Uchaguzi 2020 Prof. Rwekaza Sympho Mukandala: Hatma ya CCM 2020 bado haijulikani




Ujumbe utaishi na kukumbukwa sana na hata milele.
 
Atashinda tuu hakuna upinzani inchi hii. Leo hii kikao cha CUF kinafanyikia ofsi ya CCM.
 
Inaweza kuwa ya kawaida tu kama ilivyokuwa ya Mubarak,Mugabe au Iddi Amini Dada,Gaddafi ndo aliteseka kidogo lakini baada ya kuponda raha na utawala wa mkono wa chuma kwa miongo 4.

Ila sio mbaya ukiendelea kujifariji mkuu,uhalisia wakati mwingine ni mchungu sana.
Kwa vile yuko kibabe ngoja uone hatima yake.
 

Sawa.
 
Ili Hoja zako ziweze kukubalika na watu wengi, usiseme sana ya kwako ila rejea waliyosema na kutenda wengine.
Katika SHERIA, Mwanasheria, Wakili, hakimu au jaji anapotoa hukumu au utetezi hunukuu hukumu zilizotolewa huko nyuma zinazofanana na kosa analolitolea hukumu au utetezi.

Kuhusu maswala ya Kisiasa huko nyuma viongozi kama akiana mwalimu Nyerere waliwahi kusema:
1. Ukitaka kujua maendeleo ya Inchi, angalia maendeleo ya watu wake.

2. Fedha si msingi wa maendeleo bali ni matokeo yake. Kwa maana hiyo kama watu wanashindwa kufanya kazi ili wapate pesa au wanafanya kazi na kuzalisha lakini wanashindwa kuuza mazao yao na kwa hiyo kukosa pesa hii ina maana hakuna maendeleo.

3. You win the people through their stomach. Unawapata na kuwafurahisha watu kupitia mlo wa kila siku. Tukubaliane tu kuwa mambo yote yanayofanywa na Serikali iliyoko madarakani ni mambo muhimu sana katika uchumi wa Inchi katika siku zijazo na sasa.

Kizazi cha sasa kinaweza kisinufaike sana na miundo mbinu mingi inayojengwa sasa lakini hatuna budi kukubaliana na hali. Inabidi tuwe wapole na wenye subra katika kukubaliana na yanayofanyika sasa. Hakuna ubishi, Rais aliyeko madarakani atashinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao kwani ameonyesha kuwa ni mzalendo katika kupigania maslahi ya Inchi na hana mshindani anayetufaa na kuaminika toka vyama vya upinzani.

Rais aliyepita alitengeneza matajiri wengi na kuifanya Serikali kuwa fukara. Rais wa sasa anaifanya Serikali kuwa tajiri na matajiri kuwa mafukara. Hii ndiyo heshima ya Inchi yoyote Duniani. Haiwezekana watu na hata Mabenki yakawa na utajiri mkubwa kuliko Serikali. Inchi ya namna hii inakuwa haitawaliki na kunakuwa hakuna amani kwa sababu matajiri ndiyo wanakuwa watawala wa Inchi.

Kitu muhimu ni kuwa Rais wetu akimaliza awamu yake, hata kama bado tunampenda asikubali kubadilisha katiba ya Inchi ili apate nafasi ya kuendelea kuitawala Inchi.

Ameonyesha katika swala la gonjwa la Korona kuwa yeye hafuati wanayofanya wengine bali anafuata yale nafsi yake inavyomtuma kwa heshima yake na ya Inchi.

Ili heshima yake itukuke Duniani aondoke madarakani kama Katiba inavyosema na si kuibadili. Mwalimu Nyerere alitoka madarakani kwa hiari pamoja na kuwa Katiba ya Inchi bado ilikuwa inamrusu kuendelea kutawala na pia watu walikuwa bado wanataka aendelee kutawala.

Sasa anapata heshima kubwa Duniani kwa sababu ya hilo pamoja na kuondoka madarakani akiwa hana mali zozote alizolimbikiza.
 
Tumemsikia,ngoja tusubiri kutoka kwa profesa kitila. sisi tusiosoma tusije kusukumwa kuingia kwenye vita ya waliomo,na walioachwa nje.

Ila mimi kama mwanachi wa kawaida au baba mwenye familia, kipaumbele ni kuhakikisha wanafamilia wameshiba na watoto wanavaa na wanaenda shule, habari ya furaha mtu mmoja mmoja kwa nafasi yake anaweza kutafuta kutegemea hobi yake.
 
Kushinda uchaguzi CCM,CUF,ACT au CHADEMA hakutaisaidia nchi endapo watu watakaogombea hawatakua na nia ya dhati ya kumkomboa Mtanzania.

Mazoea ya kugombea ili kunufaika na malipo ya nafasi za uongozi yanadumaza uhalisia wa dhana na mifumo ya Uongozi wa kuleta maendeleo.

Wakati wa uchaguzi tuungane kama taifa kuwakata majina watu wasio na nia ya kutufanikishia Maendeleo yanayo tekelezeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…