Mama mwenyewe kataka. Sasa kila kitu anapewa mwarabu.
1. Posta
2. Misitu
3. Bandari
4. KIA
Yaani mtu kutoka jangwani anakuja kutusimamia misitu yetu ili aboreshe kweli. Hii misitu tumepewa na Mungu sehemu nyingine hatujawahi gusa. Dah naomba Mungu anifundishe kunyamaza. Huku kwenye misitu wanataka
1. Meno ya tembo
2. Magogo
3. Madini
4. Wanyama pori
Mimi niseme kutoka moyoni. Mheshimiwa Rais kama anasikia au anasoma humu basi ajue umoja wa kitaifa umetikiswa sana katika kipindi chake kuliko wakati wowote tangu uhuru.
Mimi tangu nizaliwe nimekuwa mfuatiliaji wa siasa hatujawahi fikia hatua kama hii.
Namshauri mama kama kweli anaipenda Tanzania basi hii mikataba isitishwe tuanze mchakato upya kwa uwazi kama alivyo amua kuwa muwazi basi aendelee kwa uwazi hivi hivi tujenge umoja wetu wa kitaifa.
Sent from my Infinix X672 using
JamiiForums mobile app