Prof Shivji: Nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba wa DP-World?

Baada ya hotuba ndefu nimenukuu haya machache kutoka kwa Prof Shivji juu ya nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba huu wa kinyonyaji wa DP- World. naandika kama anavyo sema:-

"Kwa ujumla kwa kuhitimisha, mkataba huu sisi wanasheria tunauita honoracy provitions na tukikubaliana hivyo je kuna njia gani ya kujitoa kwenye mkataba huu? Hii sitorudia kusema kwa sababu the destiny ilikuwa ni bunge kuto ridhia mkataba huu lakini kwa sasa na kwa busara zake bunge limeona mkataba huu unafaa na limesha uridhia.

Njia ya pili imependekezwa na chama cha wanasheria na Mzee Warioba, aliposema kwamba tuurekebishe mkataba huu na tufute vipengele vinavyo lalamikiwa. Je njia hii inawezekana? (haiwezekani!) kwa mkataba huu mshirika wako ni lazima akubali ndipo marekebisho yafanyike.

Kama alivyosema Bwana Richard (mzungumzaji aliyetangulia.) kwamba kama mshirika ananufaika na kifungu hiki hatoweza kukubali kurekebisha. Na hata ukisema anakubali je mkataba huo sasa baada ya kurekebishwa utarudi tena bungeni? kwa sababu huo ulio rekebishwa utakuwa haukupitishwa na Bunge!

Jambo jingine nilisikia kwenye clip kutoka kwa Dr. Slaa akisema kwamba kuna muda wa mwaka mmoja kujitoa akinukuu ibara ya tano ya mkataba huu. Nafikiri amekosea tafsiri ya jinsi alivyosoma mkataba huu, ibara ya 5 inasema tu kwamba kama katika muda wa miezi 12 baada ya kusainiwa kwa mkataba na endapo kama hawajakubaliana kupitia project agreement na negotiation, serikali ya Tanzania itakuwa na uwezo wa kutafuta proporsal sehemu nyingine, haisemi kabisa kujiondoa.

Njia ya tatu ya kuingia mahakamani kama wenasheria wengine walivyofanya hapa kuna matatizo. Kama tunavyojua mahakama zetu zinachukua muda mrefu sana kufanya maamuzi, pale kesi itakapo kuja kusikilizwa muda utakuwa umepita na wahusika watakuwa wamesha saini project agreements, mahakama itashindwa kufanya maamuzi ya haki baada ya muda huo kupita na kwakuwa uamuzi wake kwa kipindi hicho hautakuwa na maana yeyote ndivyo watakavyo sema.

Njia mojawapo sijui kama wenzangu wamefikiria hiyo, kwenda kufile case na kuomba inaction ili kuzuia serikali kusign any proporsal about agreement mpaka pale kesi ya msingi iwe imeamuliwa, inategemea kiasigani wataweza kuwasilisha hoja zao lakini kisheria inawezekana hiyo. Swali ni je, utakapoingia mahakamani utakuwa unachallenge nini? Huwezi ukachallenge mkataba (IGA) bali utakuwa unachallenge azimio la bunge kwamba ni unconstitutional kwasababu limeridhia mkataba ambao ni unconstitutional. Kwahiyo azimio la bunge liwe ni unconstitutional kwa kuridhia mkataba ambao ni unconstitutionala ihope itakuwa vizuri.

Njia nyingine ambayo inawezekana kabisa, Mheshimiwa waziri mkuu amesema watafanya amendment lakini kama nilivyosema haiwezekani. Bunge laweza kupitisha azimio kurevorke azimio lake la kwanza na bunge lina mamlaka sovereignity power ya ku unvoke it's status. Wabunge wanaweza sema baada ya kusikiliza wananchi wetu tumeona kuwa azimio hilo halikuwa sahihi na tunalifuta inawezekana kabisa na kama azimio likifutwa hakuna rectification na kama hakuna rectification mkataba umefutwa, sasa njia hii pekee inawezekana.

Ni kwa kiasigani wananchi wataweza kuwashinikiza wabunge wao kuwalazimisha wakae tena bungeni warevorke azimio hilo na kufunga huo mjadala inategemea na uwamuzi wao wananchi. Kusema kweli bunge haliko chini ya Dubai hata sheria za kimataifa haziwezi kuli zuia ndio maana ya sovereignity of parliament kwa hivyo uamuzi wa Bunge utaheshimiwa.

