Prof. Muhongo amuunga mkono Prof. Mwandosya, TCU kimya!

Prof. Muhongo amuunga mkono Prof. Mwandosya, TCU kimya!

Naona kila taaluma saa hizi imeingia michongo, kama msukuma, jaffo, biteko et al., nao wanatambuliwa kwa title ya Dr. basi nimeamua kutambuliwa kwa jina langu la awali bila kuweka title ya Dr. maana naona dharau zinazidi kwenye taaluma..........
[emoji23][emoji23]nchi hii kila mahali ni michongo tu kiasi mtu ukiitwa Dr flani watu wanakuchukulia wewe hamnazo Ile heshima iliyokuwepo hamna kabisa.
Hafu najiuliza mbona wabongo watu wanapendwa kuitwa Kwa ma title Yao mara Prof, mara Dr, mara engineer ila kwa wenzetu ni ngumu mtu kutanguliza title yake na hauwezi kujua labda sehemu husika tofauti na bongo ndio maana watu wanafanya udaganyifu huku ubunifu zero
 
Hao wazee huwa wanachukulia ongezeko la wasomi wenye PhD nchini kama threat kwao ndiyo huko kulialia na kuwabania wengine huko vyuoni

Yes,Wao wenye PhD zisizo na shaka hawana hata mchango wowote tangible kwenye jamii na huwezi hata kuwatofautisha na hao wanaowakomalia.

Heko kwa Prof Janabi.
 
Elimu yetu iko mahututi na bila kuivunja na kuunda upya tusahau kabisa maendeleo ya kweli katika sekta yoyote ile. Yaani tusahau kabisa.

Nina mengi ya kusema kuhusu elimu yetu kutokana na yale niliyoyashuhudia mwenyewe. Nitatafuta muda mzuri wa kuyasema.
 
... kwa maprofesa nguli kama hawa kuhoji, kuna kitu nyuma ya pazia! Ni jukumu sasa la mamlaka ya udhibiti wa elimu ya juu nchini (TCU) kutoa majibu fasaha. Kama kuna michezo wanasiasa wanafanya kuchezea elimu angalau wawili watatu wawe mifano kukomesha hali hii for good!

Wekeni hizo abstracts, conclusions, na supervisors online watu wapitie; hata hizo theses hazitakiwi kuwa siri. Ziwekwe public pengine watafiti wengine wangependa "kuanzia walipoishia" kwenye tafiti mpya.
Pamoja na hiyo nami nashauri ziwekwe "Online" Ili tu confirm plagiarism through TurnItin au Copyscape au plagiarisma
 
Ni vitu vya kushangaza sana. Musukuma tunaelewa hiyo takataka ameipata toka kwenye takataka huko India.

Yaani huyu Biteko na Jafo, ambao hata ukijadiliana nao, ni vigumu kufikiria wana viwango hata vya shahada za pili, leo eti wana PhD.

Kwa hili, UDOM imeonekana ni chuo takataka. Hata hao lecturers na professors wa UDOM, kuna taarifa pia hawana viwango vinavyotakiwa. Waligawana uprofesa na udokta kama mahindi ya kuchoma.

Kwanza wachunguzwe hao lecturers, pili hawa waliopewa PhD za michongo waundiwe tume ya kitaluma. Chuo kitazamwe upya, na kufanyiwa marekebisho makubwa ili kitoe elimu yenye ubora.
Hii post yako Bams itengezewe lamination halafu tuipeleke Ikulu kwa EMS
 
Mkuu si sahihi kufikiria hivyo.
Chuo Kikuu cha kwanza cha usomi duniani kilikuwa Timbuktu, West Africa, zaidi ya miaka 1000 iliyopita, fuatilia.
Na kilikuwa na mitaala ya kiislamu.
Sio kweli unajua Greece civilization wakina Plato, Aristotle, Socrates kabla hata ya kuzaliwa yesu walikua na shule wanafundisha.

Concept ya ujamaa Plato aliipigia chapuo, huku Aristotle akipigia upatu capitalism na nyingine nyingi

Hiko chuo Cha tumbaktu kilichokua kinafundisha si uislamu tu na hamna kingine in short kilikua ni seminary
 
Na PhD ya Dr AUCHO wa yanga tunaomba iwekwe hadharan pia

Hii nchi unaweza ukapewa uDr bila wwe mwenyewe kujua
 
Ni vitu vya kushangaza sana. Musukuma tunaelewa hiyo takataka ameipata toka kwenye takataka huko India.

Yaani huyu Biteko na Jafo, ambao hata ukijadiliana nao, ni vigumu kufikiria wana viwango hata vya shahada za pili, leo eti wana PhD.

Kwa hili, UDOM imeonekana ni chuo takataka. Hata hao lecturers na professors wa UDOM, kuna taarifa pia hawana viwango vinavyotakiwa. Waligawana uprofesa na udokta kama mahindi ya kuchoma.

Kwanza wachunguzwe hao lecturers, pili hawa waliopewa PhD za michongo waundiwe tume ya kitaluma. Chuo kitazamwe upya, na kufanyiwa marekebisho makubwa ili kitoe elimu yenye ubora.
Concur 100%
 
Bora Profesa Jay wa mitulinga alijitunuku mwenyewe uprofesa na kila mtu anamuita Profesa, alikuwa mbele ya muda
 
Jiwe Ndiye Chanzo Cha PHD Za Mchongo
Aliidhalilisha sekta ya elimu ya juu.
Iundwe tume kuchunguza vipi mtu ambaye hakuperform vizuri sekondari na hakukidhi viwango vya kuwa direct entrant University , bado "akakidhi" na kutunukiwa PhD ndani ya miaka 2!
 
Hivi wanajisikiaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Waziri mmoja wa Ulinzi wa Ujerumani kama mwaka mmoja uliopita aliachia ngazi ilipobainika alikuwa amenukuu kama para moja hivi bila kukiri hivyo (kuonyesha ameitoa wapi). Hakuishia hapo, chuo kilichomtunuku nacho kikafutulia mbali cheti chake. Haya ni mataifa ambayo elimu imekomaa wakati sisi ndiyo tunaanza kujikongoja. Hatuna sababu ya kufuata maadili yao katika elimu. Tuendelee na yetu mdogo mdogo.
 
Back
Top Bottom