Prof. Mussa Assad: Nilipokuwa ofisini niliomba nyaraka za SGR, Air Tanzania na mradi wa Stiegler's Gorge lakini sikupewa hata moja

Prof. Mussa Assad: Nilipokuwa ofisini niliomba nyaraka za SGR, Air Tanzania na mradi wa Stiegler's Gorge lakini sikupewa hata moja

Uongo ukiachwa ukawa mkubwa ,watu watauamin .

Assad yuko sahihi, nasasa anawafumbua macho watu sababu za yeye kutolewa nje ya ofsi

Mwachen asemeeeee,
Na amesema alipigiwa simu akaambiwa aitishe mkutano na waandishi wa habari akajibu siitishi,aliyempigia simu akamwambia lakini mimi ni boss wako ujue nakuagiza akamjibu kuwa mimi na wataalam wangu tumejadiliana tumeona hakuna cha kuongea kuongeza tena zaidi ya kilichopo kwenye ripoti hiyo kwahiyo sitaita waandishi wa habari

Aliyempigia simu akakata kwa hasira

NB: Hajamtaja aliyepiga simu ila tu alikua "boss" wake
 
Profesa Assad amefichua kuwa aliomba nyaraka za ununuzi wa ndege, reli ya SGR pamoja na Bandari ya Bagamoyo kwa kutumia technical reason lakini mkuu wa nchi wa wakati huo alikataa kuzitoa akawa anamtafutia sababu ya kumtoa ofisini.

Prof Assad amesisitiza kuna muda watu wanavunja katiba waziwazi lakini Taifa linashindwa kuwakosoa kutokana na hofu na uwoga.

Prof Assad amesisitiza kwa kukaa kwake ofsini alizihitaji sana hizo nyaraka ili azisome na atoe ushauri wa kibiashara kwani amefanya kazi hizo kwa miaka mingi kabla ya kuwa CAG kabla ya kuzikagua.

Prof Assad ametoa ushauri ni muda muafaka wa serikali kuweka nyaraka wazi kwa Raia wake ili wazichambue na kuboresha mapungufu kuliko Kuzificha Ikulu.

===

Wakati nipo ofisini, katika vitu ambavyo ninvitu vitatu: niliomba SGR, niliomba document ya Air Tanzania upya na niliomba project ya Stiegler's Gorge -- feasibility studies. Na sikupewa hata moja. Nilichopata ilikuwa ni barua kwamba mwaka haujamalizika na kwahiyo ukaguzi wa hesabu si wakati wake.

Na kila mtu mwenye akili alikuwa anajua nilichokuwa nataka kufanya si ukaguzi wa hesabu, lakini ilikuwa ni technical response ya kusogeza muda na kuniondoa katika reli tu. Kwahiyo, mpaka nimeondoka ofisini I never got that information na mpaka sasa hivi sijatafuta na sijasoma.

Wewe ni kama mimi. I'm a private citizen now. Ikitokea taarifa hii ipo wazi, tutaisoma na tutatoa commentary...
Amna cha maana hapo mradi ni mzuri sana na ni wa gharama nafuu.najua amwezi kunielewa kwasababu mnaamin kila wazo la asad ndo wazo sahihi
 
Alikuwepo Baba wa Taifa. Alilitumikia Taifa kwa muda mrefu kuliko Rais yeyote. Alikuwepo Mkapa, na wengineo kama mzee Kawawa, Aboud Jumbe, Abdul Wakili - wote wametangulia mbele za haki. Lakini hakuna ambaye baada ya kuondoka kwake, maneno yalikuwa hivi!!
Wacha kuongea vitu usivyovifahamu mkuu

Mkapa kapigwa maneno na mkewake akiwa hai hata hawakusubiri afe, JK tumemsema humu humu akiwa hai tena kuanzia yuko na rungu la madaraka mpaka kastaafu. Na tutamsema tu hata akiwa mfu,rekodi lazima ziwekwe sahihi. Awamu ya NNE ilikua miyeyusho tu, na hiyo ya 5 nayo wacha watu wachonge tu na Maza nae atasemwa pia mpk tukae sawa. Nchi yetu sote hii
 
Na familia ya Azory Gwanda, na ya Ben Saanane aliwaambia nini......
Na watu waliokufa na tetemeko la Kagera, alisema nini.....
Akafe mbele tu
Mimi siogopi kufa wala kuoza, ni lifecycle ya binadamu...
Kama unajua KIFO ni Hatma ya Binadamu basi uache kukejeli waliotangulia maana hata ww ni Mzoga Mtarajiwa. Umebeba mzigo mkubwa sana Moyoni, hope you find peace.
 
