Prof. Safari: Tume ya Warioba ifikirie kuingiza mahakama ya kadhi ndani ya katiba mpya

Prof. Safari: Tume ya Warioba ifikirie kuingiza mahakama ya kadhi ndani ya katiba mpya

Huoni kuwa Mahakama za Kadhi zitazipunguzia mzigo mkubwa sana Mahakama za kawaida ambapo zitakuwa na nafasi kubwa sana ya kushughulika na kesi nyingi kinyume na sasa hivi ambapo inapita miaka kwa kesi nyingine bila kushughulikiwa?

...nairudia tena point iliyoletwa: kwa utaratibu wa sasa hivi gharama za kushughulikia kesi za Waislamu katika mahakama za kawaida hugharamiwa na serikali!

Mbali na hasara nyingi za kichumi na kijamii,historia inaonyesha kuwa hakuna kitu kilichoundwa na serikali kikaaminika au kufanikiwa kwa waislam duniani kote.Hata ktk nchi za kiislam.Tanzania yenyewe Bakwata tumeoiona inavyoelea kisiwani.
 
Chadema inaunga mkono mahakama ya kadhi iendeshwe na waislam wenyewe sio na serikali inayotegemea kodi kwenye Bia, Sigara, Kondom, Guest houses, mabucha ya nguruwe n.k...Kwa kutaka Serikali iiendeshe hiyo mahakama ni kuinajisi.

Wabilah Tawfiq,
Mzito Kabwela
Kula like mzito kabwela.
 
Huyu anatafukuzwa any time. Chezea CDM

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huoni kuwa Mahakama za Kadhi zitazipunguzia mzigo mkubwa sana Mahakama za kawaida ambapo zitakuwa na nafasi kubwa sana ya kushughulika na kesi nyingi kinyume na sasa hivi ambapo inapita miaka kwa kesi nyingine bila kushughulikiwa?

...nairudia tena point iliyoletwa: kwa utaratibu wa sasa hivi gharama za kushughulikia kesi za Waislamu katika mahakama za kawaida hugharamiwa na serikali!
kwa hiyo mnalazimisha kupata ajira za serikali ili kutimiza malengo ya dini yenu, kwani serikali hii iliyopo ni Waislamu tu? mbona madhehebu mengi tu ya Kikristo yana mahakama zao, na hawadai zingharamiwe na serikali. Pamoja na usomi wako wote hulijui hilo, kwanini msigharamie wenyewe, mpaka mnahitaji msaada kutoka kwa watu ambao sio waamini wenu?
 
Akihitimisha hoja zake katika kipindi cha this week in perspective kinachoongozwa na Adam Simbeye (TBC) leo usiku saa 4 tarehe 14/06/2013, Prof. Safari amesema kuna mambo mawili yanayosababisha kutokuelewana miongoni mwa watu duniani; migogoro ya kidini na kugombea rasilimali.

Hivyo ili kuliepusha taifa la Tanzania katika migogoro ya kidini ni budi tume ya mabadiliko ya katiba inayoongozwa na Jaji Warioba ione uwezekano wa kuingiza mahakama ya kadhi katika rasimu ya katiba mpya! Kwa maoni yake ni kwamba nchi zote zinazotuzunguka zimeanzisha mahakama hizo, hivyo Tanzania haiwezi ikawa tofauti! Suala hili ni kwa maslahi ya ustawi wa Tanzania!
Hapo nyekundu ndo ameniacha.. Siamini Prof mzima aseme hayo.. hivi kila kinachofanywa na jirani yako ni lazima tuige??? Basi tuanze na vita vya wenyewe kwa wenyewe kama wafanyavyo majirani zetu wengi. Du! kama kweli yupo Chadema atakuwa mzigo usiobebeka.
Maoni yangu na ya wengi... mahakama ya kadhi isionekane kwenye katiba ya JMT, na ya Tanganyika. Kama ambavyo kuna madhehebu mengi Tanganyika. Vivyo hivyo na sheria zao na mahakama zao, hata wakitaka kwenye familia zao.. Sasa huyo msomi wa Chadema anatuambia nini? Asituchanganye bwana, kama keshanunuliwa, aseme.

