Prof. Shivji: Mikataba ya Bandari na Dubai inayokuja itakuwa Siri na haitapelekwa Bungeni

Sasa revenue sharing iandikwe kwenye mkataba wa makubaliano ya nchi.Profesa yupo Sahihi kabisa, kifungu hicho hakipo.

Vifungu hivyo huwepo kwenye mkataba wa biashara, ambao haupo mpaka sasa, na hata ukiwepo, msitegemee kuwa mtauona. Never.

Jamani kwenye kila biashara kablata ya kuangaza maongezi kuna mkataba unaiwa "non disclosure agreement" ni lazima pande zote mbili muusaini huo kabla hamjaingia kweye maongezi ya kibiashara.

Mnafahamu maana yake nini huo mkataba wa mwanzo kabisa, kanla hata ya mkataba wa kibiashara haujaanza kuongelewa?


Hapo ama mleta mada hamuelewi lugha ya profesa Shivji au anapinda maneno.

Haki ya Mungu Tanzania watu wanakwenda shule kucheza mdako tu. Dah!


Mnataka Profesa awe clear vipi zaidi ya hivyo? Kuwa mkataba wa kuendesha bandari hamuwezi kuuona, wala bungeni hawatouona, tena mimi naongezea, hata wanaokwenda ku negotiate huo mkataba hamtowajuwa.
 

Katika uchambuzi wa Pro. Shivji umeona hilo tu?
Kwa nini muda wa ukomo haupo?
Kwa nini kwingine kusiendelezwe?
Kwa nini inatumika nguvu kubwa kuwaaminisha waTz
Kwa nini unajiondoa asipewe mkataba wa muda?
Kwa nini unajitia upofu huoni mapungufu hili jambo?
Kwa nini upande wa serikali haulezi mapungufu?
Kwa nini hamtaki kuwasikiliza wananchi?
Kwa nini kwa nini ni nyinigi?

Hii mikataba mingi ni ya hovyo mbayo kwa baadae huwa kuna kujuta mbeleni!
Mf: Huyo anaemaliza muda wake hapo bandarini hakuna tija unampa mwingine hiyo kazi ambae hutaki awe uko wo wote ndo nini hicho?
Mf: kwenye gesi huko faida sio leo!
 
Huwezi kuwa qanasheria na wataalaam washeria waliobobea halafu ukamsukumia mama mambo ya mikataba. Kwani wanasheria serikalini wanaajiriwa kwa sababu gani?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinhga?
Haya sasa, shakunywa matapishi mwenyewe!
Hovyo kabisa.

Usitafute kusukumiza lawama kwa watu wanaoshinikizwa tu wafanye anavyotaka mhusika.

Hili ni la Samia mwenyewe, na itabidi alinywe mwenyewe.
 
Katika hali kawaida, tungalitegemea hoja kama hizi zikiibuliwa katika mjadala uliokuwepo bungeni. Na pia katika majumuisho yao ya jumla ushauri ukitolewa kuhusu kubadilishwa kwa vipengele vyote vyenye ukakasi wa kisheria.

Badala yake Bunge lilendeshwa kiushabiki na kupiga vijembe watu maarufu waliojitokeza hadharani na kutoa maoni huku wakionyesha mashaka kuhusu mkataba huu. Nafikiri ni wakati sahihi kwa wabunge wetu kujipima wenyewe na kujitathimini kama wanatosha pale wanapoona uchambuzi wa kina na mahiri ukifanywa na wabobezi wa kisheria kuhusu kile walichokiazimia kuhusu mkataba huu.

Aidha ni wakati umefika kubadilishwa kwa sifa za mtu kuwa mbunge. Vigezo muhimu viwekwe vyenye kuzingatia uwezo wa kielimu, weledi, na kiutaalamu kwa wabunge wetu. Viwekwe vigezo vyenye kuzingatia uwezo wa mbunge kufanya uchambuzi wa masuala mbalimbali kwa kina, na kwa ajili ya mustakabali mpana wa nchi yetu.

Kwa kuwa upande wa Tanzania Bara hatuna Bunge letu, wala hatuwezi kujadili peke yetu maswala yasiyokuwa ya muungano bila ya kuwashirikisha watu wa upande wa Visiwani. Lakini kwa upande wao wana haki hiyo, basi ifike wakati Bunge la Tanganyika nalo likarudishwa kisheria, na hadhi ya nchi ya Tanganyika itambulike rasmi.

Bunge likae kama la JMT pale tu ambapo wizara zenye kugusa mauala ya muungano yanapojadiliwa. Lakini kwa masuala yasiyohuso muungano, wawakilishi kutoka upande wa visiwani wasihudhurie.

La sivyo, baadhi ya wabunge wa Tanzania Bara wachaguliwe ili nao wawe wanahudhiria vikao vyote vya Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Tanzania Visiwani ili kulinda maslahi ya Tanzania Bara ndani ya vikao vyake.
 
Wewe ulielewa ninazungumzia mikataba ipi ya gesi inayoshughulikiwa na serikali wakati huu?

Mambo ya gesi ndiyo leo tumeanza kuyashughulikia? Huwezi kutumia akili yako vizuri ikuelekeze kwenye jambo linalozungumziwa?
Wewe jibu swali kama huelewi sema tukuelekeze.
 
