Mightier umesoma maoni haya ya huyu member? Hata mimi nakubaliana naye kwa asilimia zote. Nitafafanua: Siyo kwamba nakataa huko polisi au jeshini wasiajiriwe watu wenye uwezo mzuri wa kielimu, la hasha. Wasiwasi uko kwenye namna hizo division one zinavyopatikana. Sasa hivi kuna mashindano makubwa kati ya shule na shule, na mwanafunzi vs mwanafunzi ya kupata pass nzuri kwenye mitihani. Hili limefanya shule na wanafunzi wengi wagundue ''short-cut'' za kila aina ili kupata vyeti vyenye ufaulu mzuri. Hivyo kuajiri kwa kigezo cha ''huyu ana cheti kizuri'' bila kumpima kwa namna nyingine tutakuwa hatujatatua tatizo. Hivyo mimi naungana na mdau
Ultimate kuwa cheti kizuri kisiwe njia pekee ya kuamua. Siku hizi kuna njia nyingi mno za ku-test watu ili kujua uwezo wao. Tuchanganye njia mbali mbali.