Prince Kunta
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 22,797
- 28,904
Bipolar
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sikubaliani nae.
Katiba iliyopo sasa sio mbaya kihivyo, tatizo haifuatwi, kama viongozi wetu wangekuwa wanaifuata hii Katiba iliyopo kama ilivyo, hasa kuhusu masuala ya kidemokrasia, kama mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, hali isingekuwa mbaya kama ilivyo sasa.
Hata hii tume ya uchaguzi, japo Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama cha siasa anateua mwenyekiti wake, lakini hakuna popote huyu mwenyekiti na wajumbe wake wameambiwa na Katiba iliyopo waipendelee CCM, ni viherehere vyao tu, sasa kama watandelea na hii tabia ya kiherehere basi hata Katiba Mpya nayo ikija, haitakuja na suluhisho la kudumu.
Ningemuona Kitila ana hoja kama angeanza kwa kuwaambia CCM wenzake kwanza waifuate Katiba iliyopo, baada ya hapo, ndio tuangalie mapungufu yatakayojitokeza ili yakafanyiwe kazi kwenye hiyo Katiba Mpya, lakini kukimbilia Katiba Mpya wakati iliyopo mmeshindwa kuiheshimu ni ujinga.
Ukisaliti lazima utasalitiwa pia. Ni kanuni ya usaliti.This guy is an hypocrite......Sukumq Ghang sabotaging the Madame President
Pascal I ni muumini wa HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa iliyopo Kikatiba. HAKI ya MGOMBEA binafsi.Sasa hapo upinzani wasichoelewa ni nini? We naye una akili ndogo sana.
Chama DOLA kuondolewa Kwa SANDUKU la Kura 🙃🙃🙃🙃
Akili nawe inarudi polepole huku ukiuma na kupuliza. Ebu niambie ukiingia kwenye vikao vya Chama unayaongeea haya Paskali?Baada ya kutemeshwa meza kuu, sasa akili ndio zimeanza kumrudia gwiji huyu wa siasa na zitamkaa vizuri kabisa 2025 baada ya kutemeshwa rasmi jimbo la Ubungo na kulazimika au kurejea darasani kushika chaki, au kujiunga na akina sisi huku kujiweni.
Katiba inatoa haki ya kila Mtanzania kupiga kura kuchagua kiongozi na kuomba kuchaguliwa. Haki ya kuchaguliwa imeporwa na shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa!. Hii ni dhulma kubwa ambayo inatugharimu sana kupitia karma!.
Uchaguzi wetu ni uchaguzi kiini macho kugombea kisu cha makali kuwili, ambapo chama dola kimeshika mpini na vyama makapuku wakishikishwa upande wa makali kuwili!. CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
P
Napingana na dhana kwamba Katiba inayotakiwa ni ya demokrasia ya vyama vingi badala ya dhana kuwa Katiba ni ya wananchi, raia wa Tanzania kwa kuzingatia utamaduni wao na matakwa yao bila ya kuwa na msukumo wa kisiasa. Nalisema hilo kwa sababu tukiingiza mfumo ya vyama kwenye Katiba iko siku chama kingine kitaibuka na mfumo wake na kutaka katiba iliyopo ibadilishwe. Hivyo tunapojadili suala la katibu tusiingize mifumo ya demokrasia kwa kuzingatia vyama. Tuwaachie wananchi wenyewe waamue kama iliyopo inatosha au mpya. Lakini pia tusome historia ya nchi na katiba yake kuanzia utawala wa kichief na utawala wa kikoloni ndipo utajua katiba inatungwa ili kukidhi matakwa gani.Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotumika kwa sasa ni ya demokrasia ya Chama kimoja.
Amesema hali hiyo imechangia kuwa na demokrasia dumavu ambayo inapelekea kuchelewa kwa maendeleo, ambapo amedai kuwa kuna uhusiano wa demokrasia bora na maendeleo
Pia ameshauri kuwa Katiba mpya ni muhimu ili kuwezesha demokrasia ya vingi kustawi ambayo itawezesha wananchi kushiriki ipasavyo.
