SOma vizuri sheria ya CAG na Katiba ndipo ulewe. Zitto anadanganya kuwa hukumu ilikuwa dhidi ya Magufuli klumuondoa CAG kinyume cha Katiba lakini iwapo ulisoma hukumu ile ya mahakama yenyewe ilsema kuwa sheria ya Bunge iliyoweka kifungu kuwa CAG atafanya kazi kwa vipindi vya miaka mitano mitano ndiyo inayokiuka Katiba. Huyu jamaa aliondolewa kwa kufuata sheria hiyo ya Bunge. Na ukisoma vizuri sana utagundua kuwa Katiba ndiyo iliyoandikwa vibaya kwani inasema CAG atafanya kazi hadi afikie miaka 60 ila sheria hiyo ya Bunge iliyotumika kumuondoa yenyewe iliongeza umri huo hadi miaka 65. Kosa la Katiba ni kuwa iwapo mtu atateuliwa kuwa CAG akiwa na miaka tuseme 31 basi atalazimika kuendelea kuwa CAG kwa miaka mingine 30 au 35 kwa mujibu wa sheria hiyo ya Bunge, na sidhani kama hilo ndilo lililokuwa lengo la Katiba hiyo. Hakuna CAG ambaye amewahi kutumika zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano vilivyowekwa na sheria hiyo hiyo ya Bunge; yeye alitumika kipindi kimoja tu ambayo pia ilikuwa chini ya sheria hiyo kwani ilikuwa inaruhusu Rais kumteua tena au kuteua CAG mwingine, ambapo rais aliamua kuteua CAG mwingine.