Profesa Assad: Wanaounga mkono kila kitu ni wasaka fursa

Halafu mzee kasema ndege ziuzwe nimefurahi sana sasa uchumi wa kenya kwenye ndege utaendelea kupaa wa tz mtusubiri
 
Utawala wa magu ulikua wa kitapeli na kikatili sana
 
Mbona ipo wazi haiwezekani kipindi cha Jpm ulikuwa unaunga mkono hoja, na sasa kipindi cha SSH pia ukawa unaunga mkono juhudi.
Maana wana mitazamo tofauti na ukiwa pande zoote wewe sawa tuuu mti wa muhogo mizizi inatumika na majani pia ni mboga.
Means huna uchaguzi
 
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema, watu wenye tabia ya kuunga mkono kila wakati ni wasaka fursa na hawana msaada wowote katika nchi. "Kuna watu waliunga mkono na sasa wanaunga mkono tena vitu ambavyo haviendani, ni wasaka fursa tu hao, hawatusaidii chochote.

Nchi inahitaji watu wenye fikra tunduzi ambao wakati ule walisema kitu kile na sasa wanasema vilevile na wataendelea kufanya mambo sahihi"Prof Mussa Assad CAG Mstaafu, Prof. Mussa Assad amesema msisitizo zaidi unatakiwa kuhakikisha wanasiasa hawawi kwenye bodi za wakurugenzi wa taasisi kama ambavyo utaratibu unataka.

Amesema katika moja ya taasisi alizowahi kuongoza, mbunge alikuwa mjumbe wa bodi, lakini hakuwa anachangia chochote "Ndiyo maana nasema tuanze upya tuanze na hao wachache ambao wanakwenda vizuri, hilo pia ni somo kwamba ambao nao 'in the future' (baadaye) watakuwa wa ovyoovyo, dawa yao hiyo ya kuwaweka kando na kuanza upya,"amesema Profesa Mussa Assad. "Viongozi wengi sio wazuri au hawakidhi kiwango kinachohitajika, tatizo langu ni moja tu inapofika mahali unaona mtu anakosea na huwezi kusema kama mtu anakosea, umefika mahali pabaya sana," Profesa Mussa Assad

Social-#MwananchiUpdates
 
Ex CAG Assad ni mtu mwenye kunyoosha rula, huwa hapindishi maneno, kwake "spade is a spade, and spoon is a spoon". Si mnafki na ni mtu ambaye husimamia kwa dhati kile ambacho yeye anaamini kuwa ni kitu sahihi. Kongole nyingi sana kwake.
 
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema, watu wenye tabia ya kuunga mkono kila wakati ni wasaka fursa na hawana msaada wowote katika nchi. "Kuna watu waliunga mkono na sasa wanaunga mkono tena vitu ambavyo haviendani, ni wasaka fursa tu hao, hawatusaidii chochote.

Nchi inahitaji watu wenye fikra tunduzi ambao wakati ule walisema kitu kile na sasa wanasema vilevile na wataendelea kufanya mambo sahihi"Prof Mussa Assad CAG Mstaafu, Prof. Mussa Assad amesema msisitizo zaidi unatakiwa kuhakikisha wanasiasa hawawi kwenye bodi za wakurugenzi wa taasisi kama ambavyo utaratibu unataka.

Amesema katika moja ya taasisi alizowahi kuongoza, mbunge alikuwa mjumbe wa bodi, lakini hakuwa anachangia chochote "Ndiyo maana nasema tuanze upya tuanze na hao wachache ambao wanakwenda vizuri, hilo pia ni somo kwamba ambao nao 'in the future' (baadaye) watakuwa wa ovyoovyo, dawa yao hiyo ya kuwaweka kando na kuanza upya,"amesema Profesa Mussa Assad. "Viongozi wengi sio wazuri au hawakidhi kiwango kinachohitajika, tatizo langu ni moja tu inapofika mahali unaona mtu anakosea na huwezi kusema kama mtu anakosea, umefika mahali pabaya sana," Profesa Mussa Assad

Social-#MwananchiUpdates
Huu ujumbe ni kwa Ndugai na genge lake
 
Back
Top Bottom