Amesema kuwa kwa mazingira ya demokrasia ya sasa ni rahisi kutabilika tofauti na ilivyo kwa Kenya, ametoa mfano kuwa ni rahisi kutabili kuwa CCM itashinda uchaguzi 2025 kwenye nafasi ya Urais, amedai kuwa hiyo inachangiwa na takwimu za matokeo ya Urais kwenye chaguzi zilizopita.
Prof. Kitila Mkumbo ameyasema hayo leo Septemba 15, 2022 katika mdahalo ambao umeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Nchini (LHRC) kwa kushirikiana na wadau wengine, katika siku ya demokrasia duniani ambayo imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka.
Mkuu unakosea kumdhihaki Prof kuwa akili zimeanza kumrudia, kwani hakuwa na akili alipokuwa na wadhifa ?Baada ya kutemeshwa meza kuu, sasa akili ndio zimeanza kumrudia gwiji huyu wa siasa na zitamkaa vizuri kabisa 2025 baada ya kutemeshwa rasmi jimbo la Ubungo na kulazimika au kurejea darasani kushika chaki, au kujiunga na akina sisi huku kujiweni.
Huyu ni yule Original au Copy yake?Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotumika kwa sasa ni ya demokrasia ya Chama kimoja.
Amesema hali hiyo imechangia kuwa na demokrasia dumavu ambayo inapelekea kuchelewa kwa maendeleo, ambapo amedai kuwa kuna uhusiano wa demokrasia bora na maendeleo
Pia ameshauri kuwa Katiba mpya ni muhimu ili kuwezesha demokrasia ya vingi kustawi ambayo itawezesha wananchi kushiriki ipasavyo.
Amesema kuwa kwa mazingira ya demokrasia ya sasa ni rahisi kutabilika tofauti na ilivyo kwa Kenya, ametoa mfano kuwa ni rahisi kutabili kuwa CCM itashinda uchaguzi 2025 kwenye nafasi ya Urais, amedai kuwa hiyo inachangiwa na takwimu za matokeo ya Urais kwenye chaguzi zilizopita.
Prof. Kitila Mkumbo ameyasema hayo leo Septemba 15, 2022 katika mdahalo ambao umeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Nchini (LHRC) kwa kushirikiana na wadau wengine, katika siku ya demokrasia duniani ambayo imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka.
Katiba inawekwa ijisimamie au watu waisimamie?Ukiona kitu hakifuatwi jua kina mapungufu.Katiba hii iliyopo ingekua nzuri isingetoa hisani kwa mtu kuifuatwa bali lingekua ni takwa kuifuata.Hiyo tume inafanya huo ujinga kwasababu inajua maamuzi yake niyamwisho nailo linaanzia kuanzia upatikanaji wake.nahilo linatokana na katiba yenyewe kutoa huo mwanya.kwahiyo hakuna haja yakujadili kitu chenye mapungufu ambayo tayari yameshaonekana wakati una uwezo na akili zakutengeneza kingine bora.katiba inatakiwa ijisimamie yenyewe sio hadi mtu anapojisikia au kukumbushwa.
Prof. Wa ukweli huwa hajali hayoWe mwache tu, hajui kuwa wanaweza mfukuza uanachama
No sijamdhihaki nimesema ukweli ulivyo, kuna viongozi ambao ni wajengaji hoja wazuri, Prof. Kitila is one of them, wakiisha lamba teuzi na kukaa meza kuu, akili zao wakapeleka kabatini, wakiisha temeshwa ndipo wanazikumbuka.Mkuu unakosea kumdhihaki Prof kuwa akili zimeanza kumrudia, kwani hakuwa na akili alipokuwa na wadhifa ?.
Kwa vile mteuzi ni binadamu, unapokuwa meza kuu ndio wakati muafaka wa kumsaidia na kulisaidia taifa na sio kufanya table manners za huruhusiwi kuongea wakati wa kula!.Kumbuka kwa nchi ukishapokea wadhifa ni lazima uendane na matakwa ya mteuaji, muhimu alichokisema ni sahihi hiyo inatosha kabisa.
Mkuu sasa hapo Kuna Prof kweli?Prof. Wa ukweli huwa hajali hayo