Yote tisa kumi, uliofaulu ulikuwa zamani(ingawa wasomi wenyewe ndio tunaleta haya ya kipuuzi) ila sio sasa.
Matokeo yalikuwa yanatoka yakipambwa na neno "PASS" huku ukipangiwa Kantalamba, Galanos, Umbwe, Musoma Tech, Tosa, Malagarasi, Ihungo, Milambo, Minaki, Bihawana, Makuyuni n.k
Siku hiyo hupati usingizi, kijijini unaonekana "King" ushatusua, salamu za pongezi kama zote kutoka kwa wazee.
Kwa sasa Mfumo wetu wa Elimu unahitaji mabadiliko makubwa sana, tunapoteza muda mwingi shuleni lakini tunachokivuna haiionekani.
Nawaza tu huyu kijana wangu sijui nifanyeje aje kuibukia kwenye soccer/football ambapo ukiwa na miaka 16 tayari ushatusua maisha.
Mfumo wetu wa Elimu rubbish kabisa