Sikubaliani nae.
Katiba iliyopo sasa sio mbaya kihivyo, tatizo haifuatwi, kama viongozi wetu wangekuwa wanaifuata hii Katiba iliyopo kama ilivyo, hasa kuhusu masuala ya kidemokrasia, kama mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, hali isingekuwa mbaya kama ilivyo sasa.
Hata hii tume ya uchaguzi, japo Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama cha siasa anateua mwenyekiti wake, lakini hakuna popote huyu mwenyekiti na wajumbe wake wameambiwa na Katiba iliyopo waipendelee CCM, ni viherehere vyao tu, sasa kama watandelea na hii tabia ya kiherehere basi hata Katiba Mpya nayo ikija, haitakuja na suluhisho la kudumu.
Ningemuona Kitila ana hoja kama angeanza kwa kuwaambia CCM wenzake kwanza waifuate Katiba iliyopo, baada ya hapo, ndio tuangalie mapungufu yatakayojitokeza ili yakafanyiwe kazi kwenye hiyo Katiba Mpya, lakini kukimbilia Katiba Mpya wakati iliyopo mmeshindwa kuiheshimu ni ujinga.