Jambo la mwisho kama ninavyopenda kusema kuhusu mchakato mzima wa ubinafsishaji. Kila mara ubinafsishaji unahalalishwa kwa kusema kwamba sisi kama serikali hatukuwa na tija katika uendeshaji wa shirika hili, hiki ni kisingizio na kimetumika kubinafsisha mashirika yaliyokuwa yanaleta faida, nani anataka shirika linalotia hasara? Kuna sekta nyeti katika uchumi huwezi kuweka mikononi mwa watu na bandari ni sekta nyeti mojawapo, huwezi kuiweka mikononi mwa watu kwa sababu mbalimbali.

Mali yetu yote tuna export kupitia bandari, madini yetu yote yanapitia bandarini, mali yote tunayoleta kutoka nje yetu na ya wengine inapitia bandari na mali zenyewe ni sensitive. Sasa huwezi kuweka hiyo bandari mikononi mwa private company bila ya wewe kuwa na control na all say power hujui wataforward nini kupitisha ama watafaidika nini na huwezi kuzuia.

Kama kuna tatizo la ufanisi ni bora kuajiri management kutoka nje, ingawa itakuwa chini yetu kama vile Dubai wanavyoajiri watu kutoka nje kwani lazima ubinafsishe? Na hii sio ukodishaji kama watu wanavyosema ni ubinafsishaji kwa sababu unaweka control mikononi mwa private company bila ushindani kinyume na katiba ya nchi.

Kwa upande wangu mi naona kuna sekta nyeti za uchumi ambazo ni lazima zibaki mikononi mwa serikali na bandari ni moja wapo, fedha ni muhimu na nishati ni yatatu. Unaweza kubinafsisha hoteli au maduka lakini sio bandari wala sekta ya fedha, hata ukiruhusu mabenki binafsi lakini ni lazima uwe na commercial bank ya serikali ni lazima." Amesema Prof Shivji kwenye mjadala huo.
kuna remot inaendesha nchi
 
Sababu kubwa ya Bandari yetu(zetu) kugawawiwa na wala siyo kuuzwa ninkugawa bure ni Kongo, na hilo liko juu ya Viongozi wote wa Tanzania, wanaochukuwa mali za Kongo wanaopiganisha Vita Kongo ili waibe rasilimali ndiyo wanaochukuwa pia Bandari zetu, muda utaongea na ndiyo hakuna kitu tutafanya, zimeshaenda hizo, sababu ni mali za Kongo na Serikali haitahusika na kitakachopita Bandarini ili isijulikane Mali zaKongo zinaenda wapi. Serikali haitajua nini kinaingia na kipi kinatoka.
Kwa kifupi kilichofanyika ni kama karne iliyopita foreign army wangetuvamia na ku seize Bandari yetu na kuweka military post kuirun Bandari kwa manufaa yao ila leo karne ya 21 hilo haliwezekani moja kwa moja wanatumia mbinu nyingine lkn matokeo ni yale yale.

Unafikiri timing ya Bandari kavu Kigali imetokea tu? Unganishaleni dots mtafika tu kwa mwenyewe, …
 
Njia nyingine ambayo inawezekana kabisa, Mheshimiwa waziri mkuu amesema watafanya amendment lakini kama nilivyosema haiwezekani. Bunge laweza kupitisha azimio kurevorke azimio lake la kwanza na bunge lina mamlaka sovereignity power ya ku unvoke it's status. Wabunge wanaweza sema baada ya kusikiliza wananchi wetu tumeona kuwa azimio hilo halikuwa sahihi na tunalifuta inawezekana kabisa na kama azimio likifutwa hakuna rectification na kama hakuna rectification mkataba umefutwa, sasa njia hii pekee inawezekana.
Tungeweza kutumia njia hii kujindoa kwenye mkataba huu, lakini kwa namna hawa wabunge wetu walivyopatikana inatia wasiwasi mkubwa.
 
