains ni za kutafuta manake zipo sehemu chache sana!

Wenyewe wanasingizia ni teknolojia iliyopitwa na wakati kwa sababu, kimsingi wanaona hiyo speed hivi sasa inapatikana kwenye ndege
Kwema hizo train ni ghali sana kuliko ghrama ya uwekezaji kwenye hiyo rail. Unakuta watanzania wanasema kitu flani ni ghali kuliko kila lakini ukichugulia unakuta ufisadi wa bilioni 50 zaidi. Marekani sio kwamba nimeshindwa ni priority tu .kama tumenunua drimliner. Bullet ya train zinatushindaje jamani
 
Back
Top Bottom