Prof Shivji: Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania

Prof Shivji: Katiba mpya siyo mwarobaini wa matatizo ya watanzania

Huyu niliwaji pendekeza anyang'anywe PhD na afutwe uprofesa baada ya kuyakana maandiko, machapisho na mafundisho yake ya muundo sahihi wa muungano wa serekali tatu.

Hata hivyo huyu ni kibaraka wa watawala kama kabudi
Mbona wakati ule alimsifu JK kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya
Kama wewe ulivyo kibaraka wa tutashitakiwa MIGA
 
Matakwa ya watu yanawezaje kuheshimiwa ikiwa takwa la katiba mpya hamliheshimu? Hivi nyinyi mataga mbona huwa akili zenu mnapenda kushikiwa?
Takwa la katiba mpya ni takwa la wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka. Sio takwa la wananchi
 
Kwa mfano Mdude anapewa Katiba mpya. Atasaidia nini maana kiakili kweli anahitaji msaada. Katiba mpya inatutaka tubadilike hata sisi tunaoidai katiba hiyo
 
Tume huru itatuletea watawala wapya......
Watawala ni wale wale tu.

Lowassa wa CCM ni yule yule Lowasaa wa Chadema.

Usijitengenezee matamanio yasiokuwepo.

Hata leo CHAUMA wakishika Dola, watu kutoka CCM wale unaowaona hawafai watahamia huko huko Chauma kusaka fursa.
 
Shida hapo utakuta wamechukua sentensi iyo tu waandishi wakaitumia kuandika habari,tujiulize je profesa aliongea ivo akiwa wapi kwa mukutadha upi na je msingi wa iyo sentensi ni kukubali kuwa katiba ya sasa iko sawa?

Mi naona hapo kwenye Hilo gazeti kuna chembechembe za upotoshaji maana katiba ya sasa(1977) ina mapungufu kuanzia mfumo wa muungano, mamlaka ya raisi, uhuru wa mahakama, mamlaka ya bunge, haki za binadabu, maadili ya viongozi n.k.

Na pia ukizingatia nyakati zimebasilika sana kwaiyo na changamoto zimebasilika sana hivyo tunahitaji kujitazama kwa kutengeneza katiba mpya itakayokua shirikish sio iyo iliyotungwa wakati nchi ikiwa changa chini ya mfumo wa chama kimoja na mfumo wa uchumi wa kijamaa
 
Huo ndio ukweli ambao wapuuzi wamebishana sana juzi kati! Ishu ni kwamba jamaa wanataka uchochoro wa kuingilia ikulu ila wakipata hio chance mna uhakika gani hawatabadili katiba na kujiwekea vifungu vya upendeleo ili wabaki kuchuma mali kupitia madaraka!
Hata sasa hivi ikitokea tu wameshika madaraka kwa katiba hii hii, usitegemee wataleta katiba mpya.

Tena wanaweza hata kuondoa kipengele cha term limits maana ni wazoefu wa hiyo kazi.
 
Prof Yuko sahihi katiba haiwezi kumaliza umaskini simply kwa kuwa tu na katiba, wanasiasa wanaililia kisa madaraka Yao.
Everything has a backbone. Unaweza ukaona katiba haiwezi kumaliza umaskini simply kwakuwa huna uwezo wa ku link katiba ya nchi na ukuwaji wa uchumi wa nchi.

Watu wengi mnadhani kuwa katiba ina impact politically tu lakini hamjui kuwa politics (policies, regulations, checks and balancies n.k) ndio zinazo impact uchumi directly.

Katiba ndio msingi mama wa kila kitu katika nchi anzia kwenye ngazi ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na nyanja nyingize zote. So maendeleo bila checks and balances (kitu ambacho ni kama hakipo kwa sasa) ni ndoto.
 
Source ya habari ni jamvi la habari!
Source ya habari ni jamvi la habari!
Ni kweli alisema hivyo Alhamisi pale UDSM wakati wa kongamano la Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere. Kauli yake hiyo ilinishangaza maana ina'imply' kwamba kumbe tukiwa na Katiba mbaya ndiyo mwarobaini wa matatizo yetu. Labda angetoa hoja kwamba pamoja na kuwa na Katiba Mpya tunahitaji pia kuboresha maeneno kadha wa kadha.

