Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Nafurahi kujua hilo sasa nitajiepusha kujipatia dhambi kwako mkuu.Asante Glenn
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nafurahi kujua hilo sasa nitajiepusha kujipatia dhambi kwako mkuu.Asante Glenn
Alikuwa jirani mwema sana.Very sad.
Alale pema peponi.
Hiyo ni lugha tuu wewe popomaKutuandikia kiarabu..kwani nani alimwambia humu kuna waarabu...vitu vingine upuuzi sana.
Anyway apumzike kwa amani prof.
#MaendeleoHayanaChama
na wee ni old timers??
We baba duh kumbe uwa tunabishana na wazee hapa duh I'm sory kama nilishakukwaza kwa loloteDuh!!!
RIP my college mate UDSM July 1972 - March 1975.
Yes, he a real gentleman.
Hajakufundisha huyu?ooh sorry kumbe wewe umesoma SAUTMuhimbili nao wana Uhaba wa Oxygen?
Ili jukwaa nimeanza kuliogopa[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]Aise kweli watu mmekula chumvi.
Hahahaha Vijana tukiwaambia mnatukanaga Wazee wenu hapa mnakuwa wabishiWe babu duh kumbe uwa tunabishana na wazee hapa duh I'm sory kama nilishakukwaza kwa lolote
DuhSo sad. On 20/12/2020 my classmate at Old Moshi sec 1970/71 form iv/vi passed away - Prof. Bakari Lembariti - MUHAS.
Leo college mate UDSM Prof. Mayunga Nkunya 1972 - 1975 tuliyekuwa naye hapo mlimani.
So sad. Najiandaa kuagana nanyi wana jf. Hii ndiyo reality.
Mkuu mwenyewe imeniumiza sana hii kitu nitaacha kujibishana na watu nikiwa na hasira hapaHuku kuna watu tunawavujia heshima, kumbe ni wazazi au wakubwa zetu sana
Ila wewe hatujawai kupishanaHahahaha Vijana tukiwaambia mnatukanaga Wazee wenu hapa mnakuwa wabishi
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna haja ya kubadilika hakikaMkuu mwenyewe imeniumiza sana hii kitu nitaacha kujibishana na watu nikiwa na hasira hapa
Nafahamu hilo Mkuu,kikubwa kupingana kwa hoja tuu bila matusi wala dharau.Ila wewe hatujawai kupishana
Ni professor anayeheshimika sn dunianiMwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Prof. Mayunga Habibu Hemedi Nkunya amefariki dunia leo Julai 20, 2021 katika Hosp ya Taifa, Muhimbili.
Marehemu Prof. Nkunya alikuwa Profesa Emerita katika Idara ya Kemia, Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi. Alianza kazi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Mkufunzi Msaidizi mwaka 1976. Alipandishwa vyeo vya kitaaluma hadi kufikia ngazi yaya mwisho kitaaluma ya Profesa, cheo alichokuwa nacho hadi alipostaafu utumishi wa umma mwaka 2012. Baada ya kustaafu Prof. Nkunya aliendelea na utumishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajira ya mkataba. Mwaka 2020 aliteuliwa kuwa Profesa Emerita kwa kuthamini na kutambua mchango wake mkubwa kitaaluma.
Prof. Nkunya alikuwa msomi na mwanataaluma mbobezi aliyetafiti, kuchapisha na kushauri katika maeneo ya kemia ya onaniki (organic chemistry) hususani katika kemia ya dawa asilia(chemistry of natural products).
Prof. Nkunya alitoa zaidi ya machapisho 100 katika majarida yanayoheshimika duniani na katika vitabu. Alishiriki katika kazi mbalimbali za ushauri ndani na nje ya nchi. Aidha alikuwa mwenyekiti/mjumbe katika kamati nyingi za kitaaluma na za ushauri.
Prof. Nkunya alishika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwemo Afisa Taaluma Mkuu cheo (sawa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma sasa) (1999-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(2007-2010); na Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki(2011-2015).
Mpaka anafariki alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania wadhifa aliokuwa nao kuanzia mwaka 2019 na Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi la Taifa kuanzia mwaka 2016. Mipango ya mazishi ya Prof. Nkunya inafanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na familia.
Mwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa siku ya Jumatano tarehe 21 Julai 2021 kuelekea Tabora kwa Mazishi.
Roho ya Marehemu Ipumzike kwa Amani!
Pole mkuu, mkuu na wewe kumbe umekula chumvi haswa? hongera snDuh!!!
RIP my college mate UDSM July 1972 - March 1975.
Yes, he a real gentleman.