Prof. Shivji: Mikataba ya Bandari na Dubai inayokuja itakuwa Siri na haitapelekwa Bungeni

Prof. Shivji: Mikataba ya Bandari na Dubai inayokuja itakuwa Siri na haitapelekwa Bungeni

"DP WORLD wakipata faida huwezi kuwatoza kodi lakini pia hakuna kifungu chochote (katika mkataba wa bandari) kinachozungumzia revenue sharing (mgawanyo wa mapato), kama nchi itafaidika vipi?" Prof. Shivji

"Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD" Profesa Issa Shivji

"Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji" Prof. IssaShivji

"Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika" Prof. Issa Shivji

"Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa" Prof. Issa Shivji

"Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)" Prof. Issa Shivji

"Imezungumzwa sana kwamba watu wetu wataendelea na ajira zao, wafanyakazi Watanzania watashiriki vipi katika management (usimamizi)?, wafanyakazi wa kawaida (makuli) na HR (Afisa Rasilimali Watu) hawa watakuwa Watanzania lakini wengine wote katika management watatoka Dubai (DP World)" Prof. Issa Shivji

"Mikataba ya miradi (project agreement) na nchi mwenyeji (host government) mikataba hii haitapelekwa bungeni wala haitawekwa hadharani kwa sababu ni siri. Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari ) ulipelekwa bungeni kwasababu ni mkataba wa kimataifa lakini project agreement ni ya kibiashara hivyo ni confidential (siri). Watanzania hawatajua wameingia katika mkataba gani na kuna nini ndani ya mkataba na mkataba umesema nini" Prof. Issa Shivji

"Shughuli zilizotajwa katika awamu ya kwanza (ya mkataba wa bandari) sio za bandari pekee, kuna Special Economic Zone (maeneo mahususi ya kiuchumi), trade corridor, free zone" Prof. Issa Shivji

"Eneo ambalo sio la DP WORLD lakini ni karibu na eneo la DP WORLD, mtu akitaka kujenga barabara au flyover ambayo interfere (itaingilia) shughuli za DP WORLD hairuhusiwi kwa mujibu wa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari). Serikali itahakikisha kwamba shughuli hizo hazitokuwepo kando kando na eneo la DP WORLD" Prof. Issa Shivji

"Kwa mfano serikali ina dhamira au haina dhamira ya kudevelop (kuendeleza) bandari ya Tanga au Mwanza kwa mujibu wa mkataba , DP WORLD wana haki ya kupewa taarifa hizo kabla ya yote ili wakitaka waweze ku-express interest (kuonesha nia)" Prof. Issa Shivji

"Kuna sekta nyeti katika uchumi na huwezi kuweka katika makampuni ya watu binafsi na bandari ni sekta nyeti mojawapo, ni roho na mishipa ya uchumi hivyo huwezi kuweka katika mikono ya watu binafsi kwa sababu mbalimbali" Prof. Issa Shivji

"Mali zetu ikiwemo madini tunazo-export (tunazozisafirisha nje) ma mali tunazozileta zinapitia bandari na mali nyingine ni very sensitive (nyeti sana), huwezi kuweka hiyo mikono mwa kampuni mbinafsi bila wewe kuwa na mamlaka" Prof. Issa Shivji
 
Screenshot_20230626-100759_(1).png
 
Yani huyu mzee inaonekana katulia kasoma mkataba alafu kaja kutoa nondo..ila tatizo lake tu ni "mjamaa" hapo ndio alipofeli
Kuna ubaya gani kuwa "mjamaa"?

Unapokaririshwa jitahidi sana utumie akili uliyojaliwa na Muumba wako kuitumia na kuona ukweli wa jambo ulilokariri.

Ni wapi duniani pasipokuwepo na ujamaa?
 
Hilo la mikataba ya biashara kuwa siri ni ukweli kabisa, hakuna ataekubali mkataba wake wa kibiashara uanikwe, si Tanzania si Dubai.

Na nani atakaetaka mikataba ya biashara ianikwe wazi? Huyo atakuwa ni ni muhujumu uchumi na msaliti wa kijinga, auliwe tu.

Biashara ni vita kubwa sana kuliko vita ya risasi dunia ya leo.
 
Ule wa Gesi; hata sina hamu kabisa ya kusikia yaliyomo humo ndani; kama mwendo wenyewe ndio huu!

Kwa kuanzia tu, gharama za mwanzo bilioni $30, zikawa zimepaa hadi kufikia bilioni zaidi ya $40zinazoelezwa sasa!
Kijana huelewi kabisa kuhusu biashara za mafuta na gesi/

Huo wa gesi unaousema wewe ni wa kutafuta (exploration) gesi? au wa kuchimba gesi? au wa kuuza gesi?

Hapo sasa.
 
Hilo la mikataba ya biashara kuwa siri ni ukweli kabisa, hakuna ataekubali mkataba wake wa kibiashara uanikwe, si Tanzania si Dubai.

Na nani atakaetaka mikataba ya biashara ianikwe wazi? Huyo atakuwa ni ni muhujumu uchumi na msaliti wa kijinga, auliwe tu.

Biashara ni vita kubwa sana kuliko vita ya risasi dunia ya leo.
elewa context, usiri wa mikataba ya utekelezaji ndio unasukuma watu kuona kuwa mkataba mama unakuwa mzuri na wenye maslai kwa taifa, mkataba mzani umeinamia tz kwa maslai ya mwarabu ndio shida kwetu
 
Mkataba wa kinyonyaji kati ya Chifu Hangaya na Emirate ya Dubai

Mimi Chifu Hangaya nikiwa na akili timamu na nikishinikizwa na kiasi cha fedha nilichopokea kutoka kwa wajomba zangu nakubali kuwapa bure rasilimali za bahari na maziwa yote ya nchi ya Wadanganyika kampuni ya Double Penetration World
 
elewa context, usiri wa mikataba ya utekelezaji ndio unasukuma watu kuona kuwa mkataba mama unakuwa mzuri na wenye maslai kwa taifa, mkataba mzani umeinamia tz kwa maslai ya mwarabu ndio shida kwetu
Huwezi kuwa qanasheria na wataalaam washeria waliobobea halafu ukamsukumia mama mambo ya mikataba. Kwani wanasheria serikalini wanaajiriwa kwa sababu gani?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinhga?

Pia mwiko kabisa kuanika mikataba ya kibiashara. Wewe utsons mapato yako kils mwezi, nenda wizara ya fedha na TRA. Huwezi kuoneshwa mkataba.

Kumbuka, mkataba wowote siyo mapato. Mapato yote yawayo ni makadirio tu. Tena uking'ang'ania sana mapato inaweza kula kwako vibaya sana.

Watanzania wacheni ujinga, someni.
 
Mkataba wa kinyonyaji kati ya Chifu Hangaya na Emirate ya Dubai

Mimi Chifu Hangaya nikiwa na akili timamu na nikishinikizwa na kiasi cha fedha nilichopokea kutoka kwa wajomba zangu nakubali kuwapa bure rasilimali za bahari na maziwa yote ya nchi ya Wadanganyika kampuni ya Double Penetration World
Wewe umenyonywa nini? Kakunyonya TICTS miaka 22 hta hujuwi mkataba wao upoje.
Attach files

Na huu unaokuja bandarini wa kibiashara huwezi kuoneshwa, unataka uoneshwe nini zaidi wakati vigezo vyote vya mikataba ya bandari vina trange ya rates?
 
Kijana huelewi kabisa kuhusu biashara za mafuta na gesi/

Huo wa gesi unaousema wewe ni wa kutafuta (exploration) gesi? au wa kuchimba gesi? au wa kuuza gesi?

Hapo sasa.
Sasa wewe hapa umeelewa nini?

Kwani hujui tupo kwenye hatua gani hadi sasa?
Kwenye Bandari nako ulianza na maswali ya kipuuzi namna hii, kwa kudharau watu kuwa hata hawajawahi kufika bandarini.
Ni wewe tu unayeyajua mambo haya?
 
Sasa wewe hapa umeelewa nini?

Kwani hujui tupo kwenye hatua gani hadi sasa?
Wewe nimekuuliza huo mkataba wa gesi unaoungolea ni upi katika hiyo?

Tupo hatua gani kwenye lipi?
 
Wewe nimekuuliza huo mkataba wa gesi unaoungolea ni upi katika hiyo?

Tupo hatua gani kwenye lipi?
Wewe ulielewa ninazungumzia mikataba ipi ya gesi inayoshughulikiwa na serikali wakati huu?

Mambo ya gesi ndiyo leo tumeanza kuyashughulikia? Huwezi kutumia akili yako vizuri ikuelekeze kwenye jambo linalozungumziwa?
 
Back
Top Bottom