Prof Shivji: Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania

Prof Shivji: Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania

Huyo professor shivji Alisha poteza credibility yake toka kipindi cha Kila cha Katiba hana jipya asubiri afe akazikwe.
 
KILA KITAFUTWACHO KINA FAIDA. ANAYEKIPATA AWE NA SIFA NA IWE NI HALALI NA HAKI. KILA CHAMA CHA SIASA LENGO NI MADARAKA HATA CCM. SASA KWA KUWA WOTE HUTAKA NA WANAHAKI SAWA. APATAYE KWA KUWASHINDA WENGINE IWE NI KWA UHALALI NA HAKI INAYOONEKANA. WASHINDWAWO WAMSHIKE MKONO NA KUMPONGEZA ALIYESHINDA. HAPO NDIPO TUNAPOTAKA WOTE. NA NJIA NI KUPATA KATIBA MPYA AU KUREKEBISHA KATIBA ILIYOPO
“HAPO NDIPO TUNAPOTAKA WOTE...” wote na nani?

Mie sihitaji hilo nachotaka ni pesa tu kama katiba mpya itakuja na kifungu cha kugawa hela za kujiendeleza kimaisha kwa wananchi kama ilivyokuwa LIBYA basi count me in.
 
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania kwa sasa.
Prof Shivji amesema wanasiasa wanapenda madaraka na siyo siasa safi na kuwatumikia wananchi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690
Katiba na uwoga wapi na wapi

Katiba inahitaji watu majasiri wa kuisimamia na inahitaji watu majasiri wa kudai haki pindi inapovunjwa?

Watu wenyewe ndo hao wakulialia tu, Haitatusaidia chochote hiyo katiba
 
..yeye Prof anaujua muarubaini wa matatizo ya Watz?

..na wapi amesikia kuna mtu anadai kuwa katiba ni muarubaini wa matatizo yooote ya Watz?
 
Kaongea mtaalamu nilikuwa nashinnda library kusoma kitabu chake kinaitwa Constitutional and legal system of Tanzania,respect kwa Prof. Shivj. Pia hiyo Saccos ikumbuke uhuru wa kutoa maoni una mipaka yake kupitia kipengele namba 30 cha katiba yetu tunawaangalia tu wanavyowachokoza wahusika.
 
Katiba Mpya itatupa Tume HURU ya Uchaguzi japokuwa sio Mwarobaini wa matatizo yetu ila itayapunguza kwa kiasi kikibwa.
Ni mwarobaini usiwasikilize Lumumba buku saba wanapotosha wajinga South au Kenye tunaweza kufafikia kwa lolote
 
Nani kasema katiba mpya ni mwarobaini wa matatizo yote? Katiba mpya haitaleta ajira, haitaweka pesa mfukoni, haitarekebisha mausiano ktk ndoa km ni mabaya... Katiba mpya italeta haki na kuimarisha taasisi zetu na kutoa kutegemea mapenzi ya mtu mmoja. Kwa hiyo katiba mpya Watanzania tunaihitaji.
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania kwa sasa.
Prof Shivji amesema wanasiasa wanapenda madaraka na siyo siasa safi na kuwatumikia wananchi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690
 
Mna akili mbovu sana Mataga. Yaani alichokiandika Musiba kawaamulia Watanzania milioni 60?
Kaongea mtaalamu nilikuwa nashinnda library kusoma kitabu chake kinaitwa Constitutional and legal system of Tanzania,respect kwa Prof. Shivj. Pia hiyo Saccos ikumbuke uhuru wa kutoa maoni una mipaka yake kupitia kipengele namba 30 cha katiba yetu tunawaangalia tu wanavyowachokoza wahusika.
 
Kwanza tuwe nayo, ndio uulize haya maswali.
Wewe machaga, matakwa ya watu huwa yanaheshimiwa kwa shinikizo la watu kwa umoja wao.

