Prof. Mkenda, waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 kutoka shule ya msingi moja wote wamehamishiwa sekondari moja

Kumbuka shule za kata hazina boarding, unapomtioa mtoto kutoka shule ya msingi mbali na huna bweni utamuweka wapi?, point kuu hii
 
Hahahahaaaa, hizo ndio 'shule za kata'
 
Uko na ideas nzuri ili ziweze kutumika next time safi sana
 
Sasa wakibakizwa hapo na watao ingia la kwanza wakasome wapi?

Wameamua kuwapeleka kata hiyo hiyo ili isiwape wazazi usumbufu wa gharama
Hujaona swala la kuongeza madarasa?
 
Hii ipo vyema kwasababu tena hawaendi kutafuta new friends bali akili zinaendelea zilipoishia, hapo ndo wale waliokuwa wanaongoza wanapitwa na waliokuwa mkian elimu bana sijui kwanini
 
Msingi wana muundo tofauti na secondary.
Tukianzia Lugha, nidhamu, namna ya kufundisha, umri, peer group, nk.
Hatahivyo, kuwekwa pamoja hakuna ubaya ila si vizuri kuchanganya watu wenye makundi rika tofauti katika hatua za awali.
Una point lakini haina nguvu sana........kimsingi huu ni UJASUSI unafanywa kwa jamii ya kitanzania na matokeo yake huwezi kuyaona sasa ni baada ya muda kidogo
 
Shule za Serikali ni kwa ajili ya sisi watu wa chini japo sikusoma Dumu Fagio lakini , nimefundisha Dumu fagio niseme tu wanasiasa hawana Huruma
 
Kama una fedha, lolote linawezekana kwa sasa TAMISEMI NA SEKRETARIAT YA AJIRA.

Aliyeshindwa wizara ya madini kapewa TAMISEMI.
ALiyeshindwa TAMISEMI kapewa wizara ya AFYA.
 
Yote tisa kumi, uliofaulu ulikuwa zamani(ingawa wasomi wenyewe ndio tunaleta haya ya kipuuzi) ila sio sasa.

Matokeo yalikuwa yanatoka yakipambwa na neno "PASS" huku ukipangiwa Kantalamba, Galanos, Umbwe, Musoma Tech, Tosa, Malagarasi, Ihungo, Milambo, Minaki, Bihawana, Makuyuni n.k

Siku hiyo hupati usingizi, kijijini unaonekana "King" ushatusua, salamu za pongezi kama zote kutoka kwa wazee.

Kwa sasa Mfumo wetu wa Elimu unahitaji mabadiliko makubwa sana, tunapoteza muda mwingi shuleni lakini tunachokivuna haiionekani.

Nawaza tu huyu kijana wangu sijui nifanyeje aje kuibukia kwenye soccer/football ambapo ukiwa na miaka 16 tayari ushatusua maisha.

Mfumo wetu wa Elimu rubbish kabisa
 
Mbona huo mfumo ni wa muda kidogo tangu kuanzishwa kwa shule za kata, na ikumbukwe shule za msingi ni nyingi kuliko secondari hivyo waliofaulu wote kata husika hupelekwa shule iliyopo/ zilizopo kata husika

Kuna shule teule pia za wilaya na mikoa ambapo wapo wanaopelekwa huko pia

Kuna shule teule kitaifa kama mzumbe kibaha nazo hupokea kutoka mikoa mbali mbali
 
Tatizo lingine kina tunapotoa baadhi ya hoja mfano wetu ni Dar es salaam tuu au mijini, kijijini kuna shule tuu ndani ya kata husika zipo mbali sana na sekondari ya kata, na hakuna mabweni wala daladala za kulipa 200 kama Dar, huyo mtoto umpeleke nje ya kata yake si anaacha shule maana atafikaje KM 20, 30 huko
 
Kwanini wasingebakia hapo hapo msingi waendelee na kidato cha kwanza kwa shule ya msingi kuongezewa madarasa, walimu na vitendea kazi?

Hahahaaaaa
 
Kuna shule za kata alafu kuna shule ya tarafa elewa kwanza hapo

Shule A yenye watoto idadi fulani mfano 90 wakimalaza darasa la saba watoto wachache wenye ufaulu mzuri wataenda shule za vipaji kama kibaha,bwiru,tabora Mara hawa hutoka mwanafunzi mmoja au watatu kwenye shule moja

Then wanafunzi 5-20 hawa hupangiwa shule ya tarafa ni ya vipaji pia

Alafu ndio wanafunzi waliobakia wanapangiwa shule moja ya kata ambayo ipo karibu

KWANINI SERIKALI INAFANYA HIVI
ni kwa sababu wazazi wenyewe ndio walilalamika watoto kupangiwa shule za mbali na kwao hivyo serikali ndio ikaja na huu mkakati na umesaidia saana ufaulu

Huu mkakati ulianza mwaka 2011 kama upo makini kuanzia mwaka huo wanafunzi kwenye daladala walipungua
 
Na wote wapangiwe shule moja so kama ni ujinga na tabia za kijinga wanazihamishia kwenye shule mpya waliyopangiwa
Itakifia mahala. Ukifika la Saba unaanza la Kwanza tofauti ni Jina tu, itaitwa form One iliyokuwa la kwanza.

Maisha yamekuwa zaid ya abunuasi.

Hawa viongozi wanaharibu na kutuona hatuna sisi vichaa
 
Mwaka huu alijafanyika hilo kwa shule nyingi mno..kwa mfano wanafunzi wote wa Almuntazir girls wamehamishiwa form one Jangwani,wanafunzi wotee waliofanya mtihani St Augustin primary wamehamishiwa buguruni moto sekondary ukiangalia aina hiyo ya selection haiko sahihi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…