Baada ya hotuba ndefu nimenukuu haya machache kutoka kwa Prof Shivji juu ya nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba huu wa kinyonyaji wa DP- World. naandika kama anavyo sema:-

"Kwa ujumla kwa kuhitimisha, mkataba huu sisi wanasheria tunauita honoracy provitions na tukikubaliana hivyo je kuna njia gani ya kujitoa kwenye mkataba huu? Hii sitorudia kusema kwa sababu the destiny ilikuwa ni bunge kuto ridhia mkataba huu lakini kwa sasa na kwa busara zake bunge limeona mkataba huu unafaa na limesha uridhia.

Njia ya pili imependekezwa na chama cha wanasheria na Mzee Warioba, aliposema kwamba tuurekebishe mkataba huu na tufute vipengele vinavyo lalamikiwa. Je njia hii inawezekana? (haiwezekani!) kwa mkataba huu mshirika wako ni lazima akubali ndipo marekebisho yafanyike.

Kama alivyosema Bwana Richard (mzungumzaji aliyetangulia.) kwamba kama mshirika ananufaika na kifungu hiki hatoweza kukubali kurekebisha. Na hata ukisema anakubali je mkataba huo sasa baada ya kurekebishwa utarudi tena bungeni? kwa sababu huo ulio rekebishwa utakuwa haukupitishwa na Bunge!

Jambo jingine nilisikia kwenye clip kutoka kwa Dr. Slaa akisema kwamba kuna muda wa mwaka mmoja kujitoa akinukuu ibara ya tano ya mkataba huu. Nafikiri amekosea tafsiri ya jinsi alivyosoma mkataba huu, ibara ya 5 inasema tu kwamba kama katika muda wa miezi 12 baada ya kusainiwa kwa mkataba na endapo kama hawajakubaliana kupitia project agreement na negotiation, serikali ya Tanzania itakuwa na uwezo wa kutafuta proporsal sehemu nyingine, haisemi kabisa kujiondoa.

Njia ya tatu ya kuingia mahakamani kama wenasheria wengine walivyofanya hapa kuna matatizo. Kama tunavyojua mahakama zetu zinachukua muda mrefu sana kufanya maamuzi, pale kesi itakapo kuja kusikilizwa muda utakuwa umepita na wahusika watakuwa wamesha saini project agreements, mahakama itashindwa kufanya maamuzi ya haki baada ya muda huo kupita na kwakuwa uamuzi wake kwa kipindi hicho hautakuwa na maana yeyote ndivyo watakavyo sema.

Njia mojawapo sijui kama wenzangu wamefikiria hiyo, kwenda kufile case na kuomba inaction ili kuzuia serikali kusign any proporsal about agreement mpaka pale kesi ya msingi iwe imeamuliwa, inategemea kiasigani wataweza kuwasilisha hoja zao lakini kisheria inawezekana hiyo. Swali ni je, utakapoingia mahakamani utakuwa unachallenge nini? Huwezi ukachallenge mkataba (IGA) bali utakuwa unachallenge azimio la bunge kwamba ni unconstitutional kwasababu limeridhia mkataba ambao ni unconstitutional. Kwahiyo azimio la bunge liwe ni unconstitutional kwa kuridhia mkataba ambao ni unconstitutionala ihope itakuwa vizuri.

Njia nyingine ambayo inawezekana kabisa, Mheshimiwa waziri mkuu amesema watafanya amendment lakini kama nilivyosema haiwezekani. Bunge laweza kupitisha azimio kurevorke azimio lake la kwanza na bunge lina mamlaka sovereignity power ya ku unvoke it's status. Wabunge wanaweza sema baada ya kusikiliza wananchi wetu tumeona kuwa azimio hilo halikuwa sahihi na tunalifuta inawezekana kabisa na kama azimio likifutwa hakuna rectification na kama hakuna rectification mkataba umefutwa, sasa njia hii pekee inawezekana.

Ni kwa kiasigani wananchi wataweza kuwashinikiza wabunge wao kuwalazimisha wakae tena bungeni warevorke azimio hilo na kufunga huo mjadala inategemea na uwamuzi wao wananchi. Kusema kweli bunge haliko chini ya Dubai hata sheria za kimataifa haziwezi kuli zuia ndio maana ya sovereignity of parliament kwa hivyo uamuzi wa Bunge utaheshimiwa.

