- Thread starter
- #101
Wewe unayemtetea uwezo wako ni kama wake wa kuhongwa hela kubadili ripoti. Of course hata ningekuwa mimi ndiyo professor ningechukua hela ili kulinda uhai wangu. Kipindi hiki serikali inalinda wawekezaji kuliko uhai wa watanzania. Prof angeshupaza shingo wangemuua. Hivyo tumuelewe hiki ndicho kipindi cha hivyo. Hata akina Prof Kabudi au Prof Luoga asingekuwa Dkt Magufuli wangeuawa na ripoti zao za madini na makinikia etc. Kwa ufupi Prof tusimlaumu ila tuwalaumu kundi la mafisadi lililokumbatiwa na serikali. Prof kafanya hivyo kutetea uhai wake.
Unasoma wapi kuwa ninamtetea huyo profesa kiasi cha wewe hata kuujua uwezo wangu wa kuhongwa?
Kuutambua uwezo wake ili kuweza kupambana na ukakasi wa ripoti yake (head on) wewe inakupa taabu mno?
Kwamba hatimaye tukajua Professor Manyele ni nguli kwenye eneo lake la utaalamu.
Kwamba hakukosa wasaidizi wowote ambao angewahitaji. Kwamba alikuwa na access zote katika maabara zozote nchini hadi nje ya nchi, nk nk.
Wewe bado huoni kuwa tuna tatizo kubwa zaidi linalohitaji kujizatiti kweli kweli kukabiliana nalo na kuwa na facts za kutosha ni jambo la muhimu mno?
Ripoti ya Vinyesi vya Ng'ombe mto Mara haishawishi
Nina taabu na ripoti hii labda kuliko hata wewe mjomba.
Habari ndiyo hiyo.