Prof Shivji: Nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba wa DP-World?

Prof Shivji: Nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba wa DP-World?

Nashangaa!!JWZT wapo kimya wamelala usingiz wa pono,hiv hawayaoni haya yanayoendelea?
 
Tujitoe tu kutoka kwenye mkataba huu HARAMU!! Ni bora tuwe na mgogoro kama walivyo Djibouti dhidi ya DP WORLD. Tukapambane Mahakamani
Kutoka haiwezekani sababu viongozi wakuu hawaoni shida.
 
Jambo moja la msingi alipaswa Rais ni kuwashughulikia wanasheria wote walio kuwa kwenye timu hii ya mkataba huu kwani ni Wahaini na wahujumu uchumi.
Unaamini yete raisi anaona kuna shida yotote?
 
Kuna watu wameshakula hela ndefu kwa mwarabu achomoki mtu endapo dp world watafungua kesi wanapeleka machawa kulala hotel nyota tano lazima wazitapike hela hizo walizovuta
Sasa watalipa wao walio lala huko [emoji2393][emoji294]hotel. Sisi itatuhusu nn??
 
Huyu mama ni muhimu akawa na Baraza la watu wenye akili wakamshauri tuwache kuhonga chawa Ili tuu kujiingiza kwenye matatizo ,kwa sasa sidhani kama tuna Imani na bunge maana hawatujali sisi kama wananchi CCM imefikia pabaya na hii ikifanyika waje na hoja kwenye uchaguzi 2025 ....#uchawanikansainayotutafunapolepole
Kwa nini unafikiri tatizo ni kukosa ushauri?
 
Unaamini yete raisi anaona kuna shida yotote?
Rais mwenyewe ni shida.

Wewe mtu anakwambia ukimpigia kura au usimpigie kura atashinda uchaguzi, hata haogopi wapiga kura wake angalau kwenye kipindi cha uchaguzi, atakosaje kuwa shida kwa wananchi?
 
Rais aliyepita alikuwa wa ajabu aliyepo sasa hivi anaweza kuwa wa ajabu zaidi. Nchi hii imegeuzwa maabara ya kujifunza kuongoza matokeo yake anayeongoza ni mwingine.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndiyo uigawe bandari kama mali iliyokuchosha ?!. Apishe wengine wenye ubunifu, siyo kuwarudisha watu utumwani.
Magu alipokua anawatumbua mkamuona ni Dikteta bora Mama wa Watu kaamua kuwauza utumwani mkajipange tena upya huko!!
 
Sikubaliani na mikataba ya kinyonyaji ila tusijidanganye kwamba magendo au madawa ya kulevya yalikua hayapiti bandarini ilihali ipo chini ya serikali.

Hapo TPA si ndio kulijaa rushwa Kila siku mara mizigo icheleweshwe, mara mizigo ipotee, mara watu wakwepe Kodi so as much as tunapinga mikataba ya kihuni ila tusidhani kuendelea kuendesha bandari kupitia TPA ndio itatuepusha na magendo kupita. TPA hawajawahi kuwa wasafi hata siku Moja so tusiwageuze Malaika humu ni Wezi pengine kuliko hao Dp world.
Kweli rushwa imekuwepo, hata wizi wa mafuta pia. Tatizo la huu mkataba, hata baadae akija rais mzalendo wa kutokomeza wizi, hataweza kuingilia shughuli za bandari.
 
Bunge laweza kupitisha azimio kurevorke azimio lake la kwanza na bunge lina mamlaka sovereignity power ya ku unvoke it's status. Wabunge wanaweza sema baada ya kusikiliza wananchi wetu tumeona kuwa azimio hilo halikuwa sahihi na tunalifuta inawezekana kabisa na kama azimio likifutwa hakuna rectification na kama hakuna rectification mkataba umefutwa, sasa njia hii pekee inawezekana.

Hayo ni maneno kabisa ya nguli wa sheria anayeaminiwa duniani kote ! sasa nyie wa bunge jifanyeni hamuoni wakati mnaona kelele zinazoendelea, mkiziba masikio swala hili litakuja na sura mpya kabisa kwa wananchi mtambue hilo.
Wabungee waufute huo mkataba haraka sanaa.
 
Kila nikikaa na kufiri naona kabisa dalili zote za kuwa na dpw hapa Tanzania, hatuna namna zaidi ya kukubali kilicho tokea, ingawa kama wananchi wanauwezo mkubwa lakini hatufui dafu.

Silaha yetu ni kwenye sanduku la kura, maybe tujaribu hio 2025.
Sanduku la kula litaiondoa dpword?, usiwe mjinga ndugu.acha siasa,toa mawazo tufanyaje ili kujiondoa dpword.
 
Kwenye sanduku la kura nako ni kugumu mkuu. Unakumbuka alichokifanya Magufuli mwaka 2020? CCM ikifika 2025 wanafanya vilevile. Nadhani njia rahisi ni kuasi na ikibidi hata tuwakaribshe IS na Wagner waje hapa nchini kutusaidia kuwang'oa hawa mbwa madarakani. Vinginevyo tutasubiri sana.
 
Sanduku la kula litaiondoa dpword?, usiwe mjinga ndugu.acha siasa,toa mawazo tufanyaje ili kujiondoa dpword.
Maana yangu ilikua kwamba tungeweza kushinikiza kwa maandamano na migomo hili swala lisiendelezwe na serikali, hilo kwetu wananchi hatuwezi!

Nikasema hatuna namna zaidi ya kukubali kilicho tokea, ila tunaweza kutoa adhabu ya kuwaondoa madarakani waliotuingiza huu mkenge kwa kupitia sanduku la kura.
 
Ndiyo uigawe bandari kama mali iliyokuchosha ?!. Apishe wengine wenye ubunifu, siyo kuwarudisha watu utumwani.
Wapi nimesema iuzwe? Nachosema hata hao TPA ni Wezi tu pengine kuliko dp world kwani nani hajui Hilo? Hata JPM aliwahi sema hakuna sehemu Ina rushwa na wizi kama TPA. Au Kila anayekosoa TPA basi automatically anataka Dp world? Be serious.
 
Maana yangu ilikua kwamba tungeweza kushinikiza kwa maandamano na migomo hili swala lisiendelezwe na serikali, hilo kwetu wananchi hatuwezi!

Nikasema hatuna namna zaidi ya kukubali kilicho tokea, ila tunaweza kutoa adhabu ya kuwaondoa madarakani waliotuingiza huu mkenge kwa kupitia sanduku la kura.
Unfortunately sanduku la kura halijawahi kuamua Rais labda kidogo wabunge.
 
Kweli rushwa imekuwepo, hata wizi wa mafuta pia. Tatizo la huu mkataba, hata baadae akija rais mzalendo wa kutokomeza wizi, hataweza kuingilia shughuli za bandari.
Lakini TPA ndio wamesababisha hili suala, hakuna ufanisi kiasi imetumika kama loophole kubinafsishwa. Na sio TPA angalia ATCL, TRA, TTCL kote huko ufanisi ni zero kabisa sijui taasisi zetu Zina shida gani. Ifike kipindi ajira za utumishi ziwe na KPI mtu asipofikia lengo automatically afukuzwe kazi au awe demoted bila hivyo watu ni business as usual maana wanajua hakuna wa kuwagusa.
 
Back
Top Bottom