Palamagamba has just admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory has “disappeared and died”.
Akihojiwa na mtangazaji Zuhura Yunus wa BBC, waziri Kabudi amesema Tanzania kuna uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari.
Alipoulizwa kuhusu kupotea kwa mwandishi Azory, Prof Kabudi amesema serikali inaendelea na uchunguzi.
Waziri amesema hali ya Kibiti na Mkuranga ilikuwa tete na haijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru wake.
Askari wa polisi, viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa chama tawala CCM waliuawa katika kadhia hiyo lakini kwa sasa amani imerejea na hali ni shwari.
Chanzo: BBC Dira ya Dunia!
UPDATES;
WAZIRI wa Mambo ya ndani Palamagamba Kabudi akiri mwandishi wa Habari Azory Gwanda alitoweka na kufariki, ikiwa ni zaidi ya siku 500 tangu kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari za uchunguzi.
View attachment 1150947