Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Huu muungano wetu Tz haueleweki na hauvunjiki sababu hauko Katika vitabu vinavyotaja aina tatu tu za muungano,Stroke umekuwa mshabiki wa hawa watu kwa muda mrefu. Haya ndiyo tumekuwa tukiyapinga na mnatuona hatuitendei haki serikali yetu, kwa kuwakosoa.
Mimi najiuliza hata hivyo vyombo vyetu vya dola vinamshauri nini chief wao ?!.
Muungano ni tatizo kubwa sana. Na hizi ni athari zake.
i.e Union ( mnavunja serikali zenu na kuunda moja), Federal ( mnaendelea na Serikali zenu na kuwa na Serikali kuu ya muungano) , Confederal ( mnaendelea na Serikali zenu na kuungana katika mambo flani kama kutumia currency moja etc ),
Nyerere asifiwe sana kwa akili kubwa ya kukurupuka na kuleta umaskini kwa kuanzisha ujamaa ideology ambayo hakuielewa na kutunga muungano usioeleweka!
Hizi issue zisizoeleweka za muungano ni unintended consequences za muungano wetu. Tunachojua ni kuwa Zenji ni koloni letu Bara basi na muungano hauvunjiki kwa maslahi ya nchi yasiyoweza kuwekwa hadharani.
Huwa sikubaliani na Nyerere kabisa kwa kuleta ujamaa , ideology isiyofaa na ya kijinga mno kwa nchi masikini ( nimesoma ujamaa na ubepari ulaya na nikaelewa kuliko alivyoelewa Nyerere) maana msingi wa ujamaa ni kufanya kazi pamoja na kugawana Mali na Kwa Asili binadamu ni selfish and they are of different personalities wengine hardworkers wengine wavivu huwezi kusema wakae chungu kimoja utaleta unyonyaji tu na kuambukizana uvivu na Tz hatuna utajiri wa kugawana labda tugawane umaskini! Karl Marx anasema kitu Cha kwanza kinachomsukuma mtu kufanya kazi ni kupata maslahi binafsi ya kiuchumi na hata kukiwa na mgogoro chanzo Kikuu anasema huwa ni maslahi , japo sociologist wengine kina Max Weber wanasema binadamu pia anasukumwa katika kazi au mambo yake na kutaka sifa, kutaka umaarufu, kutaka uongozi, kutaka kutawala wengine etc.
Msingi wa ubepari ni mtaji, individualism, juhudi binafsi, ujasiriamali, uwekezaji na kupata profit kubwa sasa badala ya kufundisha raia uwekezaji wanafundishwa ngonjera za kijinga za ujamaa na ushirika my foot!! Hakuna ushirika katika Asili ya binadamu Kila mtu hupambania nafsi yake na hiyo ni human nature ndio maana ufisadi hautaisha bila kunyonga wahusika! Ujamaa ni ideology ya kufikirika na nchi inatakiwa kuingia katika ujamaa baada ya kuwa tajiri kupitiliza japo pia jambo Hilo ni utopia, haliko practical maana itabidi uwanyang'anye matajiri Mali zao walizopambana kujaza uzigawe Kwa jamii ya watu maskini na wavivu.
Nchi huendelea kwa ukuaji mkubwa wa viwanda vya watu binafsi ( capitalism) wanaolipa Kodi ambayo serikali isiyo ya kifisadi hutumia kodi hiyo kujenga miundombinu Bora ya Barabara, umeme, maji, reli, Usalama, amani, demokrasia etc. Sijui Nyerere alisoma vitabu Gani maana kawalisha raia matango pori na hawakumshtukia mpaka siku aliyoaga!
Ila katika hili la muungano Mwalimu apewe Maua yake maana alikuwa sahihi japo sababu za huu muungano ukitaka kuzijua nenda kasome BA Political Science pale Mlimani humu jukwaani au Mtaani si mahali pake!