Shivj Mungu akubariki sana

Huyu mama ameamua kuingamiza TANGANYIKA
Abariki kweli, anawaambia ukweli bado hamumuelewi.


Mama anawaletea maendeleo hamna macho wala muono wa kuyaona.


Shivji yupo sahihi kanisa. Hamtoweza kuuona mkataba.

Wewe ukioneshwa mkataba wa biashara za watu utakusaidia nini? Kusoma kwenyewe mkataba hujuwi.
 
Uchambuzi makini kabisa, huyu hajajurupuka amekaa akasoma neno baada ya neno kisha kutoa maoni yake.

NB, labda hata watu wa serikali hawauelewi mkataba ila wanafata tu mkumbo!!

Wasomi wetu wote wanapaswa kujitokeza hadharani kufafanua utata na upuuzi uliopo ktk Mkataba maana walisomeshwa na nchi.
 
Tumeuzwa na mzanzibari ndugu zangu.

Mikataba ya miradi (project agreement) na nchi mwenyeji (host government) mikataba hii haitapelekwa bungeni wala haitawekwa hadharani kwa sababu ni siri. Mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari ) ulipelekwa bungeni kwasababu ni mkataba wa kimataifa lakini project agreement ni ya kibiashara hivyo ni confidential (siri). Watanzania hawatajua wameingia katika mkataba gani na kuna nini ndani ya mkataba na mkataba umesema nini" Prof. Issa Shivji
 
"Mkataba huu (wa bandari) unaegemea zaidi upande mmoja na pia hauna ukomo wa muda. Wajibu wote ni wajibu wa serikali ya Tanzania lakini haki zote ni haki za DP WORLD" Profesa Issa Shivji
wanaotetea mkataba huu mama ambao serikali ilisha-sign wanasema eti ukomo utakwekwa kwenye ile mikataba itakayofuata ambayo TPA yenyewe sasa itaingia na DP world.
 
Kifupi, Mama aliwabana TRA na TPA kwamba alitaka Tshs. Trillion 30 kwa mwaka (2.5 kwa mwezi) zitoke kwenye Bandari zote ili kupunguza utegemezi wetu kwa mabeberu, majamaa kwa uvivu wa kufikiri namna ya kuiendesha kwa ufanisi wakaona njia ya mkato ni kuiuza Bandari yetu kwa mwarabu. Hii ni aibu kubwa kwa taifa ambalo lina zaidi miaka 60 ya kujitawala kwake kushindwa kusimamia upakiaji, usafirishaji na upakuaji wa mizigo bandarini.
 
Hawa ndo wasomi Sasa.
 
"Watu waliokuwa wanasema mkataba wa bandari ni wa miaka 100 hawakuwa wanamaanisha moja kwa moja ni miaka 100, walichomaanisha ni kuwa mkataba huu ni wa muda mrefu. N"

Hapo juu [emoji115]ukimsoma profesa utagundua kapuyanga tangu lini kawa msemaji wa watu? Hao waliokuwa wanasema miaka 100 alikutana nao lini ikawa wakamwambia siyo 100 ni mida mrefu? Siasa mbaya imeingia
 
"Wajibu wote kwa serikali ya Tanganyika" ajabu "Haki zote kwa mwarabu" - Prof. Shivji.

Mkataba hauna ukomo, ajabu kuna wajinga wasio na adabu walioanza kujitutumua kusema tusubiri HGA!

Huu mkataba unaonesha wazi kabisa, kuna kitu kikubwa sana Samia alihongwa na mwarabu, akaona malipo yake aje kuzitoa sadaka bandari zetu watanganyika.

Samia ana nia ovu na Tanganyika.
 
si ndo wasomi wa siku hizi ,
 
Haya sasa, shakunywa matapishi mwenyewe!
Hovyo kabisa.

Usitafute kusukumiza lawama kwa watu wanaoshinikizwa tu wafanye anavyotaka mhusika.

Hili ni la Samia mwenyewe, na itabidi alinywe mwenyewe.
Mpuuzi huyu bibi foxy, kwani yeye samia haoni hizi kelele za watu walioamua kujitokeza kufafanua upuuzi uliopo

kama wanasheria wa nchi walishindwa kumwambia ukweli yeye sa100 kwann asisitishe kutokana na ufafanuzi unaotolewa na watu kama kina shivj? Atalinywa mwenywe wala msitake kusingizia watu wengine
 
inamaana wewe ulikuwa hufuatilii tangu vuguvugu limeanza la bandari , since day one!!? Uliyekurupuka ni wewe mkuu!!!
 
Sasa wale wabunge wakiongozwa na spika, ambaye ni mwanasheria nguli (km inavyo daiwa) hawakuona haya mambo? Hadi kupitisha kwa kishindo na harakaa??

Mbona inashangaza mnooo, khaaah
Wabunge maslahi....wabunge wote wakirudi 2025 Shangazi na Msukuma pia out ....
 
Yaani miaka 60 ya uhuru bado tunageuzwa kama chapati watanganyika kweli? hapana kwenye hili watusamehe wacha tuendelee na umaskini wetu ila Bandari ni mali ya watanganyika vizazi na vizazi vijavyo.

Yaani hili saga ni sawa na yule Mzee aliyetaka kuuza shamba mtoto wa miaka 6 akakimbia police kuweka pingamizi.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…