1. Kwa upande wangu, Katiba Mpya (hasa ile iliyopendekezwa na tume ya Warioba) ni msingi wa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya Watanzania kwa sababu imeweka misingi mizuri na thabiti ya uongozi wa nchi na uwajibikaji wa viongozi wengine wa umma kwa wananchi. mfano, mbunge asipoweza ku'perform' wananchi wana haki na nguvu ya kumwondoa na kumchagua mwingine anaye'perform'.
2. Kama Katiba Mpya ni nzuri, hata sera, sheria na kanuni zitakazotungwa zitakuwa nzuri pia.
3. Ukisema Katiba Mpya siyo mwarobaini wa matatizo yetu, ina maana hata hayo mambo mengine ambayo Prof Shivji anadhani ndiyo mwarobaini nayo hayatakuwa mwarobaini.
4. Hii ina maana kwamba Katiba Mpya nzuri inaweka utaratibu mzuri au ni mahali pazuri pa kuanzia na haina maana kwamba tukishakuwa na hiyo Katiba Mpya basi mambo mengine yasifanyike.
5. Nilimsikia akitolea mfano nchi kama Afrika Kusini na Kenya (na pia Uganda) kwamba ndizo zenye Katiba nzuri sana Afrika, lakini mbona zina matatizo as if hakuna nchi duniani zenye Katiba nzuri ambazo mambo yao yanaenda vizuri. Ni kama kusema kwa vile mama akijifungua anapata maumivu, basi kujifungua siyo kuzuri. Au kwa vile ndege huwa zinapata ajali, basi usafiri wa ndege siyo salama au kwa vilevile kuna wanandoa wanaoachana basi kuoa siyo kuzuri au hakufai. Kwa nini Prof hakutolea mfano nchi zenye Katiba nzuri na zinafanya vizuri? Ni kama Katiba Mpya (yaani tukiwa na Katiba nzuri bora kuliko tuliyonayo) mambo yatazorota zaidi kuliko ilivyo sasa. Mimi naona kama ni starting point inayotupa direction ya kuboresha pia maeneo mengine kwa sababu tayari tunakuwa na msingi mzuri wa kuanzia ujenzi wa taifa letu.