MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Uelewa wako ni butu sana kutokana na mahaba ya kisiasa: Ethiopian Airlines hata wao wana ndege ambazo wanamiliki kwa kupitia mkataba wa matumizi (Aircraft Lease Agreement). Mwaka 2013 waliingia mkataba wa miaka 12 na Airlease Corporation kwa matumizi ya ndege 2 aina ya Boeing 777-300 ER. Unadhani kwanini hawakununua hizi ndege kwa pesa taslimu ???Eithiopia airline wanaponunua cash wao ni shirika binafsi?
South Afrika Airline wana ndege 8 kama sijakosea ambazo walinunua cash, je hao ni shirika binafsi?
South Africa Airlines wana mkataba (Dry Lease-Agreement) wa ndege 40 na mwaka jana walipanga kurudisha ndege 19 katika hizo ili wasaini mkataba mpya tena. Afrika Kusini wametuacha Tanzania mbali sana kiuchumi lakini bado wanaingia mikataba ya matumizi. Unadhani wao ni wajinga kufanya hivyo au hawana pesa ???
Halafu ni jambo la kipuuzi kutaka kufananisha mashirika ambayo yameanza miaka mingi iliyopita(South African Airline mwaka 1936 na Ethiopian Airlines 1946) na mpaka leo hii yapo, dhidi ya shirikina ambalo liko (Dormant) na liko katika hali ya kufufuliwa. Ethiopian Airlines, wao binafsi hawategemei safari za ndege pekee kama vyanzo vya mapato: Lakini hili shirika ni FULLY-AUTONOMOUS likifuata mwelekeo wa masoko na siyo siasa za WAJAMAA.
Haya leta jingine................