Marekani wana katiba bora sana, mbona kuna mambo kufanyika mpaka waandamane. South Afruca ni vile vile na Kenya.

Hivi mnafikiri katiba inashika bunduki na kutishia watu wafuate matakwa ya watu?

Haya COVID-19 wako bungeni kinyume na katiba hii hii mbovu, mmefanya nini ?

Kila mtu anataka vitu vizuri akiwa amekaa amekunja nne, anakunywa wine.

Haya, Hata hiyo katiba mpya ikiwa unavyotaka, ikivunjwa makusudi mtafanyaje ?
 
Shivji ni 1/60,000,000. Akili yako ina macho kweli? Kwamba alichoandika Musiba kamwandikia Shivji na Watanzania mil 60? Tingisha kichwa chako ufikiri tena. Hata kama kuna matatizo Kenya na Afrika ya Kusini - hiyo ni sababu kwa Tanzania kutokuwa na katiba nzuri? Una akili wewe kweli?
Machadema yataanza kumchukia Shivji ingawa yalikuwa yanamsifia kabla, ha ha ha. Haya majitu hayajielewi.
 
Kwanza siyo maoni ya Shivji. Ni maoni ya akina Musiba na vijamvi vyao... Arguments za kijinga kabisa. Eti kwa sababu vile Kenya kuna matatizo kwa hiyo Tanzania hahitaji katiba mpya. Lo, what a stupid argument! Kwamba sitaki kuoa kwa vile ndoa ya jirani ina matatizo!!
Na hayo hapo ni maoni yako na mtazamo wako binafsi pia...... kama ilivyo kwa Shivji na wengine
 
Na wale wanaoikataa, wanaikataa kwa nini? Mimi naitaka ili wananchi ndio tutoe na kunyima madaraka. Siyo akina Mahera na Jamana Printers...
Prof Yuko sahihi katiba haiwezi kumaliza umaskini simply kwa kuwa tu na katiba, wanasiasa wanaililia kisa madaraka Yao.
 
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania kwa sasa.
Prof Shivji amesema wanasiasa wanapenda madaraka na siyo siasa safi na kuwatumikia wananchi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690
Hakuna katiba ya nchi yoyote duniani ambayo ni mwarobaini wa matatizo yote katika nchi. Yaani katiba iwe mwarobaini wa matatizo ya ndoa, ulevi, wanaume kulala nje ya ndoa, ukabaji, ajali za barabarani na majini nk. Tunataka katiba ambayo itaweka misingi ya kutatua matatizo makubwa, kuwajibisha wanaokiuka wajibu wao nk.
 
Ni kipimo gani kitakachotumika kujua kama mbunge ana-perform au laa?? Ni nani atakuwa mpimaji wa hiyo performance?

Hebu taja wewe nchi hizo zenye katiba nzuri na zinafanya vizuri tuzione
Kwa hiyo, unataka kusema nchi ikiwa na katiba mbaya ndiyo inayofanya vizuri? Soma Katiba Inayopendekezwa (na Tume ya Warioba) utaona imetoa mwongozo gani kwa wabunge wasio 'perform'.
 
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania kwa sasa.
Prof Shivji amesema wanasiasa wanapenda madaraka na siyo siasa safi na kuwatumikia wananchi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690
Uchawa
 
Hivi hiki kigazeti cha kishoga bado kipo? Bila ruzuku kingejifia maana hakuna mwenye akili timamu anaweza kununua huo ushuzi. Kodi zetu zinatumika kiboya sana
 
Source ya habari ni jamvi la habari!
Halafu haya ni maelezo ya mleta thread. Nina uhakika profesa alizungumzia hili jambo kwa muktadha mwingine lakini hawa wakageuza. Hawa wengi wao ni wachumia tumbo wanaonufaika na mfumo huu wa kubebana na wanajua mambo yakibadilika hawawezi kupata tena vya bure.
 
Back
Top Bottom