Prof Shivji: Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania

Prof Shivji: Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania

Tume huru ni nini na inatatuaje matatizo ya watanzania?

Muhimu watawala waheshimu matakwa ya watu.
Itatuletea Viongozi waadilifu waliochaguliwa kihalali na Wananchi
 
Sasa mbona hatuambii tiba ya matatizo yetu ni ipi?Kama katiba siyo.
Prof,hawezi kuongea kitu bila kuweka SULUHU!!!lazma atakuwa alijilevya au mtoa mada Umejilevya kwa mvinyo wa Magogoni/chamwino
 
Matakwa ya watu yanawezaje kuheshimiwa ikiwa takwa la katiba mpya hamliheshimu? Hivi nyinyi mataga mbona huwa akili zenu mnapenda kushikiwa?
nyie ni mbuzi tu nani kawaambia kila mtu anataka hiyo mikalatasi ya katiba ? usitusemee wote kila mtu anamaoni yake sema wewe pekeyako unataka siyo kila mtu umsemee punda wewe
 
Natamani CDM waelewe hili. Tatizo hawatoelewa kwa sababu wana sababu zao mbali za kukomalia hoja hii
 
Wewe machaga, matakwa ya watu huwa yanaheshimiwa kwa shinikizo la watu kwa umoja wao.

Marekani wana katiba bora sana, mbona kuna mambo kufanyika mpaka waandamane. South Afruca ni vile vile na Kenya.

Hivi mnafikiri katiba inashika bunduki na kutishia watu wafuate matakwa ya watu?

Haya COVID-19 wako bungeni kinyume na katiba hii hii mbovu, mmefanya nini ?

Kila mtu anataka vitu vizuri akiwa amekaa amekunja nne, anakunywa wine.

Hata hiyo katiba ikiwa unavyotaka, ikivunjwa makusudi mtafanyaje ?

Mkuu tunataka hiyo katiba mpya ili ivunjwe. Lengo letu ni katiba nzuri ili ivunjwe makusudi.
 
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania kwa sasa.
Prof Shivji amesema wanasiasa wanapenda madaraka na siyo siasa safi na kuwatumikia wananchi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690
Huyu niliwahi pendekeza anyang'anywe PhD na afutwe uprofesa baada ya kuyakana maandiko, machapisho na mafundisho yake ya muundo sahihi wa muungano wa serekali tatu.

Hata hivyo huyu ni kibaraka wa watawala kama kabudi
Mbona wakati ule alimsifu JK kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya
 
Kama haujawahi kusoma hata kitabu kimoja cha Shivji ujitathmini upya. Haswa kama unapenda kuitazama Tz na viongozi wake.
 
Katiba siyo lazima iwe mwarobaini ambao inasemekana unatibu magonjwa arobaini.

Katiba hata ikiwa panadol inatosha kabisa kutuondolea headache!

Professa amechemsha. Wasomi wetu hovyo sana. Wao ndiyo chanzo cha matatizo tuliyonayo kama Taifa. Hawana msaada zaidi ya maji gambo na Matumbo yao tuu.
 
Prof Yuko sahihi katiba haiwezi kumaliza umaskini simply kwa kuwa tu na katiba, wanasiasa wanaililia kisa madaraka Yao.
Hawa Chadema agenda yao imegundulika.

Mama anahangaika na namna ya kuwaletea Watanzania maendeleo sio huu upuuzi.
 
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania.
Prof Shivji amesema wanapenda madaraka na siyo siasa safi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690
1. Kwa upande wangu, Katiba Mpya (hasa ile iliyopendekezwa na tume ya Warioba) ni msingi wa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya Watanzania kwa sababu imeweka misingi mizuri na thabiti ya uongozi wa nchi na uwajibikaji wa viongozi wengine wa umma kwa wananchi. mfano, mbunge asipoweza ku'perform' wananchi wana haki na nguvu ya kumwondoa na kumchagua mwingine anaye'perform'.

2. Kama Katiba Mpya ni nzuri, hata sera, sheria na kanuni zitakazotungwa zitakuwa nzuri pia.

3. Ukisema Katiba Mpya siyo mwarobaini wa matatizo yetu, ina maana hata hayo mambo mengine ambayo Prof Shivji anadhani ndiyo mwarobaini nayo hayatakuwa mwarobaini.

4. Hii ina maana kwamba Katiba Mpya nzuri inaweka utaratibu mzuri au ni mahali pazuri pa kuanzia na haina maana kwamba tukishakuwa na hiyo Katiba Mpya basi mambo mengine yasifanyike.

5. Nilimsikia akitolea mfano nchi kama Afrika Kusini na Kenya (na pia Uganda) kwamba ndizo zenye Katiba nzuri sana Afrika, lakini mbona zina matatizo as if hakuna nchi duniani zenye Katiba nzuri ambazo mambo yao yanaenda vizuri. Ni kama kusema kwa vile mama akijifungua anapata maumivu, basi kujifungua siyo kuzuri. Au kwa vile ndege huwa zinapata ajali, basi usafiri wa ndege siyo salama au kwa vilevile kuna wanandoa wanaoachana basi kuoa siyo kuzuri au hakufai. Kwa nini Prof hakutolea mfano nchi zenye Katiba nzuri na zinafanya vizuri? Ni kama Katiba Mpya (yaani tukiwa na Katiba nzuri bora kuliko tuliyonayo) mambo yatazorota zaidi kuliko ilivyo sasa.

Mimi naona kama ni starting point inayotupa direction ya kuboresha pia maeneo mengine kwa sababu tayari tunakuwa na msingi mzuri wa kuanzia ujenzi wa taifa letu.
 
Katiba siyo lazima iwe mwarobaini ambao inasemekana unatibu magonjwa arobaini.

Katiba hata ikiwa panadol inatosha kabisa kutuondolea headache!

Professa amechemsha. Wasomi wetu hovyo sana. Wao ndiyo chanzo cha matatizo tuliyonayo kama Taifa. Hawana msaada zaidi ya maji gambol na Matumbo yao tuu.
Sasa mbona Musukuma pia mnamtukana??? Nyinyi ni kutukana tu kama wehu vile
 
Prof Yuko sahihi katiba haiwezi kumaliza umaskini simply kwa kuwa tu na katiba, wanasiasa wanaililia kisa madaraka Yao.
Huo ndio ukweli ambao wapuuzi wamebishana sana juzi kati! Ishu ni kwamba jamaa wanataka uchochoro wa kuingilia ikulu ila wakipata hio chance mna uhakika gani hawatabadili katiba na kujiwekea vifungu vya upendeleo ili wabaki kuchuma mali kupitia madaraka!
 
Back
Top Bottom