Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
PROF NDAKIDEMI BADALA USHAURI ITUNGWE SHERIA WAZEE WAHUDUMIWE NA SERIKALI KWANI WALILIPA KODI. WATOTO WALIWATUMA MUWAZAE?
Anaandika, Robert Heriel.
Kila mtu ni Mzee wa baadae kama akipata nafasi hiyo. Lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Mtoto Hana jukumu wala wajibu wa kumtunza mzazi wake. Hiyo ni nature!
Ikiwa ni hivyo ni jukumu la kila mtu kujiandaa, kufanya KAZI kwa juhudi, kuweka akiba. Kupambana Kufa na kupona kwaajili ya Kesho take.
Kesho inayozungumziwa ndio huo uzee wenyewe.
Watoto hawakutuandikia barua tuwazae. Sisi ndio tuliona kuna haja ya kuwaleta Duniani.
Dini inatuambia mzazi mwema huacha urithi kwa watoto na watoto wa watoto wake. Ndio maana tunaambiwa tufanye KAZI siku sita kisha siku moja iwe mapumziko.
Kuna uzee!
Prof Ndakidemi, unatakiwa ujue kuwa mtu akifanya KAZI vyema, na sheria za nchi zikiwa za HAKI Bila kudhulumu watu haki zao.
Bila kuwalipa watu mishahara midogo, watu wanauwezo wa kujiwekea akiba bika kutegemea watoto.
Unapaswa wewe kama profesa ujue kwa nini wazee wa taifa lako wanazeeka wakiwa hawana akiba ya kujitunza.
Ulipaswa uishauri serikali iboreshe maslahi ya watu, wafanyakazi wa serikalini na sekta binafsi.
Ulipaswa uishauri serikali iwe Kali kwa watu wenye kuwafanya wananchi wa taifa hili cheap Labour. Walipwe vizuri ili wapate akiba ya uzeeni
Ulipaswa uishauri serikali namna ya kuanzisha na kushinikiza kila kijana anayefanyakazi kuwa na bima ya uzee ambayo atakuwa akikatwa kidogokidogo kama akiba yake ya uzee.
Sio utoe ushauri ambao hauna tija kwa taifa.
Yaani mtoto aache kuwaza mbele, aache kuwaza Maisha yake na watoto wake. Aanze kuangalia nyuma na maisha ya wazazi wake waliomzaa kama jukumu la lazima.
Lazima uelewe, Mtoto akishakuwa vizuri kiuchumi hawezj shindwa kulipa fadhila kwa waliomzaa na kumtunza.
Sheria uliyopendekeza haikupaswa kupendekezwa na Mtu mwenye kiwango cha Uprofesa.
Hiyo sheria huoni itazidisha uvivu na uzembe kwa vijana na kuzaa hovyohovyo bila mipango. Wakitegemea kuwa wakiwa wazee watatunzwa na watoto wao kama sheria yako ya kijinga uliyoshauri.
Wazee wasio na adabu watawasumbua watoto kuwapeleka mahakamani kuwa hawawahudumii. Jambo ambalo haliwezi kuwa Haki.
Ni wazazi wangapi wanatumia nusu ya maisha yao kufanya starehe wakitelekeza watoto wao huku wakishindwa kuwaandaalia watoto wao maisha ya baadaye?
Profesa! Profesa! Unatuabisha Sisi wasomi!
Kuzaa hukutumwa! Sikutumwa kuzaa!
Ukishazaa lazima ubebe jukumu la kuwalea hao watoto.
Lakini hao watoto hawana wajibu wowote kukutunza wala kukulea.
Watakulea kwa upendo na sio Sheria.
Na unajua upendo unakanuni zake.
Kama uliwalea kwa upendo ukawa muwajibikaji, ukawaandalia urithi, watatumia urithi uliowaandalia kukutunza. Na sio vinginevyo.
Elimu sio Urithi! Hilo kila siku tunasema!
Sio umemsomesha mtoto alafu unataka kusema ulimuachia urithi. Urithi gani? Unajua maana ya urithi wewe!
Zamani wazee walitoa elimu ya kilimo, ufugaji, uvuvi, uwindaji na kamwe hawakuita elimu hizo ni urithi.
Urithi ni Mashamba, Majumba, viwanja, miradi, magari n.k
Huo ndio urithi!
Mpe mtoto mradi, mwambie nimekupa shamba la Kiwangwa, heka 10, Lima kila utakapolima asilimia 30% ya utakachopata utaniletea hapa! Sabini utatumia utakavyo. Hiya 30% itumie kukutunza uzee wako.
Mwambie akishindwa kufanya hivyo utamnyang'anya. Na kumpa mwingine au kulikodisha kwa watu.
Mpe mtoto mifugo, labda ng'ombe 10 mwambie utakuwa ukileta asilimia 30 ya mapato yatokanayo ya ng'ombe hawa. Ukishindwa nakunyang'anya.
Unabiashara ya Duka, ushaona nguvu za usimamizi zinapungua. Mwambie mtoto 30% ya faida inayopatikana akutumie. Akishindwa hata mwezi mmoja unamnyang'anya.
Umeajiriwa, unachukua mamikopo kununua magari ya starehe yasiyozalisha, alafu ukizeeka uje usumbue watoto.
Nunua gari, MPE mtoto mwambie umemaliza chuo kikuu, Huna KAZI, chukua gari hii kapige UBA au Bolt. Niletee kila siku kiasi Fulani. Hicho kiasi kiweke Akiba ya uzee.
Hapo umemsaidia mtoto wako na kujisaidia mwenyewe na hiyo serikali yako.
Watu lazima wafanye KAZI. Hasa wanaume lazima kufanya KAZI.
Sasa mwanaume kutegemea kutunzwa uzeeni sio ishara nzuri, ni dalili ya uvivu na kutokuwa muwajibikaji. Ni kuongeza utegemezi kwenye taifa.
Mwanaume hapaswi kuwa tegemezi isipokuwa akiwa anaumwa tuu.
Lakini uzee haumfanyi mwanaume kuwa tegemezi.
Tena umepewa umri wa kutosha.
Ndio maana tunapigania HAKI ili kurahisisha mazingira ya utafutaji na uwekaji wa akiba ya Kesho yetu.
Mtu unasomesha mtoto za million mbili kwa miaka isiyopungua Kumi. Hela yote unaitoa kwa way wengine huko.
Alafu unashindwa kumuachia mtoto wako hata urithi wa milioni 10 aendeshe maisha yake. Alafu unataka akutunze, hivi kichwani kuna Moto kweli?
Wapeni watoto mitaji, au miradi waendeshe. Elimu pekee haitoshi.
Elimu sio urithi!
Profesa fikiria upya wazo Lako. Halina tija kwa taifa serious linalotaka kuendelea;
Acha nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam