Prof. Patrick Lumumba: Tanzania chama cha siasa ni CCM tu hivyo vingine ni vikundi vya wanaharakati visivyo na Filosofia wala Falsafa

Prof. Patrick Lumumba: Tanzania chama cha siasa ni CCM tu hivyo vingine ni vikundi vya wanaharakati visivyo na Filosofia wala Falsafa

Huyu jamaa nilikuwa namuamini sana ila niliacha kumuamini siku ambayo nilimsikia akimzungumzia MAGUFULI na kumfananisha na akina Osagiefo kwame nkrumah, MAGUFULIFICATION
 
Mchambuzi wa maswala ya siasa duniani aliyesoma chuo kikuu cha Dsm Prof Patrick Lumumba amesema CCM ni chama cha siasa kilicho na filosofia na falsafa.

Prof Patrick amesema Chadema na Cuf ni vyama vichanga ambavyo bado viko katika harakati za " kutengeneza" filosofia na falsafa za taasisi zao ili viwexe kukubalika na kuaminiwa na wananchi kuwa ni vyama vya siasa.

Prof Patrick anasisitiza kuwa ukiangalia vyama kama Chadema na vyama vingi vya nchini Kenya ni vyama " Kinyonga" yaani vyama vya uchaguzi na wanachama wake wanachotafuta ni madaraka na siyo itikadi ndio maana wanahama hama vyama kutafuta ugali.

Source: Medani za Siasa Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Namkubali sana huyu Prof. Ila kila akiongea lazima niwe na The Longman Dictionary!
 
Lumumba is highly paid with this crooked ruling party to pave their way, waitishe tume huru, sisi majaji tupewe uhuru, ucgaguzi usimamiwe na wengine, hata serikali ya Somalia waone

Independent committee .../ and new constitution .....The medicine of ccm to stay too long in power
 
Siasa za nchi hii hazina haja ya kumsubiri msomi hata hasiyejua kusoma anaweza kosoa dosari ulipaswa kujua ni kwamba ili chama kipate usajili kinapaswa kutimiza vigezo gani[/QUOTE]
 
Sio unaongea kinyume? Maana sumu ya CCM ni tume huru, CCM hawana watu ila mamlaka I.e vyombo vya dola plus tume mbovu ya uchaguzi, While CHADEMA wana akidi ya kutosha ya watu
Mkuu, Habari!!

Ningependa Sana kujifunza kutoka katika maneno yako hayo

JE Ni kweli kwamba CCM ndiyo Vyombo vya Dola na Vyombo vya Dola ndiyo CCM?

Unauthibitisho ambao unaweza kuuweka hapa?

JE, Ni nini Maana ya Amiri Jeshi nchini?

Unadhani kwamba, ikiwa siku moja Chadema na Mungu jalia, ikashinda, inaweza Kufanya kazi bila Vyombo vya Dola?

Kwako mkuu
 
Mchambuzi wa maswala ya siasa duniani aliyesoma chuo kikuu cha Dsm Prof Patrick Lumumba amesema CCM ni chama cha siasa kilicho na filosofia na falsafa.

Prof Patrick amesema Chadema na Cuf ni vyama vichanga ambavyo bado viko katika harakati za " kutengeneza" filosofia na falsafa za taasisi zao ili viwexe kukubalika na kuaminiwa na wananchi kuwa ni vyama vya siasa.

Prof Patrick anasisitiza kuwa ukiangalia vyama kama Chadema na vyama vingi vya nchini Kenya ni vyama " Kinyonga" yaani vyama vya uchaguzi na wanachama wake wanachotafuta ni madaraka na siyo itikadi ndio maana wanahama hama vyama kutafuta ugali.

Source: Medani za Siasa Star tv

Maendeleo hayana vyama!
We kibwengu acha kuadvertise ujinga wako na vimaneno vyako vya kutunga ambavyo ni senseless kana kwamba jf wote humu ni mazombie wa lumumba watu wasiojielewa mavuvuzera
 
umekuja kumsaidia tumbiri kutukana ma professor ?
ahaa kumbe ndomaana chadema imekufa.
hivi mataahira kama wewe ndo yanapewa nafasi za kuongoza chama ?
matokeoyake mmewadharau ma prof akina safari na baregu chama kimeshikwa na macho ya kinyonga,lema,msigwa na mdee.

Pitia uzi wangu uone kama nimetukana kama wewe, achia mbali kuwa nimeandika kwa ufasaha.
 
Sio unaongea kinyume? Maana sumu ya CCM ni tume huru, CCM hawana watu ila mamlaka I.e vyombo vya dola plus tume mbovu ya uchaguzi, While CHADEMA wana akidi ya kutosha ya watu
kwani sie sio watu mpaka useme CCM haina watu? Kwa taarifa watanzania waliowengi hawachagui vyama bali wanachagua akili dhidi ya upumbavu. Mpaka muache wehu na upumbavu wenu ndipo mtachaguliwa. Msipo sikiliza ushauri mkabaki kuwaamini wahuni waendeshe chama, NCCR hiyooooo!
 
CCM sio chama cha siasa tena bali kundi la ugaidi tuu.
Chama cha siasa kinachofikia kumlisha sumu makamu mwenyekiti wa Taifa ili afe! Na ukiona Mambosasa ameshindwa kutimiza kauli yake kuwa aliyehusika atatafutwa baharini au nchi kavu basi ujue wahusika/mhusika ni watu wenye nafasi juu sana kuguswa.
Jee nani huyo/hao? Kama wenyewe kwa wenyewe wanauana watashindwa kuwaua wengine? Sasa hivi wanajifanya wameshasahau jambo hilo na mzee Mangula kafichwa
CCM ni mashetani menyewe kwa menyewe yanawindana kuuana yatakuwa na uchungu wowote kwa watanzania ?
 
Huyu profesa Ni sawa na Lipumba.Yaani Chadema ambayo imejizolea wanachama na ina falsafa yake,chama kunachopambana na vyama vingine ikiwemo CCM yenye kutumia dola na kila taasisi ya umma na ikabaki imara yeye anasema ni chama kichanga. Hapo kwao ni chama gani aweza kifananisha na Chadema? Kuhama vyama Ni jambo la kawaida sema kuhama na kukashfu uliowaacha ndo jambo la hovyo,Trump mwenyewe kahama vyama hata Leon Trotsky alihama chama.
Amesahau kuwa kenya hakuna vyama vya siasa bali kuna mafundi ya wanasiasa wanafanya ulanguzi wa madaraka
 
CCM ipi ? hii ambayo inategemea vyombo vya dola ili ishinde chaguzi.
 
CCM ipi ? hii ambayo inategemea vyombo vya dola ili ishinde chaguzi.
 
Huyu tapeli wa kisiasa amekuwa akikipigia upatu chama cha mapinduzi. Tapeli mkubwa
Huyo ana PhD ya Tanzania kama za wale wengine wa hapa waliojazana huko bungeni na Serkalini. Anajaribu bahati yake ya kuteuliwa kwa kuunga mkono juhudi na kusifia mpaka hivi karibuni alipewa zawadi alipokwenda Ikulu.
 
Back
Top Bottom