Hata ungesoma kama ni muislam, tabia ya dini hii ni brainwash waumini wake, hivyo hata prof.Uislam ume ''mfine tune'' hadi kufuta kabisa uwezo aliozaliwa nao wa kufikiri nje ya box. hakuna cha ajabu kwa Prof. wa Kiislam kusema alichosema.kinyume chake angekuwa kama kunguru katikati ya njiwa, ukitafakari kwa makini,ni kwamba Prof. na usomi wake ameshindwa kutoa sababu kwanini,Mahakama ya kidini ya kiislam iwepo kwenye katiba ya serikali ambayo si ya kidini,ZAIDI SANA ANASEMA MAJIRANI KATIBA ZAO ZINA MAHAKAMA YA KADHI NDANI YAKE,hii sio sababu inayoweza kutolewa na msomi, lakini ni sababu ya kawaida sana kutolewa na Muislam na ni sababu nzuri na nzito kwa kadri ya Uislam na waislam walivyo. Hapa issue si kuwabeza au lah,bali ni kueleza ukweli,katiba inatoa uhuru wa kuabudu,uhuru huo ni pamoja na kuanzisha na kuendesha tasisi za kidini pasipo kuingiliwa na serikali,kwa waislam uhuru wa kuabudu ni uhuru wa dini yao kutambuliwa kikatiba,ndiyo sababu hata prof.kakanyaga taaluma yake in favor of Religion...ajabu kwa prof.wa Kiislam angesema kinyume cha Prof.safari alivyonukuliwa,kwa kusema alivyosema prof. kaonesha ukomavu wake wa kidini.Good prof.
 
Serikali ya ccm ilishasema suala la dini lifanywe na dini yenyewe! Sasa mambo ya kuweka kwenye katiba itakuwaje...
Catholic nao wana mahakama yao mbona haipo kwenye katiba...

Kwanza kiislam si sawa kupokea hela haram za kodi ya makafiri, kitimoto,pombe, sigara, dhuluma,wizi
Eti bana wafanye kesi zao wenyewe. Msione wakristo kimya mkadhani hawana sheria na mahakama zao. Tofauti ni kwamba wao wanatambua haraka sheria zao haziwezi kushughulikia kwa gharama ya serikali. Kwa mfano mkristo hawezi kumwacha mkewe hadi kifo au kuoa mke wa pili. Sasa hapo akikiuka kanisa haliwezi kumfunga jela ya serikali ila kumuadhibu kwa mujibu wa sheria za kanisa. Sasa ndugu zetu waislaam tunaomba uelewano haya mambo ya kadhi imeshaamuliwa yashughulikiwe na waislaam wenyewe na sio serikali. kwa hiyo namwomba prof. asiibue hii mada kwani iko divisive halafu waislaam wengi washaelewa.
 
Akihitimisha hoja zake katika kipindi cha this week in perspective kinachoongozwa na Adam Simbeye (TBC) leo usiku saa 4 tarehe 14/06/2013, Prof. Safari amesema kuna mambo mawili yanayosababisha kutokuelewana miongoni mwa watu duniani; migogoro ya kidini na kugombea rasilimali.

Hivyo ili kuliepusha taifa la Tanzania katika migogoro ya kidini ni budi tume ya mabadiliko ya katiba inayoongozwa na Jaji Warioba ione uwezekano wa kuingiza mahakama ya kadhi katika rasimu ya katiba mpya! Kwa maoni yake ni kwamba nchi zote zinazotuzunguka zimeanzisha mahakama hizo, hivyo Tanzania haiwezi ikawa tofauti! Suala hili ni kwa maslahi ya ustawi wa Tanzania!