Kuna kitu hakiingii akilini. Unaposema aliomba maana yake ni nini? Huwa hatuombi nyaraka, huwa tunapewa nyaraja kufanya audit. Ukishaanza audit utakuwa uneshapewa kika unachohitaji, kimeandaliwa kabla hujaja. Wao pia ni wahasibu kama wewe, wanajua mahitaji. Isitoshe tayari una data za mwaka jana na mwaka juzi hii si audit mpya. Kama angesema aliomba nyaraja za SGR, zipi, akanyimwa ningeelewa, lakini alipisema aliomba za SGR NA za ndege NA za barabara nikajua si kweli, these are different audits. Na hasemi ni nyaraka gani, kwa sababu hata jina ni nyaraka, bajeti ni nyaraja, bank statement ni nyaraka, invoice ni nyaraka na risiti ni nyaraka unapewa moja kwa moja kutoka benki au kwa creditor hupitii kwa Magu. Na pale anaposema ana uzoefu na hayo mambo si kweli, ni wa chuo kikuu mtu wa library. Sitashangaa kama hata train hajapanda si mtu wa Bara.
Well said , ni kweli hayuko specific , nyaraka zipi aliomba . Anonekana ni mwenye hasira , chuki , kwa sababu hizo hawezi kuwa na balanced judgement ya anachokisema
 
Kama unajua KIFO ni Hatma ya Binadamu basi uache kukejeli waliotangulia maana hata ww ni Mzoga Mtarajiwa. Umebeba mzigo mkubwa sana Moyoni, hope you find peace.
Yaani hata niwe mzoga mtarajiwa baada ya hii post yangu, ni poa tu
I am as happy as pig in a clover
But that dead bastard was a cowardice killer, and I am happy to see the end of him
Now I can think about retirement in my homeland
 
Mwenda zake bana ameitafunavsana nchii hii ya wadanganyika.....sukuma gang mtaani tunaona walivyokuwa juu ya sheria na upigaji majumba yameota muda mfupi tu .....muda ni mwalim mzuri ......acha kazi iendelee
 
Mambo ya rada kipindi cha ben mkapa yalianza kama hivi, mwisho ikagundulika tuliibiwa fedha nyingi sana,tena aliyebumbulusha lilikuwa bunge la uingereza baada yakuona nchi maskini tunaibiwa fedha nyingi kiasikile.tuwakumbushe watoto kizazi hichi cha cd lile neno la chenge vijisent lilitokea kwenye sakata la rada
 
Kila mtu anajua hiyo Issue Ofisi ya NAO

Ilikuwa analazimishwa aitishe Press conference akanushe ile Scandle ya 1.5 Trillion pamoja na kukana udhaifu wa Bunge aliosema
Na amesema alipigiwa simu akaambiwa aitishe mkutano na waandishi wa habari akajibu siitishi,aliyempigia simu akamwambia lakini mimi ni boss wako ujue nakuagiza akamjibu kuwa mimi na wataalam wangu tumejadiliana tumeona hakuna cha kuongea kuongeza tena zaidi ya kilichopo kwenye ripoti hiyo kwahiyo sitaita waandishi wa habari

Aliyempigia simu akakata kwa hasira

NB: Hajamtaja aliyepiga simu ila tu alikua "boss" wake
 
Ukiwa Kiongozi you have only two options
1) Kubali kusemwa Ukiwa madarakani
2) Subiri kusemwa ukishaondoka madarakan

Nyerere na JPM walichagua option ya pili

Back
Top Bottom