Prof Shivji: Nini kifanyike ili kujitoa kwenye mkataba wa DP-World?

Huu muungano wetu Tz haueleweki na hauvunjiki sababu hauko Katika vitabu vinavyotaja aina tatu tu za muungano,
i.e Union ( mnavunja serikali zenu na kuunda moja), Federal ( mnaendelea na Serikali zenu na kuwa na Serikali kuu ya muungano) , Confederal ( mnaendelea na Serikali zenu na kuungana katika mambo flani kama kutumia currency moja etc ),

Nyerere asifiwe sana kwa akili kubwa ya kukurupuka na kuleta umaskini kwa kuanzisha ujamaa ideology ambayo hakuielewa na kutunga muungano usioeleweka!

Hizi issue zisizoeleweka za muungano ni unintended consequences za muungano wetu. Tunachojua ni kuwa Zenji ni koloni letu Bara basi na muungano hauvunjiki kwa maslahi ya nchi yasiyoweza kuwekwa hadharani.

Huwa sikubaliani na Nyerere kabisa kwa kuleta ujamaa , ideology isiyofaa na ya kijinga mno kwa nchi masikini ( nimesoma ujamaa na ubepari ulaya na nikaelewa kuliko alivyoelewa Nyerere) maana msingi wa ujamaa ni kufanya kazi pamoja na kugawana Mali na Kwa Asili binadamu ni selfish and they are of different personalities wengine hardworkers wengine wavivu huwezi kusema wakae chungu kimoja utaleta unyonyaji tu na kuambukizana uvivu na Tz hatuna utajiri wa kugawana labda tugawane umaskini! Karl Marx anasema kitu Cha kwanza kinachomsukuma mtu kufanya kazi ni kupata maslahi binafsi ya kiuchumi na hata kukiwa na mgogoro chanzo Kikuu anasema huwa ni maslahi , japo sociologist wengine kina Max Weber wanasema binadamu pia anasukumwa katika kazi au mambo yake na kutaka sifa, kutaka umaarufu, kutaka uongozi, kutaka kutawala wengine etc.

Msingi wa ubepari ni mtaji, individualism, juhudi binafsi, ujasiriamali, uwekezaji na kupata profit kubwa sasa badala ya kufundisha raia uwekezaji wanafundishwa ngonjera za kijinga za ujamaa na ushirika my foot!! Hakuna ushirika katika Asili ya binadamu Kila mtu hupambania nafsi yake na hiyo ni human nature ndio maana ufisadi hautaisha bila kunyonga wahusika! Ujamaa ni ideology ya kufikirika na nchi inatakiwa kuingia katika ujamaa baada ya kuwa tajiri kupitiliza japo pia jambo Hilo ni utopia, haliko practical maana itabidi uwanyang'anye matajiri Mali zao walizopambana kujaza uzigawe Kwa jamii ya watu maskini na wavivu.

Nchi huendelea kwa ukuaji mkubwa wa viwanda vya watu binafsi ( capitalism) wanaolipa Kodi ambayo serikali isiyo ya kifisadi hutumia kodi hiyo kujenga miundombinu Bora ya Barabara, umeme, maji, reli, Usalama, amani, demokrasia etc. Sijui Nyerere alisoma vitabu Gani maana kawalisha raia matango pori na hawakumshtukia mpaka siku aliyoaga!

Ila katika hili la muungano Mwalimu apewe Maua yake maana alikuwa sahihi japo sababu za huu muungano ukitaka kuzijua nenda kasome BA Political Science pale Mlimani humu jukwaani au Mtaani si mahali pake!
 
Jambo moja la msingi alipaswa Rais ni kuwashughulikia wanasheria wote walio kuwa kwenye timu hii ya mkataba huu kwani ni Wahaini na wahujumu uchumi.
Yeye mwenyewe ndio Payonia kwenye hilo hukumbuki Burj Khalifa waliweka Picha yake? Kwanza ata hivo ubavu wa kuwawajibisha hana. Ni mlenda mlenda tu.
 
WAPO WATU WAMEUMBWA KI TOFAUTI, WAZO LA KUMFIKIRIA MWINGINE HALIPO KABISA!, AKISHASHIBA YEYE IMETOSHA!
 
Baraza la mawaziri unalisingizia bure katika hili, hili suala la Bandari ni deal la mama na genge lake, mama anajua anachokifanya na huo mkataba ulivyo sasa ndio mama ametaka uwe hivyo.
 
Prof Shivji ni mtu mzima,

Anajua Watanzania tukifanya Regime change, utakuwa mwisho wa mkataba huo wanaodai hauvunjiki.

Kuvunja mkataba na DP World ni kuiondoa CCM madarakani Kwa maandamano, maana Kwa Sanduku la kura wanaiba.
 
Amani na Utulivu uko katika Risk ya juu sana.

Tubadili uongozi wa Nchi na mambo yatabadilika.
 
Mkuu hebu tudokezee kidogo japo hata kwa code (hiyo paragra ya mwisho)
 
Tutakuwa kitovu cha madawa ya kulevya, kwasababu yataingia bila ya sisi kuwa na uwezo wa kuzuia.
Sikubaliani na mikataba ya kinyonyaji ila tusijidanganye kwamba magendo au madawa ya kulevya yalikua hayapiti bandarini ilihali ipo chini ya serikali.

Hapo TPA si ndio kulijaa rushwa Kila siku mara mizigo icheleweshwe, mara mizigo ipotee, mara watu wakwepe Kodi so as much as tunapinga mikataba ya kihuni ila tusidhani kuendelea kuendesha bandari kupitia TPA ndio itatuepusha na magendo kupita. TPA hawajawahi kuwa wasafi hata siku Moja so tusiwageuze Malaika humu ni Wezi pengine kuliko hao Dp world.
 
Mbona mnawaamsha hawa? Waacheni wagongwe kwanza ili akili ikae vizuri, wao wana fikiri privatisation inaanzia awamu ya 6 , kumbe imemuweko miaka mingi tena kwa hasara.
 
Jambo moja la msingi alipaswa Rais ni kuwashughulikia wanasheria wote walio kuwa kwenye timu hii ya mkataba huu kwani ni Wahaini na wahujumu uchumi.
Wote wamo kwenye hilo dili la kuuza nchi.
Kuanzia mshughulika hadi washunghulikiwa wote lao moja.
Sijui itakuwaje
Ila hii ni aibu ya karne na vizazi vyote vijavyo havitaelewa kilitokea nini.
 
Ndiyo uigawe bandari kama mali iliyokuchosha ?!. Apishe wengine wenye ubunifu, siyo kuwarudisha watu utumwani.
 
Mbona mnawaamsha hawa? Waacheni wagongwe kwanza ili akili ikae vizuri, wao wana fikiri privatisation inaanzia awamu ya 6 , kumbe imemuweko miaka mingi tena kwa hasara.
Sisi ndiyo tutagongwa kwa msumari na kizazi kijacho wakati wao tayari wana fungu la kutosha kuishi maisha ya kifahari
 
Shivji hana uelewa wowote huyo mzee, waulize Lord denning na Faizafoxy wao ndio wajuz wa sheria kuhusu masuala yote ya mikataba na uelewa mpaka kuhusu foreign investors!! Over 🤣🤣🤣🤣
 
Jambo moja la msingi alipaswa Rais ni kuwashughulikia wanasheria wote walio kuwa kwenye timu hii ya mkataba huu kwani ni Wahaini na wahujumu uchumi.
Upo serious? Umewaza pande zote au upande mmoja tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…