Profesa Assad: Wanaounga mkono kila kitu ni wasaka fursa

Profesa Assad: Wanaounga mkono kila kitu ni wasaka fursa

Sasa Prof. Assad alitaka na wenzie wamkazie shingo Jiwe kama yeye? ... kilichompa ujasiri yeye wenzie hawakuwa nacho!
TUANZE UPYA.

JAPO SOTE SASA TUNAONA UMUHIMU WA KATIBA MPYA ITAKAYOKUWA JUU YA RAIA WOTE WA JAMHURI YA MUUNGANO!
 

Saturday April 10 2021​


Profesa Assad: Wanaounga mkono kila kitu ni wasaka fursa

By Ephrahim Bahemu

IN SUMMARY​

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema watu wenye tabia ya kuunga mkono kila wakati ni wasaka fursa na hawana msaada wowote katika nchi.

Profesa Assad amesema hayo leo Jumamosi Aprili 10, 2021 katika uzinduzi wa mfululizo wa midahalo ya umma itakayokuwa ikiandaliwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM).

“Kuna watu waliunga mkono na sasa wanaunga mkono tena vitu ambavyo haviendani, hao ni wasaka fursa tu na kawaida yao hawatusaidii chochote, nchi inahitaji watu wenye fikra tunduzi ambao wakati ule walisema kitu kile na sasa wanasema vilevile na wataendelea kufanya mambo sahihi,” amesema Profesa Assad.

Msomi huyo alitolea mfano kutumbuliwa kwa watendaji bila hata kufuata sheria na haki za anayetumbuliwa akisema watu walishangilia na kulikuza na sasa hao hao wanashangilia mpaka leo wakati wanapaswa kukosoa mambo yanapokwenda kinyume.

Amesema ni jambo la kawada watu kuwa hivyo kwa kuwa binadamu wengi ni wasaka fursa, wanaangalia upepo unaendaje, "wakati ule walikuwa wanashadadia mambo yakifanywa hata bila kufuta taratibu za kisheria na sasa wanashadadia hata mambo ambayo yanatofautiana na yale."

Kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Profesa Assad amesema kuna haja ya Serikali kutoa nyaraka ya mradi huo kuiweka hadharani ili wananchi wasome, waangalie faida na hasara zake na watoe maoni yao kama ni mzuri au mbaya.

“Nashindwa kusema kama mradi ni mzuri au ni mbaya maana hiyo nyaraka sijaiona lakini Serikali ikitoa taarifa, ikaitoa Ikulu tutatoa maoni nami ni mzuri katika eneo hilo la uchambuzi,” amesema Profesa Assad.
 
Siyo kila mtu mwenye akili timamu lazima awe bungeni.
 
Alichosema Prof Assad ni sahihi, lakini hiyo “My take...” yako sio realistic. Professors karibu wote ni wazuri wakiwa nje kama watazamaji. Ukiwaingiza kwenye team ya utendaji, nao ni hopeless kama walivyo wengine ambao sio professors!
 
... sio kila aliyeko bungeni ana akili timamu.
Watu kama kina Assad kuwapeleka bungeni ni kwenda kuwapotezea muda tu.

Technocrats kama hao wanatakiwa kuwa kwenye decision making bodies kama taasisi za serikali badala ya kwenda kugonga meza
 
Nakubaliana na mawazo ya Professor Assad hasa hasa kuhusu watu kufikiri badala ya kwenda na upepo. Tunatakiwa kufikiri juu ya hoja zinäzöjadiliwa kwa kina na sio kuangalia ni nani anayetoaa hoja.

Kufuatana na definition ya corruption iliyotolewa na Assad, matumizi mabaya ya fedha za umma ni RUSHWA kama RUSHWA nyingine ni lazima kukemea. Unfortunately, Assad alipokuwa chairman wa Audit Committee ya NSSF wakati shirika likiongozwa na Ramadhan Dau, kulikuwa na mismanagement ya fedha nyingi sana na records zilionesha hivyo.

Binadamu wanabadilika maybe now Assad has transformed into a new person and the past is beyond him!
 
Kabisa lakini bado jiwe kwa kushirikiana na Ndugai wakatafuta sababu ya kumfuta kazi kwa kusema ukweli kwamba Bunge letu ni DHAIFU na ndiyo sababu kuna UOZO wa kutisha kuanzia Ikulu na kila sekta.

Badala ya Bunge kuisimamia ipasavyo sasa Bunge limekuwa kama ni kitengo cha maccm kuunga mkono kila kitu kwa kupiga ukelele wao wa kipuuzi ndiyooooooooooo!

Angalau yeye anashirikiana na ubongo wake kabla hajaongea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa lakini bado jiwe kwa kushirikiana na Ndugai wakatafuta sababu ya kumfuta kazi kwa kusema ukweli kwamba Bunge letu ni DHAIFU na ndiyo sababu kuna UOZO wa kutisha kuanzia Ikulu na kila sekta. Badala ya Bunge kuisimamia ipasavyo sasa Bunge limekuwa kama ni kitengo cha maccm kuunga mkono kila kitu kwa kupiga ukelele wao wa kipuuzi ndiyooooooooooo!
Halafu leo wanajifanya kushangaa taarifa ya CAG wakati [emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kujipendekeza kubaya sana kunapunguza uwezo wa kufikiri matokeo yake taifa linazidi kudumaa kimaendeleo, ila wao wanaona sifa.
 
Jamaa ni Smart upstairs! Watoto wa mjini wanasema Akili mingi!

Kihistoria madictator hupenda kuwaendesha wataaluma mfano ni kama Adolf Hitler na chama chake cha Nazi
 
Back
Top Bottom