Jadili!
nakubaliana kuwe na statement inayosema kila imani inaweza kuwa na mahakama ambayo hukumu yake itatambuliwa kisheria. Itaendeshwa na imani au kundi husika, kwa misingi isiyopingana na katiba, kwa gharama za kundi au imani husika. Maamuzi ya kupeleka kesi katika mahakama husika yatakubalika iwapo mshitaki na mshitakiwa wote watakubali kusuluhishwa na mahakama hio na si vinginevyo.
 
Prof.Safari naona safari yako ya kufukuzwa Chadema imeiwadia.
 
Mbali na hasara nyingi za kichumi na kijamii,historia inaonyesha kuwa hakuna kitu kilichoundwa na serikali kikaaminika au kufanikiwa kwa waislam duniani kote.Hata ktk nchi za kiislam.Tanzania yenyewe Bakwata tumeoiona inavyoelea kisiwani.
Basi tugawaneni nchi!
kmbwembwe said:
kwa hiyo namwomba prof. asiibue hii mada kwani iko divisive halafu waislaam wengi washaelewa.
Kwanza si kweli kuwa Waislamu wengi wameelewa!

Waislamu hawajaridhika na hili ni gogoro linalofukuta chini kwa chini ndio maana watu kama kina Profesa wanaliibua lijadiliwe ili lipatiwe ufumbuzi wa kudumu badala ya kujidanganya kuwa limeshaeleweka na Waislamu wengi halafu mkaja mkashitushwa na mshituko mkubwa.
 
Tatizo la nchi hii ni mfumo kristo uliyo asisiwa na nyerere ndiyo issue .
 
Basi tugawaneni nchi!Kwanza si kweli kuwa Waislamu wengi wameelewa!

India waligawana na Pakistani leo si tunaona tofauti..india inakwenda kataka mataifa makubwa kiuchumi..Pakistani imeshia ktk mapinduzi na ugaidi.

Akina Safari wakiamua kuchukua njia hiyo ya vitisho kuwa kama lisipoangalia matakuwa na machafuko atakuwa kawapotosha waislam big time,atawablackmail watanzania unfairly.

Kuna option moja ya kuwafanya waislam waheshimu sana dini yao, wazifaute sheria bila shuruti.Mwishowe itakuwa km katoliki,,,katoliki waumini wanajituma sana na wanahofu ya sheria zao...kubatizwa, kupata kipaimara, mazishi na ndoa...huwa lazima muumini apate barua ya jumuia(kikundi cha sala km vile nyuma kumi ki CCM) anaposhiriki.Na wanajituma na kuzikubali sheria bila shuruti.Wale wanaokaidi na kuahama kanisa au dini ni wale wakorofi ambao si kondoo wa hilo boma.
 
Tatizo la nchi hii ni mfumo kristo uliyo asisiwa na nyerere ndiyo issue .

Hata mi mimi nafikiri hivyo ndio maana wanajenga shule nyingi, na makanisa mengi na kuyachoma baadaye, ndio maana wanawaambia watoto wetu wachore nyeti na kunadika nyimbo za kiana diamond ktk mitihani ili wafeli....ndio maana wanawashawishi wengine wawe buse kubudni staili mpya ya kulalamika na kufanya mauaji na kulipua mabomu.huu mfumo umefikia pa kuwafanya watu wawe wavivu na mafisadi ktk hazina yao hela.
 
Prof.Safari naona safari yako ya kufukuzwa Chadema imeiwadia.

Pengine badala ya huu ushabiki, mngemwomba akakae na kuja na new Plan ya kuwasaidia waislam kuwa na njia bor aya kutumikia dini yao,bila kutumia hela za kodi ya makafiri, kodi za pombe na sigara ambzo ndizo zinaendesha serikali ya kina Sultan Alhaj JK.Na ziweze endeshwa kwa zakat na michango halali ya waislam.

