Responded Prof. Mkenda: Wanaopiga picha Shule zenye matatizo ya Miundombinu hawana nia mbaya, Watendaji wawajibike

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa wanaopiga picha shule zenye changamoto ya Miundombinu na kuzirusha kwenye Mitandao ya Kijamii hawana nia mbaya hata kama nia yao ni mbaya ila anachukulia hiyo ni njia ya Utoaji wa taarifa ili ifanyiwe

Prof. Mkenda ameyasema hayo Leo Jan 5,2026 Jijini Dodoma kwenye Hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa magari na vifaa vya Kidigitali Kwa walimu,wakufunzi na walimu wenye ulemavu

Pia soma:
~
Serikali yalalamikiwa, hali mbaya katika Shule ya Msingi Mbosho Wilayani Hai
~ Shule ya Msingi Ndoleleji ina miundombinu iliyochakaa na Walimu wasiowiana na idadi ya Wanafunzi

Prof. Mkenda amesema kuwa kutokana na changamoto hizo ambazo zimekuwa zikiibuliwa na watu hao sasa ni vyema jukumu Hilo likafanywa na Idara ya udhibiti ubora na kuzipeleka katika mamlaka za Halmshauri ili zipatiwe utatuzi

Prof. Mkenda amesema kuwa badala ya kulalamika kwanini watu hao wanapiga picha na kusambaza kwenye Mitandao ya Kijamii ila kinachopaswa ni kujiuliza walikuwa wapi wakati kitendo hicho kinafanyika

Aidha Prof. Mkenda amesema kuwa hakuna Halmshauri ambayo inashindwa kujenga matundu ya vyoo ya kutosha kwani kufanya hivyo utakuwa ni uzembe wa Mkurugenzi na madiwani ambao wanapeleka matumizi ya fedha sehemu zingine.

Watumishi wanaokimbilia kukanusha changamoto zinazoibuliwa maeneo yao ya kazi wawe wanachukuliwa hatua!

Juzi TRC ilikanusha mitandaoni kuhusu picha za daraja kule Moro,PM kaende mpaka pale Kidete na Mkurugenzi wao kakiri uharibifu umetokea!
 
20260103_091238.jpg
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa wanaopiga picha shule zenye changamoto ya Miundombinu na kuzirusha kwenye Mitandao ya Kijamii hawana nia mbaya hata kama nia yao ni mbaya ila anachukulia hiyo ni njia ya Utoaji wa taarifa ili ifanyiwe

Prof. Mkenda ameyasema hayo Leo Jan 5,2026 Jijini Dodoma kwenye Hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa magari na vifaa vya Kidigitali Kwa walimu,wakufunzi na walimu wenye ulemavu

Pia soma:
~
Serikali yalalamikiwa, hali mbaya katika Shule ya Msingi Mbosho Wilayani Hai
~ Shule ya Msingi Ndoleleji ina miundombinu iliyochakaa na Walimu wasiowiana na idadi ya Wanafunzi

Prof. Mkenda amesema kuwa kutokana na changamoto hizo ambazo zimekuwa zikiibuliwa na watu hao sasa ni vyema jukumu Hilo likafanywa na Idara ya udhibiti ubora na kuzipeleka katika mamlaka za Halmshauri ili zipatiwe utatuzi

Prof. Mkenda amesema kuwa badala ya kulalamika kwanini watu hao wanapiga picha na kusambaza kwenye Mitandao ya Kijamii ila kinachopaswa ni kujiuliza walikuwa wapi wakati kitendo hicho kinafanyika

Aidha Prof. Mkenda amesema kuwa hakuna Halmshauri ambayo inashindwa kujenga matundu ya vyoo ya kutosha kwani kufanya hivyo utakuwa ni uzembe wa Mkurugenzi na madiwani ambao wanapeleka matumizi ya fedha sehemu zingine.

Huwa najiuliza, wale waliokuwa wakaguzi wa shule waliokuwa wanapita mashuleni mara moja kwa mwaka au miaka miwili; sikuhizi hawapo tena?
kama bado wapo nafikiri ipo haja ya kuangalia upya hicho kitengo kama kina umuhimu wowote!
Haingii akilini mtu apige picha shule iliyojengwa kwa nyasi au watoto wamekalia ndoo darasani hadi wizara inashangaa...na kuna wanaojiita wakaguzi wanakula posho maofisini.....
 
nipo chuo kikuu fulan kinqjiita sijui ooh havard of africa leo ni siku ya tatu hatuna maji na miundombinu ya vyoo ni majanga bomba na sink zimeziba
 
Back
Top Bottom