Hapo ningemwelewa. Lakini kusema hivyo tu na kutolea mfano hizo nchi tatu Kenya, Afrika Kusini na Uganda ni kama kusema hakuna nchi zenye Katiba Bora ambazo zinafanya vizuri. Labda tu alitaka ku'dodge' swali aliloulizwa na mshiriki wa kongamano.
 
Msomi nguli wa Tanzania Prof Issa Shivji amelichambua dai la katiba mpya na kusema halina tija wala si mwarobaini wa matatizo yanayowakumba watanzania kwa sasa.
Prof Shivji amesema wanasiasa wanapenda madaraka na siyo siasa safi na kuwatumikia wananchi, ametolea mfano kwa vita ya madaraka inayoendelea nchini Kenya na Afrika Kusini licha ya kubadili katiba mara kwa mara.View attachment 1838690

Hivi Kinuju hii katiba mpya Ina nini nawe?
 
Wewe machaga, matakwa ya watu huwa yanaheshimiwa kwa shinikizo la watu kwa umoja wao.

Marekani wana katiba bora sana, mbona kuna mambo kufanyika mpaka waandamane. South Afruca ni vile vile na Kenya.

Hivi mnafikiri katiba inashika bunduki na kutishia watu wafuate matakwa ya watu?

Haya COVID-19 wako bungeni kinyume na katiba hii hii mbovu, mmefanya nini ?

Kila mtu anataka vitu vizuri akiwa amekaa amekunja nne, anakunywa wine.

Hata hiyo katiba ikiwa unavyotaka, ikivunjwa makusudi mtafanyaje ?
Kuhusu suala la covid 19 je chama hakikumtaka spika kutengue uwepo wa hao watu bungeni? Ina maana mnajisahaulisha au mnajitoa ufahamu? Huwa mnatumia makalio kufikiri au mna vichwa kama binadamu wengine.

Mbona masuala yaliyoko uchi nyie inakuwa ngumu sana ku grasp concept zake?
 
nyie ni mbuzi tu nani kawaambia kila mtu anataka hiyo mikalatasi ya katiba ? usitusemee wote kila mtu anamaoni yake sema wewe pekeyako unataka siyo kila mtu umsemee punda wewe
Wewe usie na akili huna madhara kwetu. Wewe ni msukule mmoja ambae umeshikiwa akili na kamwe huwezi ku prevail mbele ya watu wanaojielewa.
 
Takwa la katiba mpya ni takwa la wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka. Sio takwa la wananchi
Kama kwa akili yako hiyo ndio unawaza hivyo basi bora ufe tu. Hujui hata kuwa hata rasimu ya Warioba ilihusisha kukusanya maoni mitaani wa raia walala hoi.

Mimi naweza kukuambia kuwa mnaong'ang'ania katiba ya sasa yenye uozo mwingi ndio hamna akili mnahitaji kupimwa mkojo. Nyinyi wenye uchu wa madaraka mnaojimilikisha nchi na rasilimali zake ndio mnaogopa katiba mpya kwakuwa itawafanya vibaya.

Tumia ubongo wako ukitaka ku argue na mimi, usiropoke tu.
 
Kwa lugha nyepesi ambayo ni ngumu kueleweka Profesa Shivji anatueleza kwa utawala wa Chama cha mataga hata tukibadilisha katiba ni kazi bure .Dawa ni kuwafutulia mbali
 
Katiba siyo lazima iwe mwarobaini ambao inasemekana unatibu magonjwa arobaini.

Katiba hata ikiwa panadol inatosha kabisa kutuondolea headache!

Professa amechemsha. Wasomi wetu hovyo sana. Wao ndiyo chanzo cha matatizo tuliyonayo kama Taifa. Hawana msaada zaidi ya maji gambol na Matumbo yao tuu.
Kuna nchi hata hiyo katiba hawana
 
Huo ndio ukweli ambao wapuuzi wamebishana sana juzi kati! Ishu ni kwamba jamaa wanataka uchochoro wa kuingilia ikulu ila wakipata hio chance mna uhakika gani hawatabadili katiba na kujiwekea vifungu vya upendeleo ili wabaki kuchuma mali kupitia madaraka!
Uko sahihi hyo katiba ni nani anaitaka kabla umaskini haujaondolewa wanasiasa wanakuja na agenda zisizogusa Raia Moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom