Prof. Shivji: Mikataba ya Bandari na Dubai inayokuja itakuwa Siri na haitapelekwa Bungeni

Kuna ubaya gani kuwa "mjamaa"?

Unapokaririshwa jitahidi sana utumie akili uliyojaliwa na Muumba wako kuitumia na kuona ukweli wa jambo ulilokariri.

Ni wapi duniani pasipokuwepo na ujamaa?
Ww nikuulize unaujua ujamaa?au na ww umemeza tu? Ni fikra za kwenye makaratasi ambazo hazifai
 
Hilo la mikataba ya biashara kuwa siri ni ukweli kabisa, hakuna ataekubali mkataba wake wa kibiashara uanikwe, si Tanzania si Dubai.

Na nani atakaetaka mikataba ya biashara ianikwe wazi? Huyo atakuwa ni ni muhujumu uchumi na msaliti wa kijinga, auliwe tu.

Biashara ni vita kubwa sana kuliko vita ya risasi dunia ya leo.
Mbona umekwepa hoja hizo hapo juu umeenda upande ambao ni kidogo sana wa kile Shivji kaongelea? Kwa maandiko yako juu ya swala hili toka limeanza ulipaswa uje na hoja na majibu kama alivyoelezea Prof, au nondo nzito?
 
Mpuuzi huyu bibi foxy, kwani yeye samia haoni hizi kelele za watu walioamua kujitokeza kufafanua upuuzi uliopo

kama wanasheria wa nchi walishindwa kumwambia ukweli yeye sa100 kwann asisitishe kutokana na ufafanuzi unaotolewa na watu kama kina shivj? Atalinywa mwenywe wala msitake kusingizia watu wengine
Usikute FaizaFoxy ndio Chifu Hangaya mwenyewe. 🤓
 
Sasa wale wabunge wakiongozwa na spika, ambaye ni mwanasheria nguli (km inavyo daiwa) hawakuona haya mambo? Hadi kupitisha kwa kishindo na harakaa??

Mbona inashangaza mnooo, khaaah
Hajaona kwa kuwa ukijifanya umeona wewe siyo ccm
 
"DP WORLD wakipata faida huwezi kuwatoza kodi lakini pia hakuna kifungu chochote (katika mkataba wa bandari) kinachozungumzia revenue sharing (mgawanyo wa mapato), kama nchi itafaidika vipi?" Prof. Shivji

"Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD" Profesa Issa Shivji

"Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji" Prof. IssaShivji

"Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika" Prof. Issa Shivji

"Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa" Prof. Issa Shivji

"Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)" Prof. Issa Shivji

"Imezungumzwa sana kwamba watu wetu wataendelea na ajira zao, wafanyakazi Watanzania watashiriki vipi katika management (usimamizi)?, wafanyakazi wa kawaida (makuli) na HR (Afisa Rasilimali Watu) hawa watakuwa Watanzania lakini wengine wote katika management watatoka Dubai (DP World)" Prof. Issa Shivji

"Mikataba ya miradi (project agreement) na nchi mwenyeji (host government) mikataba hii haitapelekwa bungeni wala haitawekwa hadharani kwa sababu ni siri. Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari ) ulipelekwa bungeni kwasababu ni mkataba wa kimataifa lakini project agreement ni ya kibiashara hivyo ni confidential (siri). Watanzania hawatajua wameingia katika mkataba gani na kuna nini ndani ya mkataba na mkataba umesema nini" Prof. Issa Shivji

"Shughuli zilizotajwa katika awamu ya kwanza (ya mkataba wa bandari) sio za bandari pekee, kuna Special Economic Zone (maeneo mahususi ya kiuchumi), trade corridor, free zone" Prof. Issa Shivji

"Eneo ambalo sio la DP WORLD lakini ni karibu na eneo la DP WORLD, mtu akitaka kujenga barabara au flyover ambayo interfere (itaingilia) shughuli za DP WORLD hairuhusiwi kwa mujibu wa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari). Serikali itahakikisha kwamba shughuli hizo hazitokuwepo kando kando na eneo la DP WORLD" Prof. Issa Shivji

"Kwa mfano serikali ina dhamira au haina dhamira ya kudevelop (kuendeleza) bandari ya Tanga au Mwanza kwa mujibu wa mkataba , DP WORLD wana haki ya kupewa taarifa hizo kabla ya yote ili wakitaka waweze ku-express interest (kuonesha nia)" Prof. Issa Shivji

"Kuna sekta nyeti katika uchumi na huwezi kuweka katika makampuni ya watu binafsi na bandari ni sekta nyeti mojawapo, ni roho na mishipa ya uchumi hivyo huwezi kuweka katika mikono ya watu binafsi kwa sababu mbalimbali" Prof. Issa Shivji

"Mali zetu ikiwemo madini tunazo-export (tunazozisafirisha nje) ma mali tunazozileta zinapitia bandari na mali nyingine ni very sensitive (nyeti sana), huwezi kuweka hiyo mikono mwa kampuni mbinafsi bila wewe kuwa na mamlaka" Prof. Issa Shivji
Sawa ili wale ambao hawaahirishi akili zao kufikiri wasipige kelele
 
Lusinde kesho ataita press kumshambulia prof shivji , watasaidiana na msukuma, baba levo na mwijaku...hao ndo wamepewa tenda ya kujitoa ufahamu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huu mkataba usitishwe malamaja bungeni,waachane na maboresho bandari zetu zibaki chini ya TPA.
 
Profesa anasema kwa mujibu wa mkataba DP wanaruhusiwa kuanza kufanya shughuli hata kabla ya kutia saini ya mikataba midogo na shughuli ikisha anza inakuwa ni part ya mkataba utakao sainiwa na hakuna wa kuhoji!
 
Prof anasema hakutakuwa na interference from any state authorities (kwa kifupi hakuna cha polisi,TRA au TPA) ambaye atakuwa ana muingilia DP world!

Kwa hiyo ni kweli TPA watafanya kazi za kuvusha watu na mitumbwi😂😂😂😂😂😂
 
Abariki kweli, anawaambia ukweli bado hamumuelewi.

Mama anawaletea maendeleo hamna macho wala muono wa kuyaona.

Shivji yupo sahihi kanisa. Hamtoweza kuuona mkataba.

Wewe ukioneshwa mkataba wa biashara za watu utakusaidia nini? Kusoma kwenyewe mkataba hujuwi.
mkataba ni haki yetu kuujuwa kama wananchi na ni haki yetu kukemea mikataba ovu yakifirauni yani ukomo wake haueleweki alafu bado tujione tupo salama apo.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"DP WORLD wakipata faida huwezi kuwatoza kodi lakini pia hakuna kifungu chochote (katika mkataba wa bandari) kinachozungumzia revenue sharing (mgawanyo wa mapato), kama nchi itafaidika vipi?" Prof. Shivji

"Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD" Profesa Issa Shivji

"Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari) ni mkataba kati ya nchi na nchi kuhusu uwekezaji, na mkataba unasema ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ni aina ya mikataba ya uwekezaji" Prof. IssaShivji

"Katika mkataba huu wa bandari kuna mambo mawili, jambo la kwanza, mkataba unahusu ushirikiano wa kiuchumi lakini sio ushirikiano wa kiujumla bali ni katika eneo la bandari za bahari na bandari za maziwa. Na jambo la pili ni kwamba mwekezaji ameshatambulika" Prof. Issa Shivji

"Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. Na ni kweli ni mkataba wa muda mrefu na utaisha pale ambapo mikataba yote ya miradi saba ya awamu ya kwanza itapokuwa imetekelezwa. Na kama kutakuwa na migongano au mifarakano, hadi itakapokuwa imetatuliwa" Prof. Issa Shivji

"Mkataba huu hauwezi kuvunjwa kwa sababu zozote zile hata kama tumevunja uhusiano wa kidplomasia na U.A.E (Falme za Kiarabu)" Prof. Issa Shivji

"Imezungumzwa sana kwamba watu wetu wataendelea na ajira zao, wafanyakazi Watanzania watashiriki vipi katika management (usimamizi)?, wafanyakazi wa kawaida (makuli) na HR (Afisa Rasilimali Watu) hawa watakuwa Watanzania lakini wengine wote katika management watatoka Dubai (DP World)" Prof. Issa Shivji

"Mikataba ya miradi (project agreement) na nchi mwenyeji (host government) mikataba hii haitapelekwa bungeni wala haitawekwa hadharani kwa sababu ni siri. Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari ) ulipelekwa bungeni kwasababu ni mkataba wa kimataifa lakini project agreement ni ya kibiashara hivyo ni confidential (siri). Watanzania hawatajua wameingia katika mkataba gani na kuna nini ndani ya mkataba na mkataba umesema nini" Prof. Issa Shivji

"Shughuli zilizotajwa katika awamu ya kwanza (ya mkataba wa bandari) sio za bandari pekee, kuna Special Economic Zone (maeneo mahususi ya kiuchumi), trade corridor, free zone" Prof. Issa Shivji

"Eneo ambalo sio la DP WORLD lakini ni karibu na eneo la DP WORLD, mtu akitaka kujenga barabara au flyover ambayo interfere (itaingilia) shughuli za DP WORLD hairuhusiwi kwa mujibu wa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari). Serikali itahakikisha kwamba shughuli hizo hazitokuwepo kando kando na eneo la DP WORLD" Prof. Issa Shivji

"Kwa mfano serikali ina dhamira au haina dhamira ya kudevelop (kuendeleza) bandari ya Tanga au Mwanza kwa mujibu wa mkataba , DP WORLD wana haki ya kupewa taarifa hizo kabla ya yote ili wakitaka waweze ku-express interest (kuonesha nia)" Prof. Issa Shivji

"Kuna sekta nyeti katika uchumi na huwezi kuweka katika makampuni ya watu binafsi na bandari ni sekta nyeti mojawapo, ni roho na mishipa ya uchumi hivyo huwezi kuweka katika mikono ya watu binafsi kwa sababu mbalimbali" Prof. Issa Shivji

"Mali zetu ikiwemo madini tunazo-export (tunazozisafirisha nje) ma mali tunazozileta zinapitia bandari na mali nyingine ni very sensitive (nyeti sana), huwezi kuweka hiyo mikono mwa kampuni mbinafsi bila wewe kuwa na mamlaka" Prof. Issa Shivji

Shivji aanze na serikali yenyewe tokea Magufuli na uchaguzi alivyouendesha na hata kupatikana Samia mbona hatujamsikia au kwa sababu aliyefanya haya ni CCM mwenzake ??

Yote haya yanakuja kwa kukosa katiba na uchaguzi uliohuru Tz pamoja na kukosa mahakama zilizo huru ,
haya ndiyo mambo ya msingi kuliko hiyo bandari , na haya ndiyo ya Shivji anatakiwa kuyavalia njuga kwanza
 
mkataba ni haki yetu kuujuwa kama wananchi na ni haki yetu kukemea mikataba ovu yakifirauni yani ukomo wake haueleweki alafu bado tujione tupo salama apo.?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unakemea mkataba wakati hao walio madarakani wenyewe wameingia kifirauni , utegemee kitu gani ??
 
Sasa wale wabunge wakiongozwa na spika, ambaye ni mwanasheria nguli (km inavyo daiwa) hawakuona haya mambo? Hadi kupitisha kwa kishindo na harakaa??

Mbona inashangaza mnooo, khaaah

Na wala huyo Shivji hatujamsikia kusema chochote , pamoja na umafia wa Magufuli alioleta uozo wote huu
 
Atatokea mtu mmoja ameshiba mema ya nchi, anaitwa Malechela(kwa kujitia uzungu anajiandika Malecela) na kusema kuwa wanaopinga mradi hawana hoja.
 
Back
Top Bottom