hapana uwezi kudanganya na wakati mambo yapo wazi jamaa.
chadema ya wakati wa dr slaa ilikuwa na nguvu na mvuto. polisi walizuia na kupiga marufuku mikutano ya hadhara lkn wanachadema wakataa na wakaingia barabarani kuandamana mpaka dr na mke wake walipigwa.mwisho ikabidi waruhusiwe.
sasa mazingira ya kipindi kile ni kama ya sasa,isipo kuwa chadema ya kipindi kile ilikuwa na maamuzi magumu na dr slaa alikuwa anaingia front line mwenyewe.
chadema ya mbowe kwa sasa haiwezi ingia front line kushinikiza waruhusiwe mikutano ya hadhara kwa kuwa haina mvuto tena,wala haina nguvu imekwisha.
chadema ya sasa imebaki jf.tweeter,kigogo na mange kimavi.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ngoja nikupe tofauti ya Chadema wakati wa Dr
Slaa na sasa. Wakati wa Chadema ya Dr. Slaa Rais alikuwa Kikwete. Sio kwamba Kikwete alikuwa mzuri sana, ila kwakuwa alikuwa anasafiri kwenda nje, ilikuwa ngumu kwake kuendesha siasa za shuruti kama ilivyo wakati huu wa Magufuli. Kwa vyovyote iwapo Kikwete angekuwa anafanya siasa kama hizi za Magufuli angejikuta kwenye wakati mgumu, maana dunia ilishatoka kwenye siasa za kishenzi na mabavu ya dola.
Naona unataja maandamano kama sifa ya kukubalika, kumbuka hayo maandamano ndio yalitumika kama silaha ya kuichafua Chadema kuwa ni chama cha fujo, na kinachotaka kuharibu amani ya nchi. Slaa mnayemvika kilemba cha ukoka hivi leo baada ya kuhamia CCM, ndio aliyekuwa adui mkubwa wa CCM na alioga matusi yote kwasababu hiyo ya maandamano. Hata hivyo hayo maandamano unayoyataja leo kama sifa ya kukubalika hayakufanyika zaidi ya mara 5, fujo nyingine zote za kuihujumu Chadema zilizofanywa na vyombo vya dola, zilifanyikia kwenye mikutano ya Chadema.
Tuje kwenye Chadema hii baada ya Slaa kuondoka, mwanzoni kulikuwa na maandamano ya ukuta, ambayo huyo Mbowe aliyasitisha baada ya kufundishwa siasa za kikondoo na Lowassa, kwa kisingizio kuwa hizo ni siasa za harakati, na hazifai kwa Chadema. Pia kulikuwa na maandamano kwenye uchaguzi wa marudio hapa jimbo la Mtolea, baada ya Chadema kufanyiwa hujuma za kutoapishwa mawakala wao, maandamano yale yalipelekea kifo cha Akwilina, na viongozi wote wa Chadema walioshiriki maandamano yale walibambikiwa kesi. Wakati huo huo mkurugenzi aliyegoma kuwaapisha hao Chadema mpaka leo anadunda, maana ana backup ya mwenyekiti wa CCM. Je maandamano yote ya Chadema wakati wa Slaa walikuwa na hizi kesi?
Tuje kwenye hiyo kupoteza mvuto hivi sasa kwa Chadema. Kinachoendelea hivi sasa ni hujuma za wazi dhidi ya Chadema, na zote hizo zinafanywa kwa maagizo ya mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais, kisa ana nongwa na chuki ya wazi dhidi ya Chadema. Kwa hivi sasa CCM ni kama haipo, na Chadema inaonekana kupambana kisiasa na vyombo vya dola na taasisi za kimamlaka, kuliko kushindana na CCM kisiasa. Hii unayoita udhaifu wa Chadema sio udhaifu wa kisiasa, bali ni udhaifu wa kupambana na vyombo vya dola kwani Chadema haina silaha, na wala sio kikundi cha kigaidi, na haitakiwi kufanya siasa kwa uhuru na sheria za nchi, bali itegemee hisani ya mwenyekiti wa CCM aliye na chuki ya wazi dhidi ya Chadema.
Huu unaouita uimara wa CCM kwetu ni kiburi na jeuri ya madaraka ya mwenyekiti wa CCM. Uimara huu wa CCM na mwenyekiti wake, ni sawa na huo aliokuwa nao Gaddaf, Mugabe, Elbashir nk walipokuwa madarakani. Viongozi hao kwa ajili ya jeuri na matumizi mabaya ya madaraka, walijiona ni viongozi imara, na vyama vyao vilipata uimara bandia nyuma ya matumizi mabaya ya madaraka. Leo hii tuwekee mrejesho wa uimara wa viongozi hao na vyama vyao baada ya hatua dhidi yao kuchukuliwa.
Na waliokuwa wapambe wao kama ww katika kutetea uovu wao, wapi leo ili waimbe uimara wa watu walioamini ni imara? Uimara wa CCM unaousema ww ni huo wa kutoka na maboxi ya kura vituoni, wasimamizi wa uchaguzi kufunga ofisi ili wasipokee fomu za wapinzani ili CCM imara ipite bila kupingwa!? Uimara wa CCM ndio huo sasa hivi wanashinda uchaguzi wa nchi nzima bila kushindana. Je wakati wa Dr. Slaa hiyo Chadema ikiwa na mvuto uliwahi kusikia CCM ikishinda nchi nzima bila kushindana? Sasa hivi chini ya CCM hii imara, viongozi wanapitishwa kwa amri ya mwenyekiti wa CCM, kwakuwa ni Rais, basi yuko juu ya sheria. Uchaguzi umegeuka ni sehemu ya kupimia ujinga wa mtu mweusi anaposaka madaraka!