Jambo la mwisho kama ninavyopenda kusema kuhusu mchakato mzima wa ubinafsishaji. Kila mara ubinafsishaji unahalalishwa kwa kusema kwamba sisi kama serikali hatukuwa na tija katika uendeshaji wa shirika hili, hiki ni kisingizio na kimetumika kubinafsisha mashirika yaliyokuwa yanaleta faida, nani anataka shirika linalotia hasara? Kuna sekta nyeti katika uchumi huwezi kuweka mikononi mwa watu na bandari ni sekta nyeti mojawapo, huwezi kuiweka mikononi mwa watu kwa sababu mbalimbali.

Mali yetu yote tuna export kupitia bandari, madini yetu yote yanapitia bandarini, mali yote tunayoleta kutoka nje yetu na ya wengine inapitia bandari na mali zenyewe ni sensitive. Sasa huwezi kuweka hiyo bandari mikononi mwa private company bila ya wewe kuwa na control na all say power hujui wataforward nini kupitisha ama watafaidika nini na huwezi kuzuia.

Kama kuna tatizo la ufanisi ni bora kuajiri management kutoka nje, ingawa itakuwa chini yetu kama vile Dubai wanavyoajiri watu kutoka nje kwani lazima ubinafsishe? Na hii sio ukodishaji kama watu wanavyosema ni ubinafsishaji kwa sababu unaweka control mikononi mwa private company bila ushindani kinyume na katiba ya nchi.

Kwa upande wangu mi naona kuna sekta nyeti za uchumi ambazo ni lazima zibaki mikononi mwa serikali na bandari ni moja wapo, fedha ni muhimu na nishati ni yatatu. Unaweza kubinafsisha hoteli au maduka lakini sio bandari wala sekta ya fedha, hata ukiruhusu mabenki binafsi lakini ni lazima uwe na commercial bank ya serikali ni lazima." Amesema Prof Shivji kwenye mjadala huo.
Njia nyingine ya kujitoa ni kuwaondoa madarakani viongozi wote waliohusika, na wapambe wote washughlikiwe kwa mujibu wa sheria.. bila upendeleo
 
Huyu mama ni muhimu akawa na Baraza la watu wenye akili wakamshauri tuwache kuhonga chawa Ili tuu kujiingiza kwenye matatizo ,kwa sasa sidhani kama tuna Imani na bunge maana hawatujali sisi kama wananchi CCM imefikia pabaya na hii ikifanyika waje na hoja kwenye uchaguzi 2025 ....#uchawanikansainayotutafunapolepole
Mama ana TISS,na ndiyo mshauri wa Mama kwenye kila Jambo! Au unazani Mama kuleta DP hana baraka za TISS!!??
 
Jambo moja la msingi alipaswa Rais ni kuwashughulikia wanasheria wote walio kuwa kwenye timu hii ya mkataba huu kwani ni Wahaini na wahujumu uchumi.
Mkuu, atawashughulikiaje wakati ziara ya kwenda huko Dubaï kwenyewe ilipangwa na wasaidizi wake?
Kumbuka safari mbili za kwenda Dubaï kimya kimya!. Bunge nalo badala ya kuisimamia vyema Seikali, limegeuka kuwa mtetezi.
 
Kila nikikaa na kufiri naona kabisa dalili zote za kuwa na dpw hapa Tanzania, hatuna namna zaidi ya kukubali kilicho tokea, ingawa kama wananchi wanauwezo mkubwa lakini hatufui dafu.

Silaha yetu ni kwenye sanduku la kura, maybe tujaribu hio 2025.
Sanduku la kura ni Mali ya ukoo wa panya, tafuta Njia ingine.
 
Bunge laweza kupitisha azimio kurevorke azimio lake la kwanza na bunge lina mamlaka sovereignity power ya ku unvoke it's status. Wabunge wanaweza sema baada ya kusikiliza wananchi wetu tumeona kuwa azimio hilo halikuwa sahihi na tunalifuta inawezekana kabisa na kama azimio likifutwa hakuna rectification na kama hakuna rectification mkataba umefutwa, sasa njia hii pekee inawezekana.

Hayo ni maneno kabisa ya nguli wa sheria anayeaminiwa duniani kote ! sasa nyie wa bunge jifanyeni hamuoni wakati mnaona kelele zinazoendelea, mkiziba masikio swala hili litakuja na sura mpya kabisa kwa wananchi mtambue hilo.
 
Back
Top Bottom