Yule ni prof...Marekani walimhitaji prof ..mmoja abuni indoor game ..akabuni Basket Ball.Kwanini waislam wakose namna ya kua accomodate sheria zao ktk jamii mchanganyiko.Kama saccos,vyama vya ushirika, makampuni yanaweza kuwa na sheria zao na maisha yanakwenda,watu wanaandhibiwa bila kuhusisha taasisi zingine.Kwanini uislam ulioanza kabla ya serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania utake kupangia na sheria za nchi hii?

Hakika nakuhakikishia Mahakama ya kadhi ikipita waislam mtakuwa watumwa sana kwa makafiri zaidi ya mnavyodhani,kam Bakwata tuu ambayo haina interest kubwa kwa wengine inawaogopesha waislam,mahakama ya kadhi sijui ?Kuna masheikh watanunuliwa sana,watapangwa na kupangiwa cha kufanya kwa kasi na nguvu za ajabu.

Si bisara sana prof ..akachukua njia nyepesi ya kufuata mkumbo badala ya kuongoza watu,kufikia jamii ya kiislam inayoheshimu na kuyaenzi mafundisho ya dini.Ikifikia hapo ni wazi anayekwenda pembeni hakustahili kuw ammoja wenu.
 
Mtei atamvua uanachama shauri yake! Ukiwa huko ni Marufuku, Strictly prohibited kutetea Waislam ikibidi unaruhusiwa kuwa Wakili wa Serikal kwa muda, Slaa kwenye ishu ya Sensa na MOU alijikabidhi kazi ya kuwa mtetezi wa serikal, namshauri huyo Prof kuhakikisha vigezo na masharti ya kuwa huko vinazingatiwa!

Umeishia darasa la ngapi??? Inaonekana hata ufahamu lolote; si urudie darasa kama mwenzako mwigulu alivyokuwa anasomea majina ya wengine??? Yaani una tofauti na wale wanaofikiri kwa kutumia makalio
 
Basi tugawaneni nchi!Kwanza si kweli kuwa Waislamu wengi wameelewa!

Waislamu hawajaridhika na hili ni gogoro linalofukuta chini kwa chini ndio maana watu kama kina Profesa wanaliibua lijadiliwe ili lipatiwe ufumbuzi wa kudumu badala ya kujidanganya kuwa limeshaeleweka na Waislamu wengi halafu mkaja mkashitushwa na mshituko mkubwa.
Sadeek kugawana nchi haiwezekani kwani tumechanganyika kidini kijiografia, kikabila, na sehenu zingine hata kiukoo. Ndio maana ili kuendelea na amani tuliyoizoea lazima tuelewane na kwa pamoja tuwe jasiri wa kuepa mitego ya kutugawa.
 
Naomba kuuliza;
mtuhumiwa akiitwa mahakan akagoma mahakama itachukua hatua gani
mtuhumiwa wa kesi ya ndoa au mirath akigundua kua mahakama itaamua kwa kumfaidia mlalamikaji akaamua kuikana dini kabla kesi haijaisha mahakama itakua na haki ya kumhukumu japo si muumin wa hiyo dini? Ikiwa mahakam itaamuru mtuhumiwa wa uzinzi apigwe kwa mawe hadi afe je hukumu hiyo itatekelezwa na nani na je haitakinzana na haki ya kuishi? Na endapo mahakama itatoa adhabu ya kifungo cha jela(kama ipo) nani atasimamia utekelezaji wa hukumu hiyo?
 
tkiwambia mwende shule mnakasirika, Civil cases hazna mtuhumiwa, ukiitwa mahakamani ukakataa km wewe ni upande wa kesi,kesi inaskilzwa na ktolewa maamuz upande mmoja,pia hakna adhab km hzo kwa uzinz,adhab yake ni fain tu! Hatuwez kuweka kadhcourt coz ktakuwa na mgongano mkubwa,tz c dola ya kiislam!
 
kwa nini waislamu wasiruhusiwe kuanzisha mahakama yao bila kuingiliwa na serikali?
 
Ndugu zangu watz hebu tusikubali dini zitugawanye kila dini au taasis ikidai mahakama yake tunategemea nini?
 
Back
Top Bottom