Prof. Tibaijuka amshukia Wasira: "Kumshauri Rais kuangalia upya kesi ya Lissu, sio kuiamuru Mahakama"

Prof. Tibaijuka amshukia Wasira: "Kumshauri Rais kuangalia upya kesi ya Lissu, sio kuiamuru Mahakama"

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Tibaijuka.png

Profesa Anna Tibaijuka

Waziri wa zamani na mbunge mstaafu, Prof. Anna Tibaijuka, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, akisisitiza kuwa wanaodai Mheshimiwa Rais hawezi kuingilia au kutafuta ufumbuzi wa kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kwa sababu iko mahakamani "wanakosea na wanapotosha umma."

Soma zaidi: Wasira: Nilimwambia Prof Tibaijuka kuwa nchi lazima iendeshwe kwa mujubi wa sheria
Wasira.jpeg


Ametoa ufafanuzi huo kufuatia kauli za Wasira aliyenukuliwa akisema kuwa alimpigia simu Prof. Tibaijuka akimkosoa kuhusu ushauri wake kwa Rais Samia Suluhu Hassan alioutoa mapema Julai, akimwomba afute kesi inayomkabili Lissu.

Akizungumza katika mahojiano na DW, Julai 22, Wasira alisema kuwa Tanzania inaongozwa kwa mujibu wa sheria na Katiba, ambapo kuna mihili ya Bunge, Mahakama na Utawala ambayo haiingiliani.

Wasira alisema, kutokana na utaratibu huo, mhimili wa utawala hauwezi kuingilia mhimili wa mahakama.

Soma zaidi: Prof. Tibaijuka amshauri Rais Samia amwachilie Tundu Lissu

Hata hivyo, akiandika leo katika ukurasa wake wa X, Profesa Tibaijuka amekiri kuzungumza kwa simu na Wasira na walikubaliana kutokukubaliana kuhusu kesi ya Lissu, akieleza umuhimu jamii kuelimishwa na isiwe na mchanganyiko wa dhana kati ya uhuru wa Mahakama na wajibu wa Serikali.

"Mahakama zina wajibu wa kutoa maamuzi kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote, hata Rais. Huo ni msingi wa utawala wa sheria. Lakini ni Serikali kupitia vyombo vyake ndiyo huanzisha na kuendesha mashtaka ya jinai," alisema Prof. Tibaijuka.

Mamlaka ya Serikali kupitia upya mashitaka

Prof. Tibaijuka amebainisha kuwa katika nchi zinazofuata mfumo wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth), mamlaka ya mashtaka yana uwezo wa kupitia upya uamuzi wa kuendelea na shauri ikiwa maslahi ya umma au haki vinahitaji kufanya hivyo.

Amesisitiza kuwa kumshauri Rais ahimize Serikali yake kupitia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuangalia upya kesi zinazochukua muda mrefu au kuleta sintofahamu nchini, si sawa na kuiamuru Mahakama namna ya kuamua.

"Kusema vinginevyo ni kupotosha umma. Kuna wanaofanya hivyo kwa kutokujua, na kuna wanaofanya hivyo kwa hila ovu kama propaganda tu za upotoshaji. Tusichoke kuelimishana," aliongeza.

Yaliyosemwa na CMAG na Athari za Kesi
Prof. Tibaijuka amerejelea taarifa ya hivi karibuni ya Kamati ya Mawaziri wa Jumuiya ya Madola (CMAG), akibainisha kuwa haikuitaka Mahakama imwachie huru Lissu, bali ilishauri suala hilo lipatiwe ufumbuzi kupitia njia za kisiasa na kisheria.

"Hata katika demokrasia zilizoimarika, kuna wakati suluhisho la migogoro ya kisiasa hupatikana kwa kutumia taratibu halali za kisheria pamoja na busara za kisiasa. Ninaamini athari za kuendelea kumshikilia Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani kwa shtaka ambalo kwa mwaka mzima halijakamilika mahakamani haisaidii taifa hili hata kidogo."

Amesisitiza kuwa ushauri wake kwa Rais si shinikizo wala kuingilia Mahakama, bali ni ushauri wa unyenyekevu kwa uongozi wa Taifa ili kuliponya taifa, kujenga kuaminiana, na kuweka mazingira mazuri ya kupata Katiba Mpya.

"Mamlaka ya kuondoa shauri mahakamani iko chini ya Mheshimiwa Rais na Serikali yake kupitia ofisi ya DPP. Ni kwa kutambua hilo ninajielekeza moja kwa moja kwa Mhe. Rais," alisema Prof. Tibaijuka
 
Prof Tibaijuka, wewe ni professor, Wasira ni Chawa wa Samia na mganga njaa tu. Ndio maana kuna wakati alikimbilia upinzani, na alipoona hashibi huko akaomba kurudi CCM. Kubishana nae watu wanaweza wakadhani uwezo wako wa akili ni sawa na uwezo wa Wasira
 
Hakika Huyu mama ni Profesa Msomi.

Hapa ndio unaona Umuhimu wa Elimu.

Wasira ni Uzao wa Linyani
Sokwe.
Upumbavu umemjaa kichwa
 
Back
Top Bottom