QUOTE="Joe Milla, post: 55610775, member: 237095"]
Kama sijakosea kuna mtu aliwahi kushauri ili neno ' Vyama/chama kikuu cha upinzani' Si neno zuri sana kutumika hasa kwa nchi zetu sababu wengi neno 'MPINZANI' wakilisikia huwa wanalitafsiri au kulipa maana tofauti na zaidi ni kwa mlengo wa ubaya. Ndo Maana kuna kauli chama tawala wanasemaga kwamba "hawa Wapinzani wanapinga kila kitu".Sasa mtu akisikia kauli kama hii anahitimisha kwamba vyama vya upinzani wao kazi yao ni chuki na kutoona jema la chama tawala. Ni vyama/Chama kazi yake ni kukosoa mazuri,kuchochea chuki au uasi,si wazalendo, wako kuharibu amani ya nchi, wanatumika na mabeberu..yaan Ukiitwa kwa Neno ' Mpinzani' basi ni kama umbwa usiempenda unambandika jina baya tu. So, Mpinzani unabandikwa kila aina ya ubaya na unahalalishiwa uonevu wowote kutendwa kwako hata kamaa ulikuwa sahihi.
Huyo mtu alishauri litumike neno ' VYAMA/ CHAMA KIKUU SHINDANI' na si PINZANI maana halileti picha nzuri, upinzani ubaki kwenye Masumbwi huko😁😁Mtanirekebisha kama niko sahihi maana ni mda nilisoma sehemu hiyo hoja na mwandishi nishamsahau.
[/QUOTE]
Chama mbadala /vyama mbadala au shindani yote mazuri