Finally, someone has spoken the reality.
Ni kweli kuwa na katiba bora ni jambo la muhimu lakini maendeleo na mabadiliko ya kweli yanahitaji zaidi ya katiba.
Kama wanasiasa wataacha unafiki na kuamua kulitumikia taifa na si matumbo yao, kuwatumikia wananchi na si maslahi ya familia zao, marafiki zao na washirika wao basi hatutaona uroho na ulafi wa madaraka, hatutaona sheria za ajabu ajabu zikitungwa, hatutaona watu wakiwa busy kutafuta loop holes ili kupiga dili. Maana kama mtu anaweza kushawishi watu wakabadili katiba ya chama ili iendane na matakwa yake au malengo yake ni kujidanganya kudhani mtu huyo huyo akipewa dhamana ya kuongoza Taifa hata kama kuna katiba nzuri vipi hatajaribu kubadilisha baadha ya maeneo ili kuhakikisha maslahi yao yanalindwa hili tunalishuhudia kenya sasa.