Prof. Shivji: Mikataba ya Bandari na Dubai inayokuja itakuwa Siri na haitapelekwa Bungeni

Prof. Shivji: Mikataba ya Bandari na Dubai inayokuja itakuwa Siri na haitapelekwa Bungeni

Yani huyu mzee inaonekana katulia kasoma mkataba alafu kaja kutoa nondo..ila tatizo lake tu ni "mjamaa" hapo ndio alipofeli
Huyu mzee hana jipya humo alikochambua kajichanganya mwenyewe mara mkataba wenyewe hatutauona sasa huu mkataba gani anauchambua hapa? Mzee kapitwa na wakati maisha yanaenda speed sana yamemuacha mimi sijaona lolote jipya kaongea ambalo hatulijui. Mkataba wenyewe ndio unakuwa na details za kibiashara na mambo ya returning ya investment haya mengine ya kodi ni juu ya TRA wataendelea kukusanya DP kuongeza ukuwaji wa biashara ma containers. Anaongelea usiri wa tunayo export na ku import hivi anaongelea usiri gani huyu mzee? Kuna siri gani sasa hivi duniani, wanunuzi wako nje tunajuwa nini tunauza, BOT wanatangaza biashara zetu ze export siri gani tena? au tunauza silaha? huyu mzee ni kama ule ujinga wa zamani marufuku kupiga picha hapa eneo hili ni sensitive, watu wana Google wanakuona mpaka chumbani kwako wewe bado unazuia picha. Biashara hakuna usiri tena tunajuwa tunachouza(Export) tunajuwa nini tuna import, apeleke ujamaa wake huko.
 
Abariki kweli, anawaambia ukweli bado hamumuelewi.

Mama anawaletea maendeleo hamna macho wala muono wa kuyaona.

Shivji yupo sahihi kanisa. Hamtoweza kuuona mkataba.

Wewe ukioneshwa mkataba wa biashara za watu utakusaidia nini? Kusoma kwenyewe mkataba hujuwi.
Umechanganyikiwa kabisa Faiza huwezi tena kufikiri kama upo karibu na Maza mwambie alichotufanyia hatujapenda bado ana nafasi ya kurekebisha hajachelewa
 
Hilo la mikataba ya biashara kuwa siri ni ukweli kabisa, hakuna ataekubali mkataba wake wa kibiashara uanikwe, si Tanzania si Dubai.

Na nani atakaetaka mikataba ya biashara ianikwe wazi? Huyo atakuwa ni ni muhujumu uchumi na msaliti wa kijinga, auliwe tu.

Biashara ni vita kubwa sana kuliko vita ya risasi dunia ya leo.
Ndio hapo namshangaa huyu mzee mkataba gani huo anaoujadili wakati huohuo anasema mkataba ni siri na hatutauona, na ni kweli hakuna mkataba wa kibiashara ukaanikwa hadharani inaondoa dhana ya ushindani. Mzee kajichanganya lakini kwa sababu kuna watu ndio wanapenda kusikia haya watapiga na makofi lakini ukweli hakuna lolote jipya katika uchambuzi wake, zaidi naona mzee dunia imemuacha hasa pale anaposema usiri wa export na import, hakuna siri katika hili kila kitu lazima kiwe declared kabla ya kupakiwa. Eti sensitivty...
 
What is needed is impeachment tuuu tuanze upya!!

Makamu wa rais awe in ofisi for 90 days until general election
 
Hao ma professor wenu ni uchwara tu.

Ni sawa na mtu kwenda car dealership kununua gari lenye thamani la $30000 kwa hire purchase.

Hivi unaweza kujua utalipa kiasi gani na kwa miaka mingapi bila ya kukakaa chini na sales man kuamua mambo kadhaa ya payment zako kama annual interest watakayo ku-charge, amount of down payment unayotakiwa kulipa, kupanga kwenye mshahara wako utatoa kiasi gani, fines for missing payment, inflation interest, default risk interest.

Utakuta watu kumi wanaopishana kimapato, stability ya kazi zao, credit score zao; hawana mkataba unaofanana kutokana na kiasi watakachoamua kulipa kwa mwaka, interest watakayo tozwa kwa mwaka zinaweza zisilingane, down payment watakayo lipa; kuna factor kadhaa zitakazo amua ‘consideration’

Sasa we unawezaje kujua muda wa lease contract unapoenda kununua gari la hire purchase bila ya kukaa chini na sales man na kupanga makubaliano ya kulipa na kujua itachukua muda gani.

Halafu mkataba wa kibiashara za kimataifa ni independent ya siasa za nchi, ndio maana watu wakatengeneza ‘stabilisation clauses’ utekelezaji wake ahusiani na siasa ukishakubaliwa na pande mbili, kuuvunja akutotokana na siasa za baadae ata zikiwa adverse. Utavunjwa kwa njia ya dispute resolution tu.

Mpaka sasa hakuna mtu alieni prove wrong, Tanzania hakuna shahada ya business law. Wanafunzi wa sheria awasomi commercial contract law. Wanafunzi wa biashara hawana modules introduction za contract law, tort and business law. Na hii ndio shida, lakini siyo hiyo framework ya IGA ni uelewa mdogo tu wa what is to follow on concession agreement.

Mijitu imekadhana mkataba auna muda, how unaweza panga muda bila ya kukubaliana concession/lease agreement kwanza; ambayo mshaambiwa huko bado.

For gods sake nchi ina zaidi ya miaka 60 ya uhuru, imeshapeleka maelfu ya watu kusoma nje. Iweje leo concepts ambazo wanafunzi wa biashara tu nchi zilizoendelea wawe na abc ya hayo mambo, let alone washeria ndio kabisa depth yao itakuwa kubwa zaidi. Halafu sisi nchini kwetu the so called prominent professor hawana ata abc.

Shame on Tanzania education system.
 
Ndio hapo namshangaa huyu mzee mkataba gani huo anaoujadili wakati huohuo anasema mkataba ni siri na hatutauona, na ni kweli hakuna mkataba wa kibiashara ukaanikwa hadharani inaondoa dhana ya ushindani. Mzee kajichanganya lakini kwa sababu kuna watu ndio wanapenda kusikia haya watapiga na makofi lakini ukweli hakuna lolote jipya katika uchambuzi wake, zaidi naona mzee dunia imemuacha hasa pale anaposema usiri wa export na import, hakuna siri katika hili kila kitu lazima kiwe declared kabla ya kupakiwa. Eti sensitivty...
Hana analolijua na yeye kama Lissu tu kwenye mikataba ya biashara zaidi ya kuropoka tu.

Contract law hapo UDSM ni zero.
 
Hao ma professor wenu ni uchwara tu.

Ni sawa na mtu kwenda car dealership kununua gari lenye thamani la $30000 kwa hire purchase.

Hivi unaweza kujua utalipa kiasi gani na kwa miaka mingapi bila ya kukakaa chini na sales man kuamua mambo kadhaa ya payment zako kama annual interest watakayo ku-charge, amount of down payment unayotakiwa kulipa, kupanga kwenye mshahara wako utatoa kiasi gani, fines for missing payment, inflation interest, default risk interest.

Utakuta watu kumi wanaopishana kimapato, stability ya kazi zao, credit score zao; hawana mkataba unaofanana kutokana na kiasi watakachoamua kulipa kwa mwaka, interest watakayo tozwa kwa mwaka zinaweza zisilingane, down payment watakayo lipa; kuna factor kadhaa zitakazo amua ‘consideration’

Sasa we unawezaje kujua muda wa lease contract unapoenda kununua gari la hire purchase bila ya kukaa chini na sales man na kupanga makubaliano ya kulipa na kujua itachukua muda gani.

Halafu mkataba wa kibiashara za kimataifa ni independent ya siasa za nchi, ndio maana watu wakatengeneza ‘stabilisation clauses’ utekelezaji wake ahusiani na siasa ukishakubaliwa na pande mbili, kuuvunja akutotokana na siasa za baadae ata zikiwa adverse. Utavunjwa kwa njia ya dispute resolution tu.

Mpaka sasa hakuna mtu alieni prove wrong, Tanzania hakuna shahada ya business law. Wanafunzi wa sheria awasomi commercial contract law. Wanafunzi wa biashara hawana modules introduction za contract law, tort and business law. Na hii ndio shida, lakini siyo hiyo framework ya IGA ni uelewa mdogo tu wa what is to follow on concession agreement.

Mijitu imekadhana mkataba auna muda, how unaweza panga muda bila ya kukubaliana concession/lease agreement kwanza; ambayo mshaambiwa huko bado.

For gods sake nchi ina zaidi ya miaka 60 ya uhuru, imeshapeleka maelfu ya watu kusoma nje. Iweje leo concepts ambazo wanafunzi wa biashara tu nchi zilizoendelea wawe na abc ya hayo mambo, let alone washeria ndio kabisa depth yao itakuwa kubwa zaidi. Halafu sisi nchini kwetu the so called prominent professor hawana ata abc.

Shame on Tanzania education system.

Sisi bado tunakimbizana na mwenge utumilike mchana
 
Prof. Shivji yupo sahihi sana kwenye hili, baada ya azimio la bunge kupita.......ishu zote za utekelezaji zitakuwa zinapita chini ya kapeti. Ndo maana kuondokana na huu uuzwaji wa nchi ni kutupilia mbali hicho wanachoita mkataba/makubaliano.​
 
"DP WORLD wakipata faida huwezi kuwatoza kodi lakini pia hakuna kifungu chochote (katika mkataba wa bandari) kinachozungumzia revenue sharing (mgawanyo wa mapato), kama nchi itafaidika vipi?" Prof. Shivji

"Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD" Profesa Issa Shivji

"Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji" Prof. IssaShivji

"Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika" Prof. Issa Shivji

"Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa" Prof. Issa Shivji

"Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)" Prof. Issa Shivji

"Imezungumzwa sana kwamba watu wetu wataendelea na ajira zao, wafanyakazi Watanzania watashiriki vipi katika management (usimamizi)?, wafanyakazi wa kawaida (makuli) na HR (Afisa Rasilimali Watu) hawa watakuwa Watanzania lakini wengine wote katika management watatoka Dubai (DP World)" Prof. Issa Shivji

"Mikataba ya miradi (project agreement) na nchi mwenyeji (host government) mikataba hii haitapelekwa bungeni wala haitawekwa hadharani kwa sababu ni siri. Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari ) ulipelekwa bungeni kwasababu ni mkataba wa kimataifa lakini project agreement ni ya kibiashara hivyo ni confidential (siri). Watanzania hawatajua wameingia katika mkataba gani na kuna nini ndani ya mkataba na mkataba umesema nini" Prof. Issa Shivji

"Shughuli zilizotajwa katika awamu ya kwanza (ya mkataba wa bandari) sio za bandari pekee, kuna Special Economic Zone (maeneo mahususi ya kiuchumi), trade corridor, free zone" Prof. Issa Shivji

"Eneo ambalo sio la DP WORLD lakini ni karibu na eneo la DP WORLD, mtu akitaka kujenga barabara au flyover ambayo interfere (itaingilia) shughuli za DP WORLD hairuhusiwi kwa mujibu wa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari). Serikali itahakikisha kwamba shughuli hizo hazitokuwepo kando kando na eneo la DP WORLD" Prof. Issa Shivji

"Kwa mfano serikali ina dhamira au haina dhamira ya kudevelop (kuendeleza) bandari ya Tanga au Mwanza kwa mujibu wa mkataba , DP WORLD wana haki ya kupewa taarifa hizo kabla ya yote ili wakitaka waweze ku-express interest (kuonesha nia)" Prof. Issa Shivji

"Kuna sekta nyeti katika uchumi na huwezi kuweka katika makampuni ya watu binafsi na bandari ni sekta nyeti mojawapo, ni roho na mishipa ya uchumi hivyo huwezi kuweka katika mikono ya watu binafsi kwa sababu mbalimbali" Prof. Issa Shivji

"Mali zetu ikiwemo madini tunazo-export (tunazozisafirisha nje) ma mali tunazozileta zinapitia bandari na mali nyingine ni very sensitive (nyeti sana), huwezi kuweka hiyo mikono mwa kampuni mbinafsi bila wewe kuwa na mamlaka" Prof. Issa Shivji
Nchi hii imefikia uhayawani huu wa kiwango cha lami kwa sababu ya uzezeta wa CCM. Wakati umefika hawa mandondocha wa CCM watupishe.
 
Yani huyu mzee inaonekana katulia kasoma mkataba alafu kaja kutoa nondo..ila tatizo lake tu ni "mjamaa" hapo ndio alipofeli

Mkuu, kwahiyo 'ujamaa' wake unabatilisha nondo zake?

-Kaveli-
 
Wewe umenyonywa nini? Kakunyonya TICTS miaka 22 hta hujuwi mkataba wao upoje.
Attach files

Na huu unaokuja bandarini wa kibiashara huwezi kuoneshwa, unataka uoneshwe nini zaidi wakati vigezo vyote vya mikataba ya bandari vina trange ya rates?

Faiza, TICTS walikuwa na 'full coverage' kwenye bandari zote za bahari na maziwa?

-Kaveli-
 
Ule wa Gesi; hata sina hamu kabisa ya kusikia yaliyomo humo ndani; kama mwendo wenyewe ndio huu!

Kwa kuanzia tu, gharama za mwanzo bilioni $30, zikawa zimepaa hadi kufikia bilioni zaidi ya $40zinazoelezwa sasa!

Kwanini Taifa limekuwa likiingia mikataba bogus kila mara? Tunakosea wapi? Why hatujifunzi?

-Kaveli-
 
Uchambuzi makini kabisa, huyu hajajurupuka amekaa akasoma neno baada ya neno kisha kutoa maoni yake.

NB, labda hata watu wa serikali hawauelewi mkataba ila wanafata tu mkumbo!!

Wasomi wetu wote wanapaswa kujitokeza hadharani kufafanua utata na upuuzi uliopo ktk Mkataba maana walisomeshwa na nchi.

Je, wasomi wetu wameelimika na kuiva vyema?

Na Je wanaingia mezani pasipo kuwa compromised?

Mkataba wowote wa kibiashara kila party anavutia kwake. Kila party anapaswa kulenga faida. Ukizubaa unapigwa!

Both parties zikiwa makini, ndiyo huzaliwa fair contract with win-win situation.

-Kaveli-
 
Kwanini Taifa limekuwa likiingia mikataba bogus kila mara? Tunakosea wapi? Why hatujifunzi?

-Kaveli-
Viongozi wetu hawana 'commitment' juu ya taifa hili, wataanzia wapi kulinda maslahi juu ya taifa wanaloliongoza?
Tatizo linaanzia hapo.

Wanafanya mambo ya kuigiza na viini mambo huku wakijua kuwa taifa linaangamizwa.
 
Sasa wale wabunge wakiongozwa na spika, ambaye ni mwanasheria nguli (km inavyo daiwa) hawakuona haya mambo? Hadi kupitisha kwa kishindo na harakaa??

Mbona inashangaza mnooo, khaaah
Jpm alishasema unapofika wakati wa kusaini mkataba sheria zote uyeyuka
 
Back
Top Bottom