Prof. Mkumbo: Katiba iliyopo sasa sio ya Demokrasia ya Vyama Vingi

 

Attachments

  • VID-20220915-WA0092.mp4
    2.2 MB
Sasa hapo upinzani wasichoelewa ni nini? We naye una akili ndogo sana.
Pascal I ni muumini wa HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa iliyopo Kikatiba. HAKI ya MGOMBEA binafsi.

Kwa akili Yako kubwa Unadhani ndani ya CCM hawapo wapinzani makini ktk masuala ya kaki za kikatiba na kiraia??

Fikiri nje ya BOX pia Ili uwe HURU.

Ameeeen.
 
👇😁😁😁
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Akili nawe inarudi polepole huku ukiuma na kupuliza. Ebu niambie ukiingia kwenye vikao vya Chama unayaongeea haya Paskali?
 
Napingana na dhana kwamba Katiba inayotakiwa ni ya demokrasia ya vyama vingi badala ya dhana kuwa Katiba ni ya wananchi, raia wa Tanzania kwa kuzingatia utamaduni wao na matakwa yao bila ya kuwa na msukumo wa kisiasa. Nalisema hilo kwa sababu tukiingiza mfumo ya vyama kwenye Katiba iko siku chama kingine kitaibuka na mfumo wake na kutaka katiba iliyopo ibadilishwe. Hivyo tunapojadili suala la katibu tusiingize mifumo ya demokrasia kwa kuzingatia vyama. Tuwaachie wananchi wenyewe waamue kama iliyopo inatosha au mpya. Lakini pia tusome historia ya nchi na katiba yake kuanzia utawala wa kichief na utawala wa kikoloni ndipo utajua katiba inatungwa ili kukidhi matakwa gani.
 
Baada ya kutemeshwa meza kuu, sasa akili ndio zimeanza kumrudia gwiji huyu wa siasa na zitamkaa vizuri kabisa 2025 baada ya kutemeshwa rasmi jimbo la Ubungo na kulazimika au kurejea darasani kushika chaki, au kujiunga na akina sisi huku kujiweni.
Mkuu unakosea kumdhihaki Prof kuwa akili zimeanza kumrudia, kwani hakuwa na akili alipokuwa na wadhifa ?

Kumbuka kwa nchi ukishapokea wadhifa ni lazima uendane na matakwa ya mteuaji, muhimu alichokisema ni sahihi hiyo inatosha kabisa.
 
Huyu ni yule Original au Copy yake?
 
Katiba inawekwa ijisimamie au watu waisimamie?

Katiba ni maneno yaliyoandikwa kwenye makaratasi tu, watu/viongozi ndio wanaotakiwa kuhakikisha wanayasimamia hayo maandishi kwenye utekelezaji wake.

Sasa kama hao wasimamizi/viongozi wakiamua kutoyafuata hayo maandishi, ni nani atakayewezesha hilo kutekelezwa?

Ndio maana nikasema, tabia za kiherehere walizonazo viongozi wetu, kama wataendelea nazo kwenye Katiba Mpya, hali ya mambo haitabadilika.
 
Mkuu unakosea kumdhihaki Prof kuwa akili zimeanza kumrudia, kwani hakuwa na akili alipokuwa na wadhifa ?.
No sijamdhihaki nimesema ukweli ulivyo, kuna viongozi ambao ni wajengaji hoja wazuri, Prof. Kitila is one of them, wakiisha lamba teuzi na kukaa meza kuu, akili zao wakapeleka kabatini, wakiisha temeshwa ndipo wanazikumbuka.

Huyu ni hazina kubwa kwa taifa, alipaswa asaidie nchi wakati akiwa meza kuu, sasa suburia Prof. Kitila wa post 2025 atakavyokuwa anashuka na nondo na humu jf, atarejea!.
Kumbuka kwa nchi ukishapokea wadhifa ni lazima uendane na matakwa ya mteuaji, muhimu alichokisema ni sahihi hiyo inatosha kabisa.
Kwa vile mteuzi ni binadamu, unapokuwa meza kuu ndio wakati muafaka wa kumsaidia na kulisaidia taifa na sio kufanya table manners za huruhusiwi kuongea wakati wa kula!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…