Profesa Assad: Wanaounga mkono kila kitu ni wasaka fursa

Profesa Assad: Wanaounga mkono kila kitu ni wasaka fursa

Huyu Prof no m2 firm Sana na ndiye m2 pekee aliyempa jiwe wakati mgumu Mana alikuwa anasimamia utaalamu wake cjajua hao wengne Kama yye njaa wanaitoa wapi Hadi kuwa mazezeta.
 
Dar es Salaam, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema watu wenye tabia ya kuunga mkono kila wakati ni wasaka fursa na hawana msaada wowote katika nchi.

Profesa Assad amesema hayo leo Jumamosi Aprili 10, 2021 katika uzinduzi wa mfululizo wa midahalo ya umma itakayokuwa ikiandaliwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM).

“Kuna watu waliunga mkono na sasa wanaunga mkono tena vitu ambavyo haviendani, hao ni wasaka fursa tu na kawaida yao hawatusaidii chochote, nchi inahitaji watu wenye fikra tunduzi ambao wakati ule walisema kitu kile na sasa wanasema vilevile na wataendelea kufanya mambo sahihi,” amesema Profesa Assad.

Msomi huyo alitolea mfano kutumbuliwa kwa watendaji bila hata kufuata sheria na haki za anayetumbuliwa akisema watu walishangilia na kulikuza na sasa hao hao wanashangilia mpaka leo wakati wanapaswa kukosoa mambo yanapokwenda kinyume.

Amesema ni jambo la kawada watu kuwa hivyo kwa kuwa binadamu wengi ni wasaka fursa, wanaangalia upepo unaendaje, "wakati ule walikuwa wanashadadia mambo yakifanywa hata bila kufuta taratibu za kisheria na sasa wanashadadia hata mambo ambayo yanatofautiana na yale."

Kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Profesa Assad amesema kuna haja ya Serikali kutoa nyaraka ya mradi huo kuiweka hadharani ili wananchi wasome, waangalie faida na hasara zake na watoe maoni yao kama ni mzuri au mbaya.

“Nashindwa kusema kama mradi ni mzuri au ni mbaya maana hiyo nyaraka sijaiona lakini Serikali ikitoa taarifa, ikaitoa Ikulu tutatoa maoni nami ni mzuri katika eneo hilo la uchambuzi,” amesema Profesa Assad.

=====

My take: Tukiwa Na ma professa vichwa 10 tu kama huyu assad katika baraza la mawaziri na bungeni Basi tutatoboa...Asante Assad endelea kuwaelekeza.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Wewe umeacha kuunga mkono kila kitu?
 
Wewe umeacha kuunga mkono kila kitu?
Tulipoambiwa Mamv ni fisad tukaunga mkono,yule mwingine tukaambiwa ni kiongoz dhaifu tukaunga mkono,ilipotajwa list ya fisad tukaunga mkono,wale waliotajwa kwenye list ya mafisad walipokuja kwetu tuliwaunga mkono,yule shujaa wetu tulipoambiwa anapelekeshwa na mkewe tukaunga mkono,yule tuliyemnanga kuwa fisad alipokuja kwetu na kuwa mgombea tulimuunga mkono,hata sisi ni vigeugeu tunapaswa kujitafakar.
 
Namfahamu Asad kikamilifu. Yeye ni muumini mzuri wa imani yake lakini siyo mdini. Hajawahi kuonesha hilo akiwa lecturer UD wala akiwa CAG wala mahali pengine popote. Ni mtu mwema sana na asiye na makuu.

Mimi siyo muumini wa dini yake, lakini nathubutu kusema kuwa kama waumini wote tungekuwa waaminifu kwa imani zetu kama huyu bwana, Duniani pangekuwa mahali pema sana kwa kila mtu.
 
Back
Top Bottom