KERO Prof. Mkenda suala la chakula Shuleni, limekuwa mateso na mzigo kwa Wazazi / Walezi, bora kipangwe kiasi fulani cha fedha kwa wote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Waislam hawafungi,bali hubadili ratiba ya kula toka mchana na kuhamishiwa usiku.
Na usiku hukesha wana kula kama viwavi.

Nakubaliana na wewe serikali ifanye cost sharing.
 
Binafsi sijawahi sikia watoto wakichapwa au kufukuzwa shuleni kisa mchango wa chakula, ila nimeona watoto wakishinda njaa kutwa nzima bila msaada kisa hawajachangia chakula.
Wapo wanao chapwa na kufukuzwa, wengine wanaenda na wazazi wao kabisa kujieleza.
 
 
Hakuna anayepinga bali uwekwe utaratibu bora zaidi na affordable kwa umma wote!
-Tunazungumzia maswala ya umma, hatuzungumzii maswala ya mtu mmoja mmoja!
Suala la chakula ni wazazi ndo wenye maamuzi,ukiona kuna shule wanakula it means wazazi walikaa kakao wakapanga hyo michango yote walimu ni wapokeaji tu na kusimamia tatizo nyie huwa mnawapa mzigo tu walimu,mfano mimi ni mwalimi kwanibwazazi mkiikataa michango ya watotobwenu kula ntapungukiwa nini???
 
Kuna walimu wana mtindio wa ubongo. Sasa unamchapaje mtoto kwa kukosa hela aliyotakiwa apewe na mzazi[emoji2960]
Mfano wewe ndo mwalimu,mmekaa mkakubaliana na wazazi watoe michango,watoto umewaagiza walete michango ama wazazi waje kutoa maelezo hakuna wanachotekeleza unafanyaje!????
 
Wapo wanao chapwa na kufukuzwa, wengine wanaenda na wazazi wao kabisa kujieleza.
Ni kwa sababu wao wazazi ndo walikaaa na kupitisha hyo michango hawakulazimishwa,kama wazazi hawatakubali kutoa michango nafikiri hata walimu pia watakuwa wamepunguziwa majumu ya ziada.
 
Shida ni kuwa ya nyuma ya pazia wengi hatuyajui. Serikali inawalazimisha wakuu wa shule wahakikishe watoto wale chakula shuleni. Mkuu wa shule/mwalimu mkuu hakutani na mzazi moja kwa moja anayekutana nae ni mwanafunzi hicho ndicho kinachotokea. Viongozi wanaweka pressure kubwa kwa hawa walimu juu ya chakula shuleni nadhani suala lingebaki hiari kwa wanaotaka lkn hii ya kulazimishana ndo inapelekea madhila kwa wanafunzi. Lakini pia wanafunzi wenyewe baadhi yao wanapewa